Mkuu umejaribu kupita vituo vya BP ama Total leo? They are in the same boat.
Mkuu Roya Roy, jibu lako linapatikana kwa hii habari hapa chini.
Ewura sasa inatosha -Waziri
Waandishi Wetu
Daily News; Sunday,January 11, 2009 @21:15
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima amesema kama Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), imejikwaa mahali, itoe taarifa serikalini, lakini anaamini miaka miwili sasa tangu kuanza operesheni yake nchini, inatosha kuanza kuonyesha uwapo wake.
Sanjari na hilo, mamlaka hiyo imeonya kuwa kama kuna wafanyabiashara wanacheza mchezo mchafu ili mafuta ya petroli yaonekana yameadimika, sheria itachukua mkondo wake. Akizungumza jana ofisini kwake, Malima alisema yapo mambo ambayo Ewura bado inajifunza, lakini yapo mambo ambayo kimsingi, yanafaa kuchukua hatua.
Ewura inakua, kuna mambo tunaweza kuyaelewa kuwa ni mambo ya kujifunza, lakini mengine hapana
miaka miwili inatosha. Wakijikwaa, kwa sababu kujikwaa si jambo la aibu wala la ajabu, watoe taarifa kwetu, alisema Malima.
Alisema serikali itatumia sheria zake katika kuwabana wafanyabiashara wanaokiuka taratibu za biashara ya mafuta nchini, na kusababisha bidhaa hiyo iuzwe kwa bei ghali katika maeneo mengi nchini. Mara nyingi ninyi (waandishi wa habari) mnatuuliza sasa mtafanyaje? Tutatumia sheria zilizopo. Nondo zipo.
Ni mwendawazimu anayeweza kuamini kuwa nondo hazipo, lakini wakati mwingine serikali inatumia busara, aliongeza Malima. Aliwaonya wafanyabiashara hao kuwa wasije wakailaumu serikali mbele ya safari kwani inao uwezo wa kuwabana kwa kutumia sheria hizo zilizotungwa na Bunge, ikiwamo Sheria ya Mafuta ya 2008 iliyopitishwa bungeni Aprili mwaka jana.
Wakati Naibu Waziri akitoa msimamo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu ameonya kuwa wafanyabiashara wanaodanganya kuwa kuna uhaba wa petroli nchini, wanajitafutia matatizo. Akizungumza kwa simu jana baada ya Jiji la Dar es Salaam kushuhudia upungufu wa petroli, Masebu alisema hilo si tatizo kubwa kwani wanafahamu Kampuni ya GAPCO inayo mafuta mengi, lakini pia meli zaidi zilitarajiwa kutia nanga jana jioni.
GAPCO wanayo mafuta ya kutosha na meli nyingine zinaingia leo (jana). Hata huo upungufu hauwezi kubadili bei, na wala hauwezi kutokea upungufu kama ule wa mikoa ya Iringa na Morogoro, alisema na kuongeza: Tumefuatilia hali hiyo na hakika tutawashughulikia kisheria wale wote wanaotaka kuanzisha tatizo ambalo halipo.
Gazeti hili lilitembelea vituo mbalimbali vinavyouza petroli jana na kukuta hakuna huku mafuta ya taa na dizeli yakiendelea kuuzwa kama kawaida. Miongoni mwa vituo maarufu vinavyouza petroli ambavyo vimekutwa havina bidhaa hiyo ni pamoja na BP, Oryx, Total, Engen, Oilcom huku vituo vya Kampuni ya Gapco vikionekana kuuza bidhaa hiyo kama kawaida.
Licha ya petroli kutopatikana katika vituo hivyo tangu Ijumaa jioni, mabango katika vituo hivyo yameendelea kuonyesha bidhaa hiyo inauzwa kwa Sh 1,233 kwa lita moja bei halali iliyotangazwa na Ewura. Wakizungumza na gazeti hili, wafanyakazi wa vituo vilivyokutwa kutokuwa na petroli, walidai mafuta hayo hakuna katika hifadhi kuu za kampuni zao.
Mafuta si kwetu tu hata depot ya BP hakuna na ndio sababu unaona tunauza dizeli na mafuta ya taa pekee, alisema mfanyakazi wa Kituo cha BP Fire. Wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wamedai mahitaji ya petroli nchini ni makubwa kuliko dizeli na mafuta ya taa na ndiyo sababu yanamalizika mapema.