Hayo mabomba baadae yatafanya kitunguu kuharibika(kwasu) yani yanashuka had I ndani ya kitunguu na ukivunq kitunguu lile bombs linakauka hata upikeje haliivi
Kwa kawaida vitunguu hutoa maua mwaka wa pili wa maisha yake. Usipovivuna ule mwaka wa kwanza ukaendelea kuvitunza na hali ya hewa ikiwa nzuri vitatoa maua mwaka wa pili na kuzalisha mbegu.
Kwa hiyo vitunguu havipaswi kutoa mabomba (bolting) na hatimaye maua katika msimu wa kwanza. Vikifanya hivyo jua kuna tatizo.
Kwa nini vitunguu hutoa mabomba(flower stalks) katika msimu wa kwanza?
Kuna sababu 2: Joto kali au baridi kali.
Mmea wa kitunguu unapokabiliwa na hali ngumu- kutokana na joto au baridi- kwa jinsi ulivyoumbwa "hupata hofu" kuwa utakufa bila kuacha watoto! Kwa hiyo haraka haraka huanza kutengeneza maua hatimaye mbegu ili uweze kuacha uzao kabla haujafa. Jinsi ya kupunguza tatizo la kutoa mabomba
*Kama kuna hali ya joto ni muhimu kumwagilia vitunguu ili kupunguza joto na kuvipa maji ya kutosha ili visihisi kuwa kuna tatizo.
*Kama ni baridi kwa kweli hapa huna la kufanya labda ukwepe msimu wa baridi kali kabla hujapanda. Lakini kama hali ya baridi itatokea bila kutarajia basi hakuna jinsi.
Ili kuepuka hali mbaya ya hewa unaweza kuwekeza kwenye kilimo cha green house.
Kama vitunguu vimetoa mabomba yaondoe mapema maana bila hivyo chakula chote kitaelekezwa kwenye maua na mbegu(watoto).
Vitunguu vilivyotoa mabomba havifai kuhifadhi kwani vinaharibika haraka kwa hiyo vivune na kula/kuuza mara moja
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.