Vituko; Wauwaji wa Mtalii walikamatwa ndani ya 24 hrs kwann Olimboka inaenda wiki?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Hapa ndo nazidi kuitia mashaka serikali ya CCM hivi mbona haingii akilini?

Mtalii aliuwawa serengeti serikali ikahamia serengeti na wauwaji wakakamatwa ndani ya masaa 24

Kwa Dr. Olimboka tunaenda kuimaliza wiki bado kimyaaa hata wale watu wawili aliokuwa nao siku ya tukio hatujawasikia kunani ndani ya kapuuuuuuu?
 
kila mdau wa haki za binadamu anashangaa, lini mtuhumiwa akajichunguza mwenyewe ategemewe kutenda haki?ni nani anaweza kujichoma kisu tumboni, wakati anajua maumivu yake?hakuna asiyefahamu kuwa sumu huwa haionjwi.haiwezekani serikali ijipake kinyesi, maanake ikifanya hivyo ni lazima ipigiwe kura ya maoni ya kutakuwa na imani nayo.Kumbuka, serikali hii hii, ilisaini mkataba na kuridhia uhifadhi wa haki za binadamu .Hivyo kuwatambua na kusema hadharani waliofanya hivyo, ni serikali kujiondoa madarakani.Asilani ,serikali haitafanya hivyo , na kama itafanya hivyo, itakuwa kiini macho, taarifa yake haitakuwa ya kweli.dawa ya uchunguzi huu ni kuunda tume huru.
 
Hata wale walioua pale Igunga, waliokata wabunge pale Mwanza bado............waliomwekea sumu mwakyembe bado pia.......hata walioua na Zombe mahakama iliamuru kuwa akatafute muuaji halisi bado.
 
Kwa jinsi nionavyo mimi hakutakuwa na tamko lolote la serikali juu ya yaliyomkuta Dr. Uli, ila njama zao za kummalizia zikifanikiwa hapo watatoa tamko na tume yao kufanya kazi, kwani wenyewe wanajua kazi iliyopo ya kufanya uchunguzi wakati mtu aliyefanyiwa unyama na wao wenyewe serikali yupo hai.
 
Kwa hili la Ulimboka nasubiria sijui serikali itakuja na "SINGO" ipi.Kuna mambo yanakera sana nchi hii
 
Hata wale walioua pale Igunga, waliokata wabunge pale Mwanza bado............waliomwekea sumu mwakyembe bado pia.......hata walioua na Zombe mahakama iliamuru kuwa akatafute muuaji halisi bado.
Hii serikali ni chinjachinja na kikubwa ni matumizi mabaya ya usalama wa Taifa na vyombo vya Dola.
 
Hii serikali ni chinjachinja na kikubwa ni matumizi mabaya ya usalama wa Taifa na vyombo vya Dola.

Hao wanaojiita kwenye blue hapo wamebaki jina tu siku hizi, kwa wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa hao jamaa walikuwa wazalendo enzi za Nyerere.Hata kama kulikuwa na mapungufu lakini walijitahidi kupambana na waliotumia madaraka vibaya.
 
Back
Top Bottom