Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

Kuanzia katikati ya miaka ya sitini hadi mwishoni mwa miaka ya tisini katika mji Mwanza aliishi kigagula mmoja ambae alijulikana kwa jina la Bibi Fisi.

Bibi Fisi alikuwa mchawi hatari sana ambae sifa zake zilitikisa mkoa wote wa Mwanza na.mikoa jirani ya kanda ya ziwa..

Kigagula huyu inasemekana alikuwa na nguvu kubwa sana za kichawi na inasemekana kuwa alikuwa mmoja kati ya wachawi waliokuwa katika ranks za juu kabisa katika ufalme wa kichawi wenye makao yake makuu katika mkoa wa Shinyanga ( now Bariadi) katika eneo ambalo linajulikana kama Gamboshi ( ile isiyo onekana )

Pia inadaiwa kwa nguvu na uwezo wake mkubwa katika fani ya uchawi hakukuwa na mchawi yoyote nchini Tanzania ambae alikuwa na uwezo kama wa kwake.

Chanzo cha Bibi huyu kuitwa Bibi Fisi ni kwamba alikuwa ana kibanda ( nyumba ) yake katika eneo la Bugando jijini Mwanza.. Kibanda cha bibi huyu kilikuwa pembeni ya barabara.

Serikali ya Mwl Julius Kambarage Nyerere ilitaka kupanua barabara na moja kati ya nyumba ambazo zilitakiwa kubomolewa ni pamoja na nyumba yake.

Bibi huyu aligoma kuondoka katika kibanda chake kupisha upanuzi wa barabara..

Watu wa Halmashauri ya mji wa Mwanza hawakuwa na jinsi zaidi ya kufanya maamuzi ya kuvunja nyumba yake ..

Licha ya sifa za kutisha za bibi huyu lakini watu wa Halmashauri ya mji wa Mwanza walifikia uamuzi mgumu wa kuvunja nyumba ya bibi Fisi kwa kuhofia kuwajibishwa na mwalimu ( Viongozi wa Halmashauri mnaanzaje kuwambia Mwalimu kwamba kuna bibi kizee amegoma nyumba yake kuvunjwa na sisi tumeshindwa kutumia nguvu kwa sababu tunaogopa anaweza kuturoga )

Hakuna dereva aliye kuwa tayari kuendesha Grader ili kuvunja nyumba ya Bibi Fisi..Kila dereva aliyefuatwa aligoma ..

Watu wa Halmashauri wakafikia muafaka wawatumie wafungwa walio kuwa wamehukumiwa kunyongwa ambao walikuwa wanasubiria adhabu yao katika gereza la Butimba lililopo kusini mwa jiji la Mwanza..

SIKU YA KUVUNJA NYUMBA YA BIBI FISI

Inasimuliwa kwamba madereva walipoenda kuvunja nyumba ya bibi huyo nyumba ilitoweka na kitokea Fisi wengi sana katika eneo hilo hali iliyozua taharuki kubwa kwa wakazi wa maeneo ya Bugando,Bugarika,Igogo na mji wote wa Mwanza kwa ujumla.

Wengine wanasema Bibi huyu aliitwa Bibi Fisi kwa sababu alikuwa anafuga Fisi kwa ajili ya shughuli zake za ulozi na uchawi.

Tukio hili la bibi Fisi liliwatisha sana viongozi wa mji wa Mwanza ambao waliamua kumtaarifu Mwalimu.

Inasemekana Mwalimu alienda hadi nyumbani Kwa bibi huyu kwa ajili ya kuongea NAE na kumsihi akubali kupisha upanuzi wa barabara katika eneo hilo na kwamba serikali itamjengea nyumba nyingine nzuri katika eneo ambalo bibi huyo atalichagua mwenyewe lakini bibi Fisi alikataa kata kata kwa madai kwamba lile ni eneo ambalo amerithi Kwa mabibi na mababu zake na kwamba makaburi ya mabibi na mababu zake wote yapo katika eneo hilo na kwamba hawezi kuwakosea heshima wazee wake kwa kuliacha eneo hilo..

Mwalimu Nyerere kwa kuwa aliheshimu sana imani za watu hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na bibi huyo..

Hatimae upanuzi wa barabara ukampisha yeye na sio yeye kupisha upanuzi wa barabara.

Bibi huyu inasemekana alikuwa na utajiri mkubwa sana ambao hata hivyo ulikuwa hauonekani kwa macho ya nyama .

Chanzo cha utajiri wake inasemekana ilikuwa ni misukule.

Bibi huyu alikuwa anawauza misukule wake kwa wafanyabiashara wakubwa wa kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla.

Wateja wake wakuu inasemekana walikuwa wafanya biashara wa kihindi.

Watu wengi waliogopa kupita peke yao karibu na nyumbani kwa bibi huyu na ilikuwa ikifika usiku basi watu walikuwa hawapiti kabisa katika eneo hilo..

Inasemekana pia ilikuwa ukiingia kwenye kibanda chake unakutana na mjengo mmoja wa hatari sana .

Karibu na nyumbani kwake bibi huyu alikuwa na shamba la kama robo heka ambalo lilikuwa na mazao karibu wakati wote wa mwaka..

Bibi huyu alikuwa na maajabu sana. Mwaka 1983 kuna watoto walikuwa wakisoma katika shule ya msingi Mlimani ambayo haipo mbali sana na mahali ilipo nyumba ya bibi Fisi

..Watoto hao wa shule wakati wakati wanarudi makwao walipita nyumbani kwa bibi Fisi na kwenda kuiba maembe kwenye mti wa maembe ulio kuwa katika shamba la bibi huyo.

Bibi huyo inasemekana aliwafuata watoto hao hadi nyumbani kwa Wazazi wao kila mmoja kwa wakati wake lakini ndani ya muda huo huo.

Alipofika majumbani kwa watoto hao aliwasemelezea kwa wazazi wao kwa kuwataja majina yao kamili.

.Watoto hao waliishi katika eneo la Igogo..

Wazazi walishangaa sana bibi huyo amejuaje majina ya watoto wao na amefikaje nyumbani kwao kwa sababu watoto wakati wanachapwa bakora walisema bibi aliwakuta wakiwa wanachuma maembe na walipomuona walikimbia mbio.

KIFO CHAKE : Bibi Fisi alikufa kwa kuuwawa na watu wanao sadikiwa kuwa majambazi mwaka 2000 akiwa na umri unaokadiriwa 100 na zaidi..On the fateful day MWILI usio kuwa na uhai ( Lifeless body )wa bibi Fisi ulikutwa chumbani kwake ukiwa umekatwakatwa mapanga
Mimi nimesoma Mwanza miaka ya 86-89 na hii nyumba nilishawhi kuiona kwa macho yangu. Ni kweli
 
Bibi fisi ni true story na kwa mwanza alikuwa hana mpinzani kwa zama zile.

Nilishaingiaga kwenye kisanga na Bibi Fisi live.. Mbele ya nyumba yake kulikuwa na kauwanja kakulazimisha ka watoto watukutu wa Bugando kuchezeapo mpira wa miguu ule chandimu.. Sasa nakumbuka tulitoka shule tukaenda kuchezea pale na watoto wa Bugando. Bahati mbaya mpira ukapigwa ukaingia ndani ya kajumba ka Bibi fisi then dogo mmoja wa Bugando akaingiamo kufuata mpira, tulisubiri pale nje dogo atoke hadi saa moja jioni tukaamua twende kwao kuwataarifu wazazi wake.. Nao wakachanganyikiwa maana wanamjua yule bibi ni kigagula wa jiji zima na huwa hapendi watoto wachezee mpira mbele ya kale kajumba kake. Waliangahika usiku mzima... Kajumba mlango huko wazi hadi saa 12 za usiku lakini hakuna aliethubutu kuingia kipumbavu..Ukiangalia Giza na hakuna kelele yeyote ile ilhali na dogo yumo mule ndani. Hadi usiku wa manane walimfuata mzee mmoja nae alikuwa ana mambo ya kigagula ndo akaingia wakayajenga na Bibi then dogo akaachiwa kama usiku wa manane sisi watoto tushasepa makwetu then baada ya muda kupita tukaonana na dogo kwenye mpira tukamuuliza vipi uliona nini mule... Dogo anakwambia acha tu.. Ukiwa nje unaona ka nyumba kadogo ila ndani ni pakubwa sana na kuna watu wengi sana.

Bibi alikuwa na mengi sana Mimi ni miongoni mwa watu waliomfaidi sana Bibi.
Ananitamanisha huyu yaani natamani angekuwa hadi leo halafu mimi ningeenda nikaingia nyumbani kwake na kufanya ninachotaka, nikwa na smartphone ambayao ina BIBLIA TU!
 
Umesahau kitu.. naongezea wakati wa Vita vya Kagera inasemekana Bibi fisi ndo alichengesha Rada za Nduli Idd Amin alie taka kuipiga Bugando Hosptal na lile Bomu kwenda kuangukia jirani na chuo cha Bitimba (hadi leo mabaki ya lile Bomu yapo pale Chuo cha Ualimu Butimba) na ndio chanzo cha mwalimu Nyerere kuona Bibi ana heshima kuliko Barabara na ndo maana Barabara ilipinda kukwepa nyumba ya Bibi.. Nia ya Iddi Amin kuipiga Bugando ili wanajeshi na wote waliopata majereha ya kivita wakose huduma za matibabu.
Inasemekana Rada ya Idd Amin alipima vizur mara ya kwanza akaseti mitambo, mara ya pili alivyo pima ili aandae mabomu akaona pale alipo pima kuna uwanja tu na milima (watu wanasema Bugando hospital ilipotea kukawa na fisi tu ndo wanaonekana hapo). Nduli ikabidi apime upya baada ya kupotezwa na Bibi ndo akaona gereza kule na taa zikamchanganya akaachia kombora.. and it was a wrong direction.. story hii nilipewa na mlinzi wa Nyerere..
Inawezekana mkuu Yule bibi hakuwa wa mchezo mchezo.. Anyways Iddi Amin alipiga hilo kombora akiwa wapi ? Uganda au Kagera? By that time Uganda walikuwa na uwezo wa kurusha kombora kutoka Uganda hadi Mwanza?
 
Kifo kina nguvu kuliko uchawi ..Kifo kilimtaka..Hakukuwa na jinsi wala namna yoyote ile..she had to die

Uchawi ni mabaki ya ujinga wa jamii za kijima na woga wa pamoja katika watu wanaopenda kuendekeza majibu rahisi kwa maswali wasiyoyaelewa.
 
Uchawi ni mabaki ya ujinga wa jamii za kijima na woga wa pamoja katika watu wanaopenda kuendekeza majibu rahisi kwa maswali wasiyoyaelewa.
Uchawi upo mkuu na unafanya kazi sana tu
 
Kwa hoja isiyojipinga kimantiki, inayoweza kupimwa, inayiweza kutabiribmambo na inayiweza kusimama baada ya uchunguzi thabiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchawi ni sayansi..Sayansi ya siri.Sayansi isiyo onekana kwa macho.. Hawezi kuthibitishwa kwa hoja.Inathibitishwa kwa vitendo
 
Back
Top Bottom