Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

Kipindi hicho ndpo ule mtindo wa kuua vikongwe ulipoanza,,, kule mwanza vikongwe wengi walio kuwa wanahisiwa kuwa ni wachawi walianza kukatwa mapanga.. Bibi fisi pia alikutwa na hlo timbwili...
Ni kweli kabisa hata mm Nyumba yake niliiona Kwa macho yangu, na hata baada Ya kuuawa, nyumba yake ilikaa muda bila Wale vijana wezi wa igogo kuja kuchukua chochote.. Ilianguka yenyewe na hakuna hata aliye chukua bati... Na kweli sehemu hyo wakati wanaweka lami, barabara iliikwepa hyo nyumba yake.


Hilo eneo lipoje sasa? maana na kuuwawa lazima mizimu yake itawasumbua wenyeji.
 
Bibi fisi ni true story na kwa mwanza alikuwa hana mpinzani kwa zama zile.

Nilishaingiaga kwenye kisanga na Bibi Fisi live.. Mbele ya nyumba yake kulikuwa na kauwanja kakulazimisha ka watoto watukutu wa Bugando kuchezeapo mpira wa miguu ule chandimu.. Sasa nakumbuka tulitoka shule tukaenda kuchezea pale na watoto wa Bugando. Bahati mbaya mpira ukapigwa ukaingia ndani ya kajumba ka Bibi fisi then dogo mmoja wa Bugando akaingiamo kufuata mpira, tulisubiri pale nje dogo atoke hadi saa moja jioni tukaamua twende kwao kuwataarifu wazazi wake.. Nao wakachanganyikiwa maana wanamjua yule bibi ni kigagula wa jiji zima na huwa hapendi watoto wachezee mpira mbele ya kale kajumba kake. Waliangahika usiku mzima... Kajumba mlango huko wazi hadi saa 12 za usiku lakini hakuna aliethubutu kuingia kipumbavu..Ukiangalia Giza na hakuna kelele yeyote ile ilhali na dogo yumo mule ndani. Hadi usiku wa manane walimfuata mzee mmoja nae alikuwa ana mambo ya kigagula ndo akaingia wakayajenga na Bibi then dogo akaachiwa kama usiku wa manane sisi watoto tushasepa makwetu then baada ya muda kupita tukaonana na dogo kwenye mpira tukamuuliza vipi uliona nini mule... Dogo anakwambia acha tu.. Ukiwa nje unaona ka nyumba kadogo ila ndani ni pakubwa sana na kuna watu wengi sana.

Bibi alikuwa na mengi sana Mimi ni miongoni mwa watu waliomfaidi sana Bibi.
 
Back
Top Bottom