Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

Mhindi alikufa kwa ajali ya ndege aliitwa Ragu kiwanja aliuziwa na Baba yangu,ajab Baba yangu alikuwa anaiva na Bibi Fisi mpaka huwa naona kama uzushi tushacheza sana maeneo hayo.
Huyo bibi Fisi habari zake tulikuwaga tunazisikia hadi mjini daslamu miaka ya tisini hiyo. Walikuwaga wanasema ndio mkuu wa wachawi wote Tanzania nzima kuna mechi Yanga waliwahi kufungwa na Pamba ya Mwanza zikaja story kwamba Pamba mganga wao ni Bibi Fisi na kwamba ana ziwa moja wachezaji wakinywa maziwa yake hamuwafungi siku hiyo
 
N
Mleta mada umenikumbusha mbali .
Hiyo story ni ya ukweli .
Mimi nilikuwa naishi jirani na huyo bibi wakati tunaishi kwenye nyumba za Railway & Marine .
Huyo bibi nimemshuhudia kwa macho yangu kwa miaka mingi .
Nyumba yake ndogo ya tope iliyokuwa inaonesha ingeanguka wakati wowote ilikuwa katikati ya nyumba za watu wa tabaka la kati na matajiri . Fikiria upande wa juu wa nyumba yake kulikuwa na nyumba ya Ubalozi mdogo wa Uganda , upande mwingine ni wa pembeni kuna fence na shamba zuri na makazi ya taikuni mmoja wa kihindi aliyekuwa amemuoa mzungu .
Upande mwingine kulikuwa na nyumba nafikiri ilikuwa ya mkurugenzi au ofisa mkubwa sana wa Bugando hospital , upande wa chini yapo maghorofa mazuri na nyumba nzuri za makapteni na wahandisi wa Marine . Sisi tukiwa tunasoma ile nd'o ilikuwa njia yetu na tulikuwa tunacheza mpira kwenye kiwanja kidogo kilichokuwa kwenye maghorofa ya watu wa railway maarufu kwa jina la kisimenti .

Wale ambao hamjamuamini mleta mada naomba angalau mumuamini katika hili la bibi fisi .
Naam mhindi Raghu alimuowa mzungu mjane mke wa alie kuwa rafiki yake alipomuowa nae akapata ajali ya ndege akafariki baba alikuwa rafiki yake mkubwa ndo alomuuzia hilo eneo akachomwa moto hapa maeneo ya kwa bosco kama waenda station
 
Huyo bibi Fisi habari zake tulikuwaga tunazisikia hadi mjini daslamu miaka ya tisini hiyo. Walikuwaga wanasema ndio mkuu wa wachawi wote Tanzania nzima kuna mechi Yanga waliwahi kufungwa na Pamba ya Mwanza zikaja story kwamba Pamba mganga wao ni Bibi Fisi na kwamba ana ziwa moja wachezaji wakinywa maziwa yake hamuwafungi siku hiyo
Halafu Juma Njemba babu yangu Khatari 😁😁😁
 
LIKUD ujue ulisema utarudi na nondo za kutosha za mchawi Njemba...
Bibi Fisi alitisha sana ila mbona alikufa kwa kuuwawa?
Hakuweza kujitetea au matunguri yalikuwa yameishiwa nguvu?
hata uwe mchawi nguli ukipigwa ambush hutoboi😁
 
Watu wanasema ukanda huo kufuga fisi ni kawaida kwa wale manguli wa ndumba.

Wakati wa kampeni 2015 kulienea uvumi kuwa a learned brother from Havard alicheza na fisi laivu bila chenga.

Kama kuna atakaekuwa na picha yake ni vyema akatuwekea hapa!
A learned braza ntu ya dili za 10% nguli kabisa wa sheria 😂😂😂
 
N

Naam mhindi Raghu alimuowa mzungu mjane mke wa alie kuwa rafiki yake alipomuowa nae akapata ajali ya ndege akafariki baba alikuwa rafiki yake mkubwa ndo alomuuzia hilo eneo akachomwa moto hapa maeneo ya kwa bosco kama waenda station
Pale panaitwa tafico sio bosco...
 
Hadi leo ile sehemu ilipokuwa nyumba ya bibi huyo hakuna aloweza kuiendeleza na iko katikati ya jiji. Kwa wanaofahamu Agha Kan hospital ya jijini Kwanza, sehemu hiyo iko adjacent na hiyo hospital. Kwa sasa naona kuna wamachinga wanapanga bidhaa pembeni mwa hiyo sehemu.
Anayesema hayo mambo hayapo namshangaa sana tena sana.
Sio aghakan hosp...ile ni hindumandal hosp zamani ilikua mtaa wa balewa...ndio wamejenga hiyo hapo bugando
 
🤣🤣🤣 wewe ni wa kigoma? Basi utakuwa maji marefu wewe. Bibi Fisi alikuwa bestie wa baba ako na Juma Njemba babu yako
Mmanyema Mgoma na Mhombo 😁wewe umemsikia Juma Njemba kuna Mwamba Sheikh Mtumwa wa Sengerema Mwanza nae marehemu alikuwa Khatari Mwamba yule
 
Watoto wa Mwanza Igogo kuna group Facebook la wazawa wa Igogo mkajikumbushe story za bibi fisi.
 
Watoto wa Mwanza Igogo kuna group Facebook la wazawa wa Igogo mkajikumbushe story za bibi fisi.
Mi niliwahi kukaa Yale maghorofa ya mwanza south jirani na mchafu koge, huyo bibi fisi tulikuwa tunamsikia tu huko Bugando
 
N

Naam mhindi Raghu alimuowa mzungu mjane mke wa alie kuwa rafiki yake alipomuowa nae akapata ajali ya ndege akafariki baba alikuwa rafiki yake mkubwa ndo alomuuzia hilo eneo akachomwa moto hapa maeneo ya kwa bosco kama waenda station
Nani anaishi hapo kwa mhindi kwa sasa na Ile satellite bado ipo?
 
Sio aghakan hosp...ile ni hindumandal hosp zamani ilikua mtaa wa balewa...ndio wamejenga hiyo hapo bugando
Kwani hapo ndo Bibifisi alikuwa anaishi hapo kulikuwa na kichaka zamani baadae walikiwa wanacheza ball kwa Bibifisi ni upande WA pili kutoka nyumba ya kibopa WA tra karibu na get la marehemu Raghu
 
Hadi leo ile sehemu ilipokuwa nyumba ya bibi huyo hakuna aloweza kuiendeleza na iko katikati ya jiji. Kwa wanaofahamu Agha Kan hospital ya jijini Kwanza, sehemu hiyo iko adjacent na hiyo hospital. Kwa sasa naona kuna wamachinga wanapanga bidhaa pembeni mwa hiyo sehemu.
Anayesema hayo mambo hayapo namshangaa sana tena sana.
Acha uongo
 
Back
Top Bottom