Huyo Bibi ni kweli alikuwa na hayo maajabu yake, sitakaa nisahau tukio alilotufanyia, mimi na jamaa yangu enzi hizo tunasoma Lake Sec. tukapita eneo hilo, Bibi akatuomba kumsaidia kupasua kuni, alikuwa anapasua kuni nje ya kibanda chake, kwa kuwa tulishaambiwa mambo yake, tukasimama kweli tukamsikiliza, nikataka kwenda jamaa yangu akinishika mkono na kunivuta, tukaondoka, lakini cha ajabu tulishashtuka tumemaliza kupasua ule mti, tunamemkabidhi Bibi shoka na tunaondoka eneo la tukio !!! sasa hivi tumekwa watu wazima , kila tukikutana au kuongea kwa simu ni lazima tukymbushane tukio lile.