Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa

MKUU lKUD kiujumla me bibifisi namfaham kuna mambo umekengeuka kidogo mfano kisa cha matebgenezo ya hiyo balabala ya bugando miaka na namna alivyokufa bibi huyu
 
MKUU lKUD kiujumla me bibifisi namfaham kuna mambo umekengeuka kidogo mfano kisa cha matebgenezo ya hiyo balabala ya bugando miaka na namna alivyokufa bibi huyu
Ni miaka IPI? Alikufaje? Unamfahamu VP?
 
Bibi fisi ni true story na kwa mwanza alikuwa hana mpinzani kwa zama zile.

Nilishaingiaga kwenye kisanga na Bibi Fisi live.. Mbele ya nyumba yake kulikuwa na kauwanja kakulazimisha ka watoto watukutu wa Bugando kuchezeapo mpira wa miguu ule chandimu.. Sasa nakumbuka tulitoka shule tukaenda kuchezea pale na watoto wa Bugando. Bahati mbaya mpira ukapigwa ukaingia ndani ya kajumba ka Bibi fisi then dogo mmoja wa Bugando akaingiamo kufuata mpira, tulisubiri pale nje dogo atoke hadi saa moja jioni tukaamua twende kwao kuwataarifu wazazi wake.. Nao wakachanganyikiwa maana wanamjua yule bibi ni kigagula wa jiji zima na huwa hapendi watoto wachezee mpira mbele ya kale kajumba kake. Waliangahika usiku mzima... Kajumba mlango huko wazi hadi saa 12 za usiku lakini hakuna aliethubutu kuingia kipumbavu..Ukiangalia Giza na hakuna kelele yeyote ile ilhali na dogo yumo mule ndani. Hadi usiku wa manane walimfuata mzee mmoja nae alikuwa ana mambo ya kigagula ndo akaingia wakayajenga na Bibi then dogo akaachiwa kama usiku wa manane sisi watoto tushasepa makwetu then baada ya muda kupita tukaonana na dogo kwenye mpira tukamuuliza vipi uliona nini mule... Dogo anakwambia acha tu.. Ukiwa nje unaona ka nyumba kadogo ila ndani ni pakubwa sana na kuna watu wengi sana.

Bibi alikuwa na mengi sana Mimi ni miongoni mwa watu waliomfaidi sana Bibi.
Natamani uyo aliyefungiwa ndani naye aje aanzishe uzi wake hapa atiririke aliyokutana nayo humo ndani
 
Niliwahi kuweka Uzi hapa kuwa naenda kufanya utafiti kuhusu uchawi..huu ndio mrejesho sasa
Miaka ya 80 hivi niliwahi mshuhudia bibi huyo!! Nyumba yake ilikuwa mitaa ya jirani na maghorofa ya madaktari nadhani wa Bugando. Ukitokea Igogo kwenda Bugando barabara ya lami inachepuka kupisha nyumba ya bibi fisi. Habari za bibi fisi za kweli kabisa!!!
 
Umenikumbusha mbali

Nilikua nikipita ile njia aliyokua akiishi Bibi Fisi nikiwa naenda kwa shangazi yangu Igogo kutokea Mabatini

Nakumbuka upande wa pili wa barabara kulikua na kichuguu kikubwa.
Napakumbuka mahali hapo miaka ya 80s.. Nimemuona bibi fisi. Naukumbuka ile barabara ya lami, iliyochepuka kuipisha nyumba ya bibi fisi.... Tumepita mitaa hiyo sana tu tukitoka Igogo kwenda hospitali ya Bugando.... Nina hamu ya kupiga mitaa ile sijui ipoje baada ya kifo bi yule
 
Hadi leo ile sehemu ilipokuwa nyumba ya bibi huyo hakuna aloweza kuiendeleza na iko katikati ya jiji. Kwa wanaofahamu Agha Kan hospital ya jijini Kwanza, sehemu hiyo iko adjacent na hiyo hospital. Kwa sasa naona kuna wamachinga wanapanga bidhaa pembeni mwa hiyo sehemu.
Anayesema hayo mambo hayapo namshangaa sana tena sana.
 
Kaombe ramani ya mipango miji utapata majibu
Hadi leo ile sehemu ilipokuwa nyumba ya bibi huyo hakuna aloweza kuiendeleza na iko katikati ya jiji. Kwa wanaofahamu Agha Kan hospital ya jijini Kwanza, sehemu hiyo iko adjacent na hiyo hospital. Kwa sasa naona kuna wamachinga wanapanga bidhaa pembeni mwa hiyo sehemu.
Anayesema hayo mambo hayapo namshangaa sana tena sana.
 
ila naomba isiwe ndo chachu ya kuwatenga wazee kwenye jamii zetu kwa kuzania ni wachawi kuweni makini sana!
 
Back
Top Bottom