Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,440
- 38,437
Ktk harakati za kimaisha huwa inatokea mtu akaamua kufake Kitu flani mf mavazi, sauti ama maandiahi ili tu atimize haja zake flani flani, wapo wanaofake identity, wapo wanaofake Elimu, wengine wanafake Mapenzi ama tabia! Sikia hii!
Pale Ubungo Maji, huwa jioni wanajaa abiria wanaoelekea Njia ya Mbezi lkn hawataki kupanda MWENDOKASI.
Kwa kawaida pale, Gari ikija mf IT ama daladala inagombaniwa coz pale hamna kituo na muda wwt bao, so makonda huwa wanahamasisha abiria kupanda juu kwa juu!
Siku hiyo nimevaa Kaunda (huwa navaa Kaunda km Kinga na hasa nikiwa naenda baadhi ya Ofisi za umma kuhitaji huduma) nlikuwa nimesimama pembeni ya abiria wengi, nasubiria usafiri, mi huwa sigombanii daladala kuhofia kupigwa CMU ama wallet!
Basi ikaja daladala, abiria wakagombania pale mlangoni km kawaida yao! Abiria fake nikamuona anamchomolea brazamen CMU yake, kisha akafanya km kaghairi safari, akashuka!
Ile anageuka tu, uso kwa uso na Mimi! Nikamkazia macho. Nikamsoma usoni, nikagundua km kashapoteza self confidence hivi kwa uovu alioutenda ndani ya sekunde chache. Kule nyuma jamaa aliechomolewa CMU kashuka, anakuja wangu wangu!
Fasta nikafanya kama namsalimia yule Kibaka, afu kwa sauti ya kiaskari nikamuamuru SIMAMA PEMBENI! Muda huo tayari Brazamen alieibiwa kashafika, macho yamemtoka anaangalia angalia wale masela kama atambaini mwizi wake! Watu hawajui kinachoendelea, ni 3 Men show!
Akapata akili ya kutulia na kufuatilia kile kinachotokea kati yangu na yule msela! Nikatoa amri ya pili kwa sauti: HAYA MPE SIMU YAKE! Jamaa huku ana wasiwasi, akatoa CMU kiunyonge na kumpa brazamen!
Brazamen akaanza kumchana yule Kibaka, Kibaka akabaki anaomba msamaha tu!
Mwishowe Brazamen akatoa mwekundu Mmoja kunipa, nikamuambia hapana, fanya mpango wa kuita tax, tumpeleke huyu Hapo URAFIKI (Police) Daah Kibaka kuskia vile ndio akazidi kuchanganyikiwa! Macho yamemtoka, akilini anajua mi Mzee wa kazi!
Brazamen akakataa, akasema ameshapata CMU yake so hana haja ya police! Kiukweli nilikuwa naenjoy Sana yale maigizo yangu pale! Basi nikaishia kumuambia Kibaka "acha MCHEZO wako!" Akaniahidi harudii tena!
Ndani ya dk 5, mateja wote wa pale nikaona wameyeyuka! Hata sikuwaona wakati wanaondoka, Sijui waliondokaje pale! Kiukweli mpk sasa huwa siamini amini namna gani niliweza kuigiza vile!
Wapi uliwahi kukwama, ukafake ili kufanikisha mishe yako?