Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

= Asante Mungu
🙏🏿🙏🏿🙏🏿

20230723_160521.jpg
 
PICHA: Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mama Chuda akiwa ameshika jiwe kubwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Mount Meru Jijini Arusha ili kujihami iwapo Kijana aitwae Ally Dangote ataamka kutoka ndani ya chumba hicho.

“Sijaamini kama amekufa ndio maana nimeshikilia jiwe tunaweza kufanya mzaha ukakuta tu kazimia, nimejihadhari na jiwe” ———amenukuliwa akiongea Mama Chuda.

Marehemu Ally Dangote alikua akituhumiwa kwa wizi, ubakaji na mauaji huku akidiwa kufanya hayo yote akiwa anajiziba sura kwa kutumia vazi la hijabu ambapo hadi anafariki inadaiwa alikua amechoma visu Watu 15 na kuua Watu watatu Jijini Arusha.

Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha Salvas Makweli ameithibitishia AyoTV leo na kusema kuwa kifo cha Ally kilitokana na kujirusha kwenye gari la Polisi kwenye safari ya kwenda kuwaonesha Polisi makazi ya Wahalifu wenzake. #MillardAyoUPDATES

View attachment 2820363

Sent using Jamii Forums mobile app
watu wa arusha bhana,nilijuaga huyo ally
ni kipande cha mtu hadi anawalaza wababa saa 12 jioni
 
Back
Top Bottom