TUKIO LA KUSIKITISHA SANA : KATA YA IGALULA, WILAYA YA UVINZA : JUMAMOSI 11-11-2023.
Kwanza tuanze kwa kupongeza jitiada za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusikiliza kilio Cha muda mrefu Cha wananchi wa Mkoa wa kigoma kuhusu vitambulisho vya taifa ( NIDA), na kuja na majawabu stahiki.
Serikali imeleta vutambulisho vya taifa ( NIDA), vingi tu Mkoani kigoma na kila Wilaya, Halmashauri, kata ilikabidhiwa ili kuvifikisha moja kwa moja kwa walengwa ( wananchi). Zoezi kimefanya na linaendelea kufanyika Karibia kwenye kata zote za Mkoa wa kigoma na kata ya IGALULA ikiwemo. Unakuta majina na number za vutambulisho vya taifa vimebandikwa kwenye ofisi za watendaji wa kata, Mwananchi akiliona jina lake, Basi anaingia ofisini kuchukua kitambulisho chake.
• JUMAMOSI 11-11-2023 : Zoezi liliendelea vizuri tu ofisi za Mtendaji wa kata ya IGALULA. Wananchi wanachukua vutambulisho vyao vya taifa ( NIDA) Kama kawaida.
Kama wasimamizi, walikuoepo : Mtendaji wa kata ya IGALULA, Watendaji wa vijiji vya Ndele, Rukoma na Lubarisi.
Ngazi ya wilaya ( Wilaya ya Uvinza), alikuwa Afisa wa NIDA wa wilaya, na kijana mmoja aliyekuwa akijitambulisha kuwa ni Afisa usalama wa taifa toka ofisi ya DSO Uvinza.
Akaja kijana mmoja kwa jina SEIF HARUNA MTULA, Mkazi wa kijiji Cha Rukoma, mwenye number ya sim : 0787085787 kuchukua kitambulisho chake Cha taifa ( NIDA).
Alipoingia ofisini kwa Mtendaji wa kata, walifanya mahojiano, akaambiwa kitambulisho chake Cha taifa kipo lakini hatopewa. Wakaanza kuvutana, na baadae akatolewa nje ya ofisi. Kijana huyu SEIF HARUNA MTULA akaamua kurudi Nyumbani.
Baada ya muda mfupi, akaitwa Tena ofisini kwa Mtendaji wa kata ya Igalula kuchukua kitambulisho chake Cha taifa ( NIDA).
Alipokuja, akawekwa Katikati ya watendaji hao : wa kata na vijiji, na kuanza kumkaripia vikali kwa kudai kwamba alipiga sim ofisi za NIDA taifa na kuwashitaki kwamba walimnyima kitambulisho chake.
Sauti zikazidi kupanda kwa hasira toka kwa Mtendaji wa kata na Afisa NIDA wa Wilaya, na ndipo akaitwa Askarijeshi wa JWTZ, mwenye number ya sim : 0627674113 toka Kituo Cha doria kijiji Cha RUKOMA na kumwambia amshughulikie kijana huyu SEIF HARUNA MTULA.
Kijana aligaragazwa kwenye tope, kamwagiwa maji, kapigwa kuanzia mida ya saa Tisa mchana ( 3:00' PM) Hadi saa Kumi na Mbili Jioni ( 6:00' PM)...kisa tu kufwatia kitambulisho chake Cha taifa ( NIDA), ambacho Ni haki yake ya msingi.
Wananchi wengine walitamaki, walishangaa, na wengine kuanza kukimbia. Wapo wananchi waliodai kuombwa pesa ( 2,000 Tshs Hadi 5,000 Tshs) za usunbufu wa kupekua na kuwatafitia vutambulisho vyao.
Kijana huyu Mhanga SEIF HARUNA MTULA Hadi muda huu wa leo Jumatatu, Hali yake sio nzuri, maumivu, homa Kali, anashinda ndani akilia kwa maumivu makili upande wa mbavu za kushoto.
Tukio hili la ukiukwaji wa haki za Binadamu, na ukatili wa kijinsia ( kimwili), aukubaliki kabisa na uliwafanya wananchi wengi katani hapo kuogopa hata kuja ofisini kwa Mtendaji wa kata kufwatia vitambulisho vyoa vya taifa ( NIDA) Hadi sasa. Tuna wasiwasi vutambulisho vingi vitarudishwa Wilayani kukosa wachukuaji, na wakati wachukuaji wapo lakini wakiogopa kufika ofisi za Mtendaji wa kata.
Ndugu zanguni watanzania wapendwa, hivi hivi ni vitendo vya kibinadamu kweli?
Askari wa JWTZ anakijaje na kumpa kipigo raia mwema huyu, kwa amri ya Nani, vipi hii ndio kazi yake?
Mhe. Diwani wa kata ya Igalula, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Mhe. Mbunge wa Jimbo la kigoma kusini, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, viongozi wa chama Cha Mapinduzi kata ya Igalula na viongozi wa chama chetu Cha Mapinduzi Wilaya ya Uvinza, ebu liangalieni hili kwa jicho pevu sana maana Wilaya ya Uvinza imekua Ni kichaka Cha manyanyaso kwa wapiga kura wetu na hasa kata hii ya Igalula.
Taasisi za kutetea haki za Binadamu, taasisi za kupambana na ukatili wa kila aina, TAKUKURU, tusaidieni pia kwenye hili maana sio Jambo jema kwenye jamii ya watu waliostarabika.
TUNAOMBA MAJAWABU STAHIKI TOKA SERIKALINI.
Ndimi RAIA MWEMA..
Sent using
Jamii Forums mobile app