Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva Profesa Jay amefanya mahojiano na Clouds FM na amefunguka haya
"Kuna sindano nilikuwa nachona kwa siku Mil. Tano asubuhi na Jioni. Ile sindano ndio iliyoniamsha. Nilikuwa nachoma mara Tano kwa wiki. Kwa wiki Mil. 25. Nilichoma kwa wiki moja kila siku mara Mbili. Nilichoma sindano 10 ni mil 50. Hiyo ni sindano tu, bado kusafisha figo, (dialysis) ukianzia pale Muhimbili ni Laki na Themanini kwa mgonjwa anayetoka nje ni Laki Tatu na Nusu. Hiyo ni mara moja na unatakiwa ufanyiwe hadi mara Nne kwa wiki kutokana na tatizo lako"
"Kwa kuanzia nimeanza na @professorjayfoundation kwa sababu nimeona watu wanapata tabu sana na hizi hela ni nyingi sana. Na wote hawawezi kufikiwa na Rais na watu wanataabika sana. Kwangu ilikuwa kawaida lakini kuna watu figo zilikuwa zimefeli. Nilikuwa nachomwa hivyo sindano lakini figo zangu zilikuwa hazijafeli na ni kwamba figo moja likuwa na na mchanga na moja ilikuwa inasuasua ilikuwa na sumu nyingi" professor jaytz,
"Ingawa magonjwa ni mawaidha watu wanasema, lakini watu wanakufa sana, kwa mimi niliyekaa ICU siku 127, unajua kule ICU watu hali zao mbaya sana, kujikuta ICU na una- survive siku 127 sio mchezo" professor jaytz
"Watu wanaumwa sana, na wanakufa mno, ndio maana nikasema foundation yangu nianze na suala la figo" professor jaytz
"Kutokana na nilipopitia kwa sasa nipo vizuri kila siku naimarika namshukuru sana Mhe Rais samia_suluhu_hassan yeye amenipigania kwenda India nilitamanii kukutana naye, kitendo alichokifanya alikifanya kama Mama. Kwahiyo nina sababu ya kushukuru na kumpa maua yake" professor jaytz
#Monmedia
Sent using
Jamii Forums mobile app