Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

IMG_1696760691756.jpg
 
AMTELEKEZA MPENZIWE SIKU YA KUFUNGA NDOA BAADA YA KUGUNDUA SIYO BIQRA KAMA ALIVYOMWAMBIA.

MBAGALA️Pichani ni screenshot picha kutoka kwenye video ya mwanadada ambaye ameachwa siku ya ndoa yake ambayo ilitakiwa ifanyike Octoba 7, 2023 huku sababu ya mwanaume kuikwepa ndoa hiyo ikiwa ni kuchukizwa na uongo wa bidada huyo ambaye awali kabla hawajakutana kimwili alimwambia yeye ni biqra hajawahi kufanya mapenzi, lakini baada ya mwanaume kutaka kujua kama yaliyomo yamo ndipo akagundua yaliyodhaniwa kuwemo hayakuwemo.

Kwa mujibu wa video hiyo inaelezwa siku ya tukio bibi harusi na ndugu zake walijiandaa wakajipamba kwa mapambo ya pwani, unguja na pemba wakajitia nakshi za kitanga wakimsubiri mwanaume afike amchukue binti yao. Waliendelea kusubiri bila mafanikio wakaanza kupata hofu, ndipo mwanaume akamtumia meseji bidada huyo akamwambia mimi siji na nimeghaili kukuoa kwa sababu ulinidanganya kwamba una biqra kumbe hauna, mimi nataka mwanamke biqra kwahiyo ng'oa mapambo yako uendelee na shughuli zako.

Baada ya kuisoma meseji hiyo bibi harusi huyo alimuonyesha mama yake na mishangazi zake, ndipo walipoangua kilio. Na haya ni maneno ya mmoja wa mashangazi wa binti huyo.

"Huyu mwanaume vipiii!! Unampata wapi mtoto wa kike sasa hivi umuoe umkute ana biqra, biqra zenyewe zimekuwa kama maji ya kunywa ukiibandua dakika mbili tu imetoka, wanaume wa siku hizi ni wachezeaji sana"View attachment 2776773

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida siyo kupata biqra, tatizo hapo udanganyifu.
'Nina biqra' kumbe huna lolote
 
Back
Top Bottom