Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Wenzetu wanahangaika. Wanataka kujua chemical composition ya huu mwamba maana utakuja kugongana na dunia siku zijazo. Zipo nadharia nyingi za jinsi ya kuepukana na janga kama hili maana kama mgongano huo utatokea basi itakuwa karibia sawa na ule uliowaondoa wababe wa dunia akina dinosaurs na kuua zaidi ya asilimia 90 ya viumbe wote duniani.

Njia mojawapo ni kumfuata Bennu huko huko aliko na mabomu ya nyuklia kwenda kumsambaratisha. Njia nyingine pia ni kumfuata huko huko na mashine kali za laser na kuanza kumvuta pole pole ili hatimaye kumwondoa kwenye orbit aliyomo - orbit ambayo hatimaye itamfanya agongane na dunia. Nyingine ni kwenda kumpasha moto ili kuyeyusha barafu yake na hivyo kumfanya awe mwepesi na kumfanya ajiondoe mwenyewe kwenye orbit yake ya sasa...

Jamaa angalau wanajaribu tuwape tu maua yao!

View attachment 2763215
Jamaa wako poa sana.
Nilivutiwa na habari kwamba zile sampo zitahifadhiwa ili kuwaonyesha wanasayansi ambao bado hawajazaliwa, waje wafanye utafiti kwenye mashine nyingine kabisa watakazozitumia. Angalau na wao waje na majibu yao.
 
Screenshot_20230926-230353.jpg
 
Back
Top Bottom