Unajua mume/mke/mpenzi wako anafanya kazi flani, unajua kabisa kuwa kazi yake inamfanya kuwa bize. Hana muda wa kuongea na simu wala kujibu meseji akiwa kazini. Lakini wewe bado unapiga, wewe bado unatuma meseji, akichelewa kujibu meseji au akisahau, akikuambia nitakutafuta baadaye akasahau basi unalalamika, unanuna, unavimba na kukakamaa kama chapatti za kichaga!
Ndugu yangu kama huelewi na hilo kuwa anatafuta pesa basi hembu nenda katafute mtu ambaye hana kazi ili muwe mnachat naye! Siwezi kudili na kelele za bosi wangu na nirudi nyumbani kujibu kelele eti kisa sijajibu meseji? Meseji yenyewe iliuliza “UMEKULA!” Kama unataka ni jibu meseji ya namna hiyo basi tuma kwanza pesa ya chakula ili baadaye ndiyo uniulizie kama nimeitumia vizuri hiyo pesa kwa kula au nimenunulia vocha!
Zaidi ya hapo Tusichoshane! Wala hata sijaulizwa na mtu ila nimeamua tu kuandika kwani huyo mpenzi wako ameshachoka na hayo maswaliswali yako ila tu hapendi kukuambia kwaku anajua kisirani chako si cha nchi hii! Ni sawa na wale ambao anakutumia meseji hujajibu, anakupigia badala akuambie shida zake anaanza kukuambia kwanini hujajibu meseji zake!
NIMEMALIZA!
Copy &Paste