Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Screenshot_20230115-101235.jpg
 
Hicho ndicho kitakachokupata, kwa mfano, ukija kwangu Misungwi. Utachinjiwa beberu la mbuzi na matokeo yake ndo hayo. Nyama za kila aina. Na ni lazima ule kweli kweli maana usipokula ni dalili ya dharau na kutukosea heshima wenyeji wako. Na nyama zingine zinakaushwa (mitanda) ukiondoka tunakubebesha. Ikibidi na ngozi ya beberu lako pia unafungiwa vizuri.

Utayaweza haya? 😁😁😁
😂😂 mbona sasa sheeeeda?

Kwanza kabisa mimi kula sana uwa siwezi, sasa ukiniwekea msosi mwingi afu nisile sana ndio uone nina madharau si vibaya hivyo? Mnakuwa mnamkomesha mgeni.
 
mbona sasa sheeeeda?

Kwanza kabisa mimi kula sana uwa siwezi, sasa ukiniwekea msosi mwingi afu nisile sana ndio uone nina madharau si vibaya hivyo? Mnakuwa mnamkomesha mgeni.
Siyo kumkomoa mgeni. Tunajulikana kwa ukarimu wetu hasa kwenye ishu za misosi.

Na usipokula basi maana yake safari nyingine afadhali usije maana hatutakuwa na msaada wo wote kwako!

Muulize shoga yako atakuelezea sema naye mtoto wa kishua sina uhakika hata kama anajua cho chote kuhusu hizi protokali za kimila
 
Back
Top Bottom