STAR TV NA REDIO FREE KUFUNGWA.
Steve Diallo, mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Star TV, Radio Free Africa na Kiss FM amesema “Wanadai malipo ya mishahara ya miezi tofauti, wapo wa miezi mitatu na wengine zaidi, tumetoa taarifa TCRA na kwenye Ofisi ya Kamishna wa Kazi, hata Waziri Nape (Nnauye) alipiga simu kuulizia kinachoendelea.”
Ameongeza “Tunafanya vikao na wafanyakazi ili kutatua changamoto. Pesa hatuna, hatuzalishi ya kutosha ukilinganisha na mahitaji yaliyopo ya Satellite na kukatika kwa umeme. Kukatika-katika kwa umeme kumesababisha matumizi makubwa ya jenereta.”.