Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Tangazo tangazo
FB_IMG_15757527994760531.jpeg
 
Kipindi hicho jamaa alikua watano kidunia kwa utajiri, aliweza kujenga nyumba nzuri hakuna mfano mpaka iliiwa pepo ya duniani.

Juu mlangoni mwa hiyo pepo aliweka ndege kubwa nzuri zenye kupendeza kama mapambo

Huyo binti yake alishawahi kupewa fursa ya kuchagua chochote anachokitaka, dogo akachagua farasi ambaye anamabawa.

Jiulize farasi mwenye mbawa utampata wapi?

Jamaa alichukua farasi akaleta jopo la wanasayansi wafanye upandikizi wa mbawa kwa yule farasi ilimradi tu kutimiza ahadi kwa bintiye

Aliweza kufanikisha zoezi hilo lakini hakuchukua muda mrefu, yule farasi akafa

Pablo escobar ndo mfungwa pekee ambaye alijijengea gereza kwa pesa yake, na ramani ali design yeye.

Gereza lilikua zuri lililofungwa mitambo ya kisasa, waterfall na system za mawasiliano ya kisasa iliyoweza kumfanya awasiliane na familia yake vizuri kwa njia ya kuonana, huku akiendelea kufanya biashara ya madawa akiwa humo humo gerezani

Na waluothibutu kumdhurumu mali zake kwa kujua kua yuko jela hawezi kufanya lolote, watu hao waliuwawa kwa mkono wake akiwa humo humo gerezani

Baada ya serikali ya nchi hiyo kusanukia huo mchezo wakaweka mpango wa kumuua, wakati wako nje hawajalifikia gereza escobar aliwateka wale askari waliokua wanamlinda mle kwa kutumia jeshi lake lililokua miongonj mwa hao askari

Akawaamuru majeshi yaliyokua nje yasithubutu kusogea kwani watasababisha askari wao wauawe, jeshi likatii amri yake

Baada ya kimya cha muda mrefu kutoka ndani ya gereza, wanajeshi wa serikali walijaribu kuingia ndani ya gereza na kukuta walinzi waserikali wameuawa na kilichowashangaza zaidi kutomuona escobar

Kwasababu wao ndio walikua mlangoni kwaiyo kama angetoka lazima angekutana nao pale nje, na mfumo wa hilo gereza lilikua na umbo kama duara kwamba mlango ulionekana ni mmoja tu sasa yeye katokea wapi??

Hilo ni swali ambalo mpaka leo halijatafutiwa ufumbuzi
Alikufa lini na nini kilimuua?
 
Back
Top Bottom