Msichana wa kazi:
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshahara..... Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu
tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kashtuka kwa mshangao, hasira na ghadhabu huku akijiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: ssshhhh... mwanangu, tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Chonde chonde, mwenzio nipo chini ya miguu yako. Ntakuwa mgeni wa nani mie.. Nakupandishia mshahara wako mara tatu kuanzia leo....