Vituko mitandaoni. Tupia chako

Dah!

Kuna siku home kulikuwa na ujenzi basi mi nikatoroka siku nzima niko mtoni na masela. Nilikuwa najua jioni home kutakuwa na kibano hatari na nilikuwa nimeshajiandaa kisaikolojia. Bahati nzuri jioni jioni hivi wakaja jamaa wawili hivi wana majani ya miti yamepondwa pondwa wakaweka kwenye maji. Mara samaki wakaanza kutapatapa na kuruka. Basi tukaanza kuwakamata kila mtu kwa juhudi zake.

Nilikamata samaki wakubwa kibao mpaka wakawa wananielemea. Nilipofika home aisee nilipokelewa kishujaa sana hakuna kibano wala nini samaki wakakaushwa na tuliwala karibu wiki nzima.

Gate pass muhimu sana


Good ole days


#BeautifulChildhood
 
ukajipatia gate pass kiulainii. Kama muujiza yani ukapona kipondo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…