Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

FB_IMG_16343349116060584.jpg
 
Aliyevamia nyumbani kwa diwani wa Narumu, Nicodemus Mbowe, akampiga na kumvunja mguu, akamkata mwanae sikio, akavunjavunja TV na samani nyingine za ndani leo anasomewa hukumu.

Aliyewapiga mawakala wa Chadema kwenye kituo cha kura Mungushi, akawafunga mikono na miguu, akawajaza matambara mdomoni na kuwatupa Sanya station anasomewa hukumu leo.

Aliyevamia hotel ya kitalii ya Weruweru akiwa na silaha na kulazimisha aoneshwe chumba alicholala msanii Nandy anasomewa hukumu leo.

Aliyemvamia mzee Eliot Lyimo na kumlazimisha ampe 25M au ampakazie kesi ya uhujumu uchumi anasomewa hukumu leo.

Aliyempiga diwani wa Sombetini, Bakari Msangi hadi kupoteza fahamu anasomewa hukumu leo.

Aliyevamia duka la Mohamed Saad na kutembeza kipigo kikali akitaka apewe 100M bila kujali anarekodiwa na CCTV camera anasomewa hukumu leo.

Aliyevamia hotel ya Freeman Mbowe usiku wa manane na kukamata viongozi wa Chadema waliokuwepo anasomewa hukumu leo.

Aliyeingiza taifa ktk mgogoro wa kidiplomasia kwa kughushi namba za UN na kupachika kwenye magari binafsi anasomewa hukumu leo.

Aliyeghushi kitambulisho cha TISS na kujifanya afisa usalama wa taifa anasomewa hukumu leo.

Aliyetumia madaraka yake kutesa watu, kuumiza, kulala bure kwenye mahoteli mbalimbali, na kulazimisha mapenzi na wanawake aliowataka anasomewa hukumu leo.

Aliyekamatwa kwenye appartment Mikocheni akishiriki ngono za makundi (group sex) wanaume 8 na wanawake 6 anasomewa hukumu leo.

Aliyekua akiongea na mwendazake anamrekodi na kwenda kuwasikilizisha wafanyabiashara, kisha anawadai pesa anasomewa hukumu leo.

Aliyezorotesha biashara mikoa ya kaskazini na kuua makampuni mengi ya utalii ikiwemo kampuni kubwa ya Asante Tours anasomewa hukumu leo.

Aliyedanganya kuwa wamiliki wa mabasi wameng'oa miondombinu ya reli anasomewa hukumu leo.

Ni hukumu ya kihistoria. Ni hukumu itakayoonesha picha halisi kuwa serikali yetu iko wapi kati ya HAKI vs UONEVU.

Wachache wanamuombea aachiwe huru wakidai halikua kosa lake bali alitekeleza maagizo kutoka juu. Wengi wanamuombea afungwe ili iwe fundisho kwa wanaotumia madaraka vibaya. Mimi naomba HAKI ITENDEKE. Na sio tu itendeke bali IONEKANE KWELI KUTENDEKA.!
Nimeukumbuka ule msemo wa kutomtukana mamba kabla ya kuvuka mto
 
Back
Top Bottom