Vituko mitandaoni. Tupia chako

Hongera kwa pumziko jema kamanda.
Uraibu wa hapa nao ni mgumu aisee, kuna wakati unaona heri upumzishwe kidogo,
Ingawa ukiwa mapumzikoni unajikuta kuwamiss vijukuu vyako
Aisee ni kweli. Ni sawa sawa na mtu wa kokeini. Akitiwa lupango kidogo anapata ahueni na kama ana washauri wazuri wa saikolojia anaweza kuachana na uraibu huo kabisa.

Ban mimi nazipenda kwa sababu kusema kweli unapumzika na uraibu wa JF. Wiki moja ya kutoingia hapa kidogo nimeweza kutafakari mambo kadha wa kadha na kupumzika. Hizi memes nazo ni uraibu kwa kweli kwa sababu ukiiona nzuri mahali ni lazima uje kuiweka. Tunapoteza muda sana hapa kwenye JF yao japo pia ni kijiwe muhimu sana pia...

Nikichoka tena najua jinsi ya kujipatisha ban nitamkorofisha tu mods nitandikwe nyingine hata ya mwezi mzima. Wajukuu zangu wanajua mahali pa kunipata
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…