Hadithi za Allan Qurtamain...kazi muhimu katika mlolongo mrefu wa fasihi ya kikoloni iliyolengwa katika kumwonyesha mtu mweusi kama chombo tu cha kumtumikia mzungu. Umslopagasi - mzee shujaa wa Kizulu mwenye uwezo wa ajabu kimapambano; na shoka lake lisilo na huruma (Inkoskazi) hana faida nyingine yo yote mbali na kupigania himaya ya kizungu mpaka kupoteza uhai wake. Ndiyo maana kitabu hiki kilipigwa marufuku sehemu mbalimbali duniani ambako kulikuwa na msisimko wa watu weusi (na wengineo) kujikomboa kifikra.
Si hivyo tu.
Mtu mweusi kwenye kitabu hiki alionekana ni kiumbe kinachopenda kumwaga damu ovyo.
Alionekana aliye tayari kuhatarisha maisha yake binafsi na jamii nzima kwa sababu ya mtu mweupe.
Kitabu hiki na kingine cha "Mashimo ya mfalme Suleimani" kimemuweka mwafrika kwenye daraja la chini.
Hata hivyo pamoja na madhaifu hayo, ndani ya vitabu hivi viwili kuna mafunzo ambayo yangali yana maana kubwa kwa mwafrika mpaka hivi leo.
Kwamba binadamu ni lazima upambanie maendeleo yako kwa machozi jasho na damu bila kuogopa kifo.
Safari iliyojaa vitisho ili kuifikia nchi ya Zuvendi inafundisha ujasiri uliotukuka.
Safafari nyingine ya kwenda kutafuta Almas kwenye nchi ya Ukukuana ni ujasiri mwingine unaoweza kumfaa mwafrika.
Wafrika leo ni magoigoi kwenye kusaka ustawi .
Tusome vitabu hivi kujifunza namna ya kuzikabili shida kwenye njia ya kusaka mali.
Wenzetu walitoka kwenye mabara yao kutafuta ustawi barani Afrika nasi tupambane bila kuchoka kufikia malengo yetu.