Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

IMG-20210909-WA0095.jpg
 
Huna hili waka lile upo home unarilaksi mara anatokea binti mrefu mrembo amefungasha hatari akiwa na Biblia yake mkononi. Anafika hapo kwako na kuuliza "eti Moud ndiyo yupi hapa?". Nawe bila kusita unajitutumua ni mimi hapa na bila kusema neno anakusogelea na kuanza kukupa vitasa vya uhakika tu halafu kama alivyokuja huyooo anakwenda zake. Familia yote inaachwa imepigwa na bumbuwazi

Mtumishi hebu fanya kweli mtu ale vitasa vya kueleweka leo hii hii au kesho!
Hahahaha
We jamaa kumbe haujuagi vipigo vya hawa watu
 
Juzi nilikosea nikatuma Tsh.250,000 kwa Wrong number, baada ya kuona hilo, niliamua kujaribu kutuma sms ya kutisha alieipokea hela hiyo...

Text hiyo niliiandika hivi,
Habari yako rafiki, naitwa Mazon, ni balozi wa kanisa jipya la Shetani hapa Tanzania. Ni tumaini langu umeiona posho yetu ya uanachama ya Tsh.250,000 tumekutumia TIGOPESA ili kujiunga na kanisa letu la Shetani.

Huo ni mwanzo tu wa mambo mazuri yanakuja. Usiku wa leo tuna mkutano ambapo tutachinja watu watatu kwa ajili ya kafara. Tumekubaliana kufanya kafara hii katika viwanja vya nyumbani kwako mida ya saa nane za usiku na unatakiwa uchague mmoja wa watu unaowapenda ili tunywe damu yake pia.

Lakini kama hungependa kujiunga katika kanisa letu hili la Shetani, rudisha hiyo pesa kwa namba yangu hii hii"

Baada kama ya dk 10, nikapokea sms inasema, "Oyoo bro, kama vp tuma Tsh.250,000 nyingine kuna mshikaji wangu nae kavutiwa na kanisa lenu"

Kidogo nizimie

Yaani watu vyuma vimekaza kiasi kwamba wako tayari kwa lolote
 
Hii nchi yaani dah!
Hata mkulima masikini naye akienda kuuza vimazao vyake ni lazima akamuliwe. Halafu ripoti ya CAG ikitoka watu wameiba mpaka kufuru. Halafu ndio hawa hawa wanajiona wajanja wanajenga majumba ya kushangaza na kusukuma ma Range Rovers. Ukisema utaambiwa unaona wivu...

Kama kweli tungekuwa na dhamira ya kuendelea kwa kodi zote hizi na tozo pamoja na mabilioni ya misaada na mikopo tunayopewa, tungeweza kabisa aisee. Lakini leo hii unakwenda vijijini huko unakuta watu wetu bado masikini wa kutupwa; wakati pesa zinachezewa tu...
IMG-20210909-WA0066.jpg
 
HAPA BUSARA INAHITAJIKA

Mwanamke kaazima ndoo ya mpangaji mwenzake chumba cha pili ambae ni kijana hajaoa.Alipomaliza kuoga akajifunga khanga yake moja akatoka bafuni akairudisha ndoo, alipofika ndani kwake akakumbuka amesahau chupi yake kwenye ile ndoo, akatoka harakaharaka vilevile na khanga moja na kugonga mlango.

Jamaa akamwambia aingie ndani aichukue, Anatoka tu mlangoni anakutana na mumewe anatoka kazini kamuona mkewe kavaa khanga moja na mkononi kashika chupi.

Je wewe ungekuwa ni mume au mchumba wake ungefanya maamuzi gani?
 
Back
Top Bottom