Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

2.5503677710188324E18.jpg
 
Hana majaribu yo yote huyu. Nyie endeleeni kufurahia kwa sababu ni haki yenu. Ndivyo dunia ilivyo. Hata uwe mwema namna gani siku ukitetereka jua utachekwa tu. Alichekwa Bwana Yesu sembuse mimi na weye Ostaadh? Funzo hapa kwangu na wewe ni kwamba tuishi kwa wema na haki lakini pia tutambue kuwa siku tukianguka watu wengi tu watafurahi; na watacheka. Na kama tuliishi maisha mema na yenye kuliwaza roho zetu na za wengine hilo halipaswi kutuumiza
Ni kweli kamanda, mwanadamu ni kiumbe aliyejaa hila, choyo, wivu, husda, tamaa nk.
Kuna watu wengi wasiopenda kuona kuinuka kwa wengine.
Wengi tunapenda kuona kuanguka kwao, ilikuwa hivyo pia hata kwa mzee Ali Hassan Mwinyi wakati analazimishwa kujiuzulu uwaziri kwa kashfa zilizofanywa na wengine.
Lakini baadaye akainuka mpaka juu kabisa.
Yaweza kuwa hivyo pia kwa mwingine, lakini ni vema kuyaishi maisha ya siasa kwa adabu. maana hatujui kesho yetu itakuwaje
 
Mwenyewe amewahi kulisema hili? Kuwa anaumia sana kupoteza hizo nafasi? Ataumia tu kama hajitambui. Wangapi tumewaona wakipoteza hizo nafasi wakakaa kimya halafu wakarudi, tena kwa nafasi za juu zaidi? Tena huyu balozi na mbunge?

Simtetei na wala simjui lakini Wabongo tuna tabia mbaya ya kufurahi na kushangilia "wenzetu" wanapoanguka hata kama kuanguka kwao hakutusaidii kwa namna yo yote ile. Tabia hii ipo kuanzia kwenye familia na kwingineko. Ni tabia ya hovyo!
Ukiona mamia ama maelfu wanashangilia anguko lako, jitafakari.
 
Back
Top Bottom