Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

IMG_20210411_143317.jpg
IMG_20210328_125539.jpg
 
Hizo ni hesabu rahisi tu haihitaji kuombana misamaha zito nae anashindwa nini kuelewa
Tangu jamaa ale uteuzi sidhani kama alishawahi kuwasilisha report
Mzee mwenyewe mwamba angekuwepo kungekuwa na report yake tofauti na hii
Lakini upepo umebadilika na jamaa kajiongeza tu juu kwa juu
Zitto anatafuta kiki au anakoleza moto tu. Tatizo ni kwamba mifumo hii ya ulaji imejichimbia sana katika taasisi zetu; na upigaji huu utaendelea tu miaka nenda miaka rudi hata aje nani. Wapigaji akina Kigwangalla hawatafanywa cho chote; na wataendelea tu kuturingishia mitandaoni humu na "Think out of the box" na "vijana mnakwama wapi kujiajiri?". Wakati huo huo mtu anayeiba kuku tukimkamata tunampiga mawe na kumchoma moto. Jamii ya ajabu sana !!!

Kinachonitia huzuni miye ni ukweli kuwa katika sekeseke lote hili sijasikia popote mjadala wa maana kuhusu jinsi ya kuondokana na upigaji huu au japo tu kuupunguza. Badala yake umegeuka na kuwa mnyukano na ushabiki uliopitiliza kimo kati ya MATAGA na MATHA. Hopeless !!!
 
Mbona kama wanalia hahahaaa
Wanaamini kuwa Supreme leader wao ni mungu kwa hiyo kupata bahati ya kupiga naye picha hivyo ni tukio la kipekee na lenye kusisimua sana maishani!

Na inasemekana wasiolia wanaweza kutiwa ndani na hata kuuwawa (kulingana na propaganda za vyombo vya habari vya Kimagharibi)
 
Back
Top Bottom