UPUUZI WANGU NIKIWAGA SINA HELA!!
Ipo hivi,tuna kizazi ambacho lazima tukilazimishe kufikiri Sio kwa sababu hakiwezi kufikir,inawezekana kimekosa muda wa kufanya hivyo baada ya kuumaliza kwenye Instagrams pages za Diamond,Hamornize na Ally Kiba ,Wema Sepetu ,Zali na Hamisa Mobeto ujua wamepost picha gani
Kwa namna ambavyo maisha ya sasa yalivyo ,sioni namna kwa taaisisi yenye malengo ya kibiashara ikaamua tu hivi hivi ikupatie elfu 84? Bure tu ,kuliko bure yenyewe.Nimeandika huu upuuzi baada ya kusambaa ujumbe unaodaiwa kutoka kampuni ya Vodacom kuwazawadia wateja wake shilingi elfu themanini na nne na kenda.
Ladies and gentlemen dunia na maisha kwa sasa ni ubepari umetamalaki.Ndani ya ubepari hakuna pesa ya bure.Unakula betting laki mbili baada ya muhindi kuwala wengine milioni mbili walizokuchangia.
Usitarajie nitasema hii imetokana na Serikali iliyopo madarakani ,sitosema kwa sababu mimi sio miongoni mwa wasiojua kwamba hata Marekani idadi ya wasiokua na ajira rasmi ni kubwa kuliko walioajiriwa,naweza kuwa na hitimisho kwamba hata Mgombea wangu Hashimu Rungwe angeshinda asingeweza kubadilisha hili.
Suluhu pekee ni sisi tusukosee walipokosea wazazi wetu.Tutafute hela hili watoto wetu wasije kushinda kwenye magroup ya Whatsapp kusambaza ujumbe wa Vodacom.Unapataje hela kwenye ubepari???? .Zipo njia mbili tu,kama huna mtaji hakikisha unakua mbunifu!
2020