Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

IMG_20200907_203047_440.jpg
 
Nilitaka nijue generally ila poa nita google mkuu.
Swali lako halikuwa wazi mkuu. Ndiyo maana nikauliza kama unaulizia kuhusu huyo mtoto ambaye anasumbuliwa na hydrocephalus (kichwa kujaa maji) au kama ni swali la jumla tu kwamba kwa nini watoto wanazaliwa na vichwa vikubwa.

Kama ni swali la jumla kwa kifupi nadhani ni sababu ya ukubwa wa ubongo. Kumbuka kuwa Homo Sapiens ndiye kiumbe mwenye ubongo mkubwa zaidi kushinda wanyama wote (akilinganishwa na uzito wa mwili wake); na kusema kweli ubongo ndiyo silaha yake kuu iliyomwezesha kuwatawala wanyama wengine pamoja na mazingira yake. Kwa hiyo kichwa kinakuwa kikubwa ili kuhakikisha kuwa angalau anazaliwa na ubongo ambao tayari uko katika hali ambayo itampa nafasi ya ku-survive, ubongo ambao utaendelea kukua akiwa nje ya tumbo la mama yake.

Hata hivyo kuna shida fulani hapa ukiangalia vizuri. Pamoja na kuwa na ubongo mkubwa anapozaliwa, ubongo huu unakuwa bado mchanga sana na hauwezi kumfanya ajiendeshee maisha yake japo kidogo. Hii ni kinyume sana na watoto wa species zingine ambapo mtoto anazaliwa na chini ya masaa matatu tayari huyoo ana uwezo tayari wa kukimbia hali ikimlazimu. Ubongo wa wanyama hawa ni mdogo na umelengwa katika kuhakikisha mambo ya msingi katika survival yao tu (mf. kuona na kunusa hatari, kupiga mbio n.k) na ukuaji huu karibu wote hufanyikia wakiwa tumboni. Ili kufikia hali hiyo, hata hivyo, mtoto wa binadamu ingebidi abakie tumboni mwa mama yake kwa angalau miaka minne au mitano kabla hajazaliwa ili kuhakikisha kuwa ubongo wake unakomaa kiasi cha kumpa uwezo wa kusimama, kukimbia na hata kujifanyia vitendo muhimu kuhakikisha survival yake. Lakini hapa napo kuna shida. Njia ya kutokea ni ndogo mno na kukaa tumboni kwa miaka mitano, japo kungetoa nafasi kwa ubongo wake kukomaa sawa sawa, kichwa chake kingekuwa kikubwa mno na isingewezekana kutoka. Na akina mama kubeba mimba kwa miaka mitano ingekuwa sekeseke sana.

Kwa hivyo kinachofanyika ni kuhakikisha ubongo unakua kiasi cha kufikia hatua ya kuwezesha mambo ya msingi kufanyika na ukuaji mwingine hufanyikia nje ya tumbo la mama. Wanasayansi sasa wanaamini kuwa ubongo wa binadamu pengine huendelea kukua na kujiimarisha mpaka mtu anapofikisha miaka 24!

Maelezo marefu ya kimawanda tu lakini jibu fupi ni kwamba watoto wanakuwa na vichwa vikubwa sababu ya kuwa na ubongo mkubwa. Na ubongo mkubwa ulio tayari kuendesha shughuli za muhimu huku ukiendelea kukua ukiwa nje ya tumbo la mama (baada ya miezi 9 tu) ndiyo kila kitu kwa Homo Sapiens ambaye, bila ubongo wake unaompa ujanja wa kila aina, kusema kweli ni kiumbe mnyonge sana ukimlinganisha na wanyama wengine huko Serengeti...
 

Hebu sisiemu muwe mnatumia akili zenu wakati mwingine sio kuendeshwa kimuhemko tu.

Hao viongozi hela wanazo wanaeza kupanda hizo ndege (Swali labda jee kwanini wazipande hizo? Sababu ni kuwa serikali imefanya uhuni kuuwa mashirika mengine ambayo tangu mwanzo yalikuwa yakifanya kazi zake vizuri hivyo hawana jinsi kupanda hizo)

Serikali ingetakiwa ijikite kwenye mambo yanayogusa wengi na sio wachache. Imejiingiza kwenye biashara ambazo mashirika mengine yanaweza hudumia hali ya kuwa wananchi wake wanateseka na ukosefu wa Maji wengine madawati shuleni hakuna. Bado zinatupa hasara alafu tunaendelea kuzifidia hasara kwa kodi zetu.
 
Hebu sisiemu muwe mnatumia akili zenu wakati mwingine sio kuendeshwa kimuhemko tu.

Hao viongozi hela wanazo wanaeza kupanda hizo ndege (Swali labda jee kwanini wazipande hizo? Sababu ni kuwa serikali imefanya uhuni kuuwa mashirika mengine ambayo tangu mwanzo yalikuwa yakifanya kazi zake vizuri hivyo hawana jinsi kupanda hizo)

Serikali ingetakiwa ijikite kwenye mambo yanayogusa wengi na sio wachache. Imejiingiza kwenye biashara ambazo mashirika mengine yanaweza hudumia hali ya kuwa wananchi wake wanateseka na ukosefu wa Maji wengine madawati shuleni hakuna. Bado zinatupa hasara alafu tunaendelea kuzifidia hasara kwa kodi zetu.
Huku nilipo serikali imekarabati shule, imejenga kisima na barabara imewekwa lami.

Kagombee na wewe ufanye hayo ya wengi.
 
Anaweza kupanda ndege yoyote hata isipokuwa Air Tanzania maana ana HELA, kwani alipanda kwa msaada humo? Suala la kujiuliza WEWE au BABA yako mnatumia hizo ndege kama mnavyotumia UDART?
Ukiwa mpinzani lazima dish liyumbe kama ww, sidhan kama umeelewa point ya hy pic
 
Back
Top Bottom