Vituko mitandaoni. Tupia chako

View attachment 2952730
Kwani siku hizi wanapandikiza moyo?
Ndiyo. Ni operesheni ya kawaida tu. Nadhani hata Muhimbili wanafanya kama sikosei japo wenye hela zao huwa wanakimbilia nje.

Marekani kule ukienda kukata leseni ya udereva unaulizwa kama unataka kuwa organ donor. Ukikubali leseni yako inakuwa na alama ya moyo kwa nyuma na neno Organ Donor.

Siku ikitokea umepata ajali na huwezi kupona basi wanavuna viungo vyote ambavyo havijaharibika na kwenda kuvipandikiza kwa wanaovihitaji ambao huwa ni wengi. Ndiyo maana biashara ya viungo vya binadamu ni biashara ya mabilioni ya dola kwa mwaka maana kuna waiting list ndefu sana kwa viungo hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…