Beatrice James Minja (47) mkazi wa Tarakea, Rombo anapigania maisha yake kitandani. Alijeruhiwa kwa kuchomwa visu 25 na Bw.Paul Tarimo ambaye anadaiwa ni mfanyakazi wa Prof.Adolf Mkenda, Mbunge wa Rombo na Waziri wa elimu.
Beatrice na Paul walikua kwenye mahusiano lakini Paul akawa anamtesa kwa vipigo vya mara kwa mara. Amewahi kumpiga mpaka mimba ikatoka. Beatrice alitafuta suluhu kwa muda mrefu bila mafanikio. Hatimaye akaamua kuondoka na kwenda kuanza maisha yake.
Kabla ya kuondoka Tarimo alimpora kiasi cha 10M ambazo zilikua mtaji wa biashara pamoja na pesa za ujenzi wa nyumba ya mama yake. Beatrice aliripoti polisi lakini Tarimo hakuwahi kuitwa kuhojiwa.
Beatrice alipoondoka kwa Tarimo aliacha baadhi ya mali ikiwemo nguruwe wakubwa 6 na vitoto 11. Baada ya Beatrice kuondoka Tarimo alienda kwenye banda na kukatakata nguruwe wote pamoja na vitoto. Bado polisi hawakufanya lolote.
Tarehe 13/11/2023 saa 12 jioni Beatrice akiwa na akina mama wengine wawili, walishambuliwa na Tarimo, ambaye alimkwida Beatrice na kumchoma jumla ya visu 25 maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Alikimbizwa hospitali ya Huruma lakini alipewa rufaa kwenda KCMC. Tayari ameshafanyiwa operation kubwa 2 za tumbo, na ameshonwa jumla ya majeraha ya nje zaidi ya 20. Kwa sasa yupo ICU. Yupo kwenye mstari mwembamba kati ya kifo na uzima. Wakati huohuo Tarimo anaendelea na shughuli zake kama vile hakuna kilichotokea.
Beatrice ana watoto wawili ambao aliwazaa kabla hajakutana na Tarimo. Mmoja yupo chuo kikuu UDSM mwaka wa 3 na mwingine yupo darasa la 5. Katika hali ya kushangaza Tarimo amesema atawasaka watoto hao na kuwaua. Watoto hao wameripoti kutishiwa maisha kwenye kituo cha polisi Tarakea lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
#MyTake:
Polisi kwanini mnasita kuchukua hatua dhidi ya Bw.Paul Tarimo? Mtu anachomwa visu 25 hadharani na mtuhumiwa anatamba mtaani? Lini mmekua "goigoi" kiasi cha kuogopa watuhumiwa? Mnataka Beatrice afe ili mseme mlikosa ushahidi wa kumkamata Tarimo? OCD Rombo hivi Beatrice angekua mwanao, huyo Tarimo angekua uraiani hadi sasa? IGP Wambura tafadhali shughulika na OCD Rombo na askari wake maana wanafanya jeshi la polisi litukanwe unnecesarily.!
Sent using
Jamii Forums mobile app