RAY C AENDELEA KUMKALIA KOONI LAD JAYDEE
"Sina Twitter nitakujibu hapa, wewe ukijiangalia kwenye kioo tu ni depression tosha, umuue nani kwa depression sasa kwa lipi hasa? Kutwa kutembea na michupa ya pombe kwenye gari hivi huwezi kuwa sawa bila kunywa hiyo mipombe kila siku? kama hujui basi nakujuza you are alcoholic you need Jesus! Acceptance and Rehab. Kuzomea mapito ya wenzio haitakujenga, chuki zako wewe kwangu ni za miaka na miaka, labda watoto wa juzi hawajui"
"Najua huamini kama nimesimama tena ndio maana una wenge, nilikuachia nafasi miaka nikataabika, ungefanya basi ya maana ufike levo za kina Tiwa Savage lakini wapi, anyway tuongee kiutu uzima wewe ni mkongwe nadhani ulitakiwa usiwakebehi watu wenye depression unatakiwa uwe makini na mambo uyaandikayo kwenye platforms zako maana watu wanajinyonga kila siku sababu ya msongo wa mawazo ( mental health is real)"
Familia nyingi tu zinateseka, so kashfa haikufanyi wewe uwe bora kuliko wengine maana kila mtu ana mapito yake kwenye hii dunia, ingekuwa mtu ana uwezo wa kuchagua pito basi nina uhakika anayeteseka na kansa leo pale ocean road angechagua gonjwa lingine. Nadhani kwanza wewe mwenyewe labda hujui ngoja nikujuze, kwa experience yangu niliyoipata pombe ina addiction mbaya mnoo na ina madhara makubwa tu"
"Ukiendekeza kunywa kama ufanyavyo mbeleni unaweza jisababishia matatizo makubwa tu, tafuta msaada wa kisaikolojia eidha uende Rehab maana zipo nyingi za wenye uraibu wa pombe. Unajua kuna umri ukifika alafu vitu fulani hujaweza kufanikisha mtu anaweza vurugwa akajikuta anaongea hovyo hovyo tu ilimradi kujiburudisha angali ndani ya moyo ana mengi yanamsibu, ama ukajikuta unalewa tu hovyoo huwezi lala bila pombe"
"Naomba nikushuhudie leo naona Ukuu wa Mungu kwenye maisha yangu sababu nilikubaliana na hali nikakubali kuwa nina tatizo na nikakubali kupata msaada wa kisaikolojia. Leo hii natembea huku nang'ara maana Mungu wangu kaniheshimisha, kwahiyo hujachelewa dada, maisha bila mipombe inawezekana, maisha bila madawa inawezekana ni kuamua tu bidada"- Ujumbe wa Ray C kwa Lady Jaydee
**********************************

View attachment 2843812
Sent using
Jamii Forums mobile app