Vitu vya kuzingatia ili kuwa na afya na kuishi miaka mingi

Uliowekwa na nani?
Kwa mujibu wa Biblia muda tuliowekewa wanadamu wa kuishi duniani ni miaka 120. Umri huo wangapi wanaufikia? Nafikiri sababu mojawapo ni kutozingatia vigezo na masharti ya kuishi. Kijana wa miaka 30 anampiga baba yake; baba anamlaani...laana inampata...kijana anapata ajali, anafariki. Hapo utasema kijana amekufa kwa sababu aliwekewa kuishi miaka hiyo michache? No, please.
Miaka tuliyopewa ni 70, 80 ikiwa tuna nguvu, wanaozidi bonus ya zaidi ya miaka 80 ni kwa neema ya Mungu tu. Zaburi 90:10.
Ukipata nafasi soma Zaburi ya 90 yote.....
 
Je, unapenda kuishi maisha marefu? Kwa ujumla, hakuna mtu asiyetaka kuishi miaka mingi na kuwa na afya njema. Wanasayansi na wataalamu mbalimbali wamethibitisha kuwa ukizingatia mambo yafuatayo unaweza kujiongezea miaka au umri wa kuishi duniani:
1. Hakikisha unakula vyakula vyenye virutubisho vyote muhimu
2. Epuka unene uliopitiliza. Uzito wa mwili wako usizidi viwango vya uzito vinavyokubalika kiafya
3. Usivute sigara
4. Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku na unywe maji ya kutosha
5. Usikae kivivuvivu - uchangamshe mwili wako kwa kufanya kazi
6. Epuka msongo wa mawazo; ishi na wenzako kwa furaha
7. Zingatia sheria za usalama barabarani
8. Jitahidi mara kwa mara kwenda hospitali kupimwa afya yako
9. Epuka ulevi
10. Pata muda wa kutosha wa kulala usingizi.
Wasomi wa Maandiko matakatifu, wamegundua jambo jingine linaloweza kumfanya mtu aishi miaka mingi. Jambo hili tunalisoma katika kitabu cha Waefeso 6:2-3(BHN). Imeandikwa hivi: “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”

Kwakuwa ahadi hiyo imetolewa na Mungu mwenyewe, ni hakika kwamba tukitekeleza agizo hilo - tukiwaheshimu wazazi wetu, Mungu atafanya kama alivyoahidi - atatupatia maisha ya heri na kutuwezesha kuishi miaka mingi duniani.

Hiyo ni siri iliyofichika kwa wengi, lakini leo imefunuliwa kwetu!
Na niaminivyo mimi ni kwamba, baba na mama sio wale tu waliotuzaa, ni pamoja na wote wenye umri unaozidi au unaolingana na umri wa wazazi wetu. Tuwaheshimu wote. Tusikwaruzane nao. Tusiwanyooshee vidole. Tusiwakaripie. Tusiwadharau hata kama tunaona wamepitwa na wakati.
Iyo namba moja ndio inayotumika ulaya...

Huku kwetu tunaletewa ngano grade F huko
 
11. Usijihusishe na vitendo vyovyote vya kihalifu kama vile Ujambazi, uzaaji wa dawa za kulevya na wizi.
utaishi miaka mingi tena kwa amani na utulivu wa moyo.
 
Uhai ni tunu unayopewa.. you don't earn it you didn't get it for a certain favor.
Aliekupa uhai ndio anaweza kukuamulia uishi muda gani. Usiniambie kua wazungu wanaishi muda huo kwakua wanahuduma bora ya afya
Kwa jibu hili tu mjadala na wewe kuhusu hii mada ninaufunga rasmi.
Have a nice day!
 
Back
Top Bottom