Fahamu chakula unachopaswa kula ukiwa na zaidi ya miaka 40

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Chakula ni kirutubisho muhimu sana kwa wanadamu na maisha hayangewezekana bila lishe bora.

Hata hivyo licha ya umuhimu wa lishe kwa mwili wa mwanadamu, wataalamu mara nyingi huwa wanazingatia faida za lishe bora na kiwango cha chakula ambacho mtu anapaswa kula kwa ajili ya afya yake.

Wataalamu wametoa angalizo pia na kutoa tahadhari dhidi ya aina ya chakula ambacho watu wanapaswa kula kutokana na hali yao ya kiafya au umri.

Lakini kadri mtu anavyozeeka, kuna aina za vyakula ambavyo mtu anahitaji kula mara kwa mara.

Ukiendelea kuzeeka, unashauriwa ni aina gani ya vyakula unapaswa kula mara kwa mara ili kuboresha afya yako na kinga ya mwili.

Lishe bora ukiwa na miaka 40
Daktari wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Ilorin cha Nigeria, Dkt Sadiya Musa anasema ukifika miaka ya 40,kwa kawaida ni muhimu kubadilisha lishe.

Anasema ni muhimu kwa mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 40 kuwa muangalifu na afya yake kwa sababu kadri mtu anavyozeeka anaweza kupungua uzito pia.

Hivyo inakuwa rahisi kupata magonjwa.
Mtu mwenye umri mkubwa anahitaji lishe bora ambayo itamfanya kuwa na afya na nguvu, anasema Dkt Sadiya.

Kutokuwa makini katika lishe ukiwa na miaka hiyo, ni hatari kwa afya wakati ambao utapata magonjwa kama kisukari, presha na matatizo ya miguu kunaweza kuathiri mtu.

Dkt Sadiya anasema vyakula ambavyo mtu mwenye umri wa miaka 40 anatakiwa kula ni pamoja na:

Samaki
Mboga za majani na mizizi kama moringa,
Matunda
Kula uyoga badala ya nyama
Vyakula vya protini kama maharage ya soya badala ya mayai
Ni muhimu kufanya vipimo vya damu ili kusaidia kupunguza hatari za maambukizi, kwa mujibu wa daktari.

Kupunguza kula vyakula vinavyohifadhiwa kwenye makopo

Kupunguza matumizi ya limao ni hatari kwa afya

Kupunguza kiwango cha chumvi katika chakula

Kupunguza kula nyama, karanga na siagi
Daktari amesema pia mtu akifika umri huo hapaswi kuacha kula vyakula alivyozoea ghafla badala yake anapaswa kuacha taratibu mpaka atakapoacha kabisa haswa kwa wale wenye matatizo ya kisukari na presha.

Vyakula asili
Licha ya kwamba daktari ameshauri kula vyakula vinavyoboresha afya, ni vyema kupunguza vyakula ambavyo ni hatari kwa afya kwa kuzingatia umri.

Ni muhimu kudhibiti matumizi ya dawa za mitishamba au dawa za hospitalini bila maelekezo ya daktari pia ni hatari kiafya, kwa mujibu wa daktari.

Pia ni muhimu kula vyakula vya asili kama vile mahindi, mtama, maboga na vinginevyo.

Moringa
Moringa ni chakula maarufu cha asili ambacho ni muhimu.

Jizuie kula vyakula ambavyo vina kemikali.

Dkt Sadiya, anasema watu ambao hawana magonjwa ya kisasa wanawezekana kuwa na lishe bora zaidi.

Aidha daktari amesema watu wenye afya bora, ni kutokana na aina ya chakula cha asili wanachokula na wengine wanapata magonjwa kutokana na uchaguzi mbaya wa chakula.

Chanzo: BBC
 
Ukifuata maoni ya kila mmoja ya hawa wataalamu uchwara wa lishe hutakula cho chote. Leo huyu atasema hivi. Kesho mwingine atasema hivi ali mradi vurugu tupu.

Ukimsikiliza Profesa Janabi ndo hutasogelea chakula kabisa. Anakwambia ana miaka zaidi ya 10 hajagusa chapati, mkate wala andazi na hata wali/ugali. Sababu eti ni carbohydrates na ni hatari sana kwa afya yako.

Sasa kweli jamani Msukuma kama mimi ndo nisile ugali kabisa kabisa kisa naogopa kunenepa au magonjwa? Maisha yana faida gani bila ugali?

Ili kuepuka upopoma huu wa hawa washauri mimi nina kanuni moja. Naepuka vitu vya hatari vilivyothibitishwa kisayansi kuwa vina madhara (mf. sigara, pombe, exygenated oils, processed foods...). Vingine vyote nakula in moderation na nabadilisha badilisha. Vimazoezi vya hapa na pale. Kila mwaka comprehensive physical exam. I know my important numbers (BP, Sukari na lehemu) na mambo mengine ya muhimu.

That's how you enjoy life vinginevyo utaishi kwa hofu kama vile utaishi milele. Na ugali nilishasema siachi ng'o!
Screenshot_20230121-230640_Samsung%20Internet.jpg
 
Back
Top Bottom