Vitu vya kuzingatia ili kuwa na afya na kuishi miaka mingi

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Je, unapenda kuishi maisha marefu? Kwa ujumla, hakuna mtu asiyetaka kuishi miaka mingi na kuwa na afya njema. Wanasayansi na wataalamu mbalimbali wamethibitisha kuwa ukizingatia mambo yafuatayo unaweza kujiongezea miaka au umri wa kuishi duniani:

1. Hakikisha unakula vyakula vyenye virutubisho vyote muhimu
2. Epuka unene uliopitiliza. Uzito wa mwili wako usizidi viwango vya uzito vinavyokubalika kiafya
3. Usivute sigara
4. Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku na unywe maji ya kutosha
5. Usikae kivivuvivu - uchangamshe mwili wako kwa kufanya kazi
6. Epuka msongo wa mawazo; ishi na wenzako kwa furaha
7. Zingatia sheria za usalama barabarani
8. Jitahidi mara kwa mara kwenda hospitali kupimwa afya yako
9. Epuka ulevi
10. Pata muda wa kutosha wa kulala usingizi.

Wasomi wa Maandiko matakatifu, wamegundua jambo jingine linaloweza kumfanya mtu aishi miaka mingi. Jambo hili tunalisoma katika kitabu cha Waefeso 6:2-3(BHN). Imeandikwa hivi: “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”

Kwakuwa ahadi hiyo imetolewa na Mungu mwenyewe, ni hakika kwamba tukitekeleza agizo hilo - tukiwaheshimu wazazi wetu, Mungu atafanya kama alivyoahidi - atatupatia maisha ya heri na kutuwezesha kuishi miaka mingi duniani.

Hiyo ni siri iliyofichika kwa wengi, lakini leo imefunuliwa kwetu!
Na niaminivyo mimi ni kwamba, baba na mama sio wale tu waliotuzaa, ni pamoja na wote wenye umri unaozidi au unaolingana na umri wa wazazi wetu. Tuwaheshimu wote. Tusikwaruzane nao.
Tusiwanyooshee vidole. Tusiwakaripie. Tusiwadharau hata kama tunaona wamepitwa na wakati.
 

testifier

Member
Apr 21, 2021
47
125
Heshima kwa wazazi ni sawa. I do agree. But kuna wazazi ni wachokozi. Kwa mfano, unawezakuta baba au mama anamlazimisha kijana wake amuoe binti wa ukoo fulani wakati kijana hampendi huyo binti. Hapo vipi. Au baba anawalazimisha watoto waishi kama yeye baba anavyotaka, wakati watoto wanataka to go with time. Hapo ugomvi si lazima utafumuka?
 

testifier

Member
Apr 21, 2021
47
125
Enjoy what you're being served...Huwezi kuongeza umri wako uishi muda zaidi ya uliowekwa
Uliowekwa na nani?
Kwa mujibu wa Biblia muda tuliowekewa wanadamu wa kuishi duniani ni miaka 120. Umri huo wangapi wanaufikia? Nafikiri sababu mojawapo ni kutozingatia vigezo na masharti ya kuishi. Kijana wa miaka 30 anampiga baba yake; baba anamlaani...laana inampata...kijana anapata ajali, anafariki. Hapo utasema kijana amekufa kwa sababu aliwekewa kuishi miaka hiyo michache? No, please.
 

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Hii nayo ni chai

Maisha ya Kila mtu yapo programmed

Huwezi kurefusha labda ufupishe
Mkuu, umewahi kusoma habari za Hezekia? Kama maisha yako programmed huyo Hezekia angekufa kwa ugonjwa kabla ya wakati wake. Lakini alijua siri ya kurefusha maisha yake. Alimuomba Mungu kwa bidii na Mungu akamponya na kumuongezea miaka 15 zaidi ya kuishi. Ina maana angeacha kuomba angekufa mapema.

Habari kamili hii hapa:

2 Fal 20:1-6​

Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA akasema, Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la BWANA likamjia, kusema, Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA. Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.
 

Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,012
2,000
Umemsoma Einstein kwenye General na special relativity??
Anaseama kwamba muda ni Relative. Utawahi kwakua mimi nimechelewa au utachelewa kwakua mimi nimewahi hakuna aliye kwenye muda.
Tuachane na Einstein..

Kiroho.. kwa Mungu hakuna muda! Hakuna jana wala kesho everything is in Present form muda upo kwako wewe mwanadamu ili ukuue na kuhesabu majira (Time is what makes you die)
Hivyo basi kila mtu kapewa mida wake wa kuishi pindi tu muda wako ukishawekwa wa kuishi asi huwezi kuuongeza au kuupunguza labda upate favor kutoka kwa Mtoa uhai maana kuna sehemu anasema kwamba miaka yako ya iliyoliwa na mchwa nitaiongeza

Hata ufanye vipi huwezi kuishi zaidi ya ule muda uliopangiwa kuishi. Ikifika imifika. Mtu akifa na miaka 2,10,25,20,30,40, wewe mwenye miaka 80 usimuone mzembe na mjinga...Kila mtu anaishi muda wake.

Enjoy what you're being served...Huwezi kuongeza umri wako uishi muda zaidi ya uliowekwa
Hii imeeleweka kwangu. Swali moja mkuu, zile life span zinazowekwa na wanataaluma huwa wana-refer nini hasa? Utasikia sijui, life span ya Mjapani ni 75yrs wakati ya Mmatundi ni 49yrs?

Wanaangalia wastani wa umri wa watu wanaokata moto au?
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,631
2,000
Mimi sivuti sigara lakini hiyo namba 3 usivute sigara ni uongo.
Nchi zinazoongoza kwa kuvuta Sigara duniani moja wapo ni Japan.Wastani wa umri wa mtu wa Japan ni zaidi ya miaka 85

Rudia utafiti na si kusoma madesa ya kitanzania yana vitu walikaririshwa tu
 

Ngorunde

Platinum Member
Nov 17, 2006
2,507
2,000
Hata ufanye vipi huwezi kuishi zaidi ya ule muda uliopangiwa kuishi.
Huu ndio uafrika kamili. Kulishana matango pori.

Wakati wenzetu(nchi zilizoendelea) wakifanya utafiti wa kuongeza siku za kishi, huku kwetu tunapeana story za ajabu ajabu...eti siku za kuishi zimepangwa😅

Ina maana watoto wa kizungu wamepangiwa wasife wengi huku wa kiafrika wakapangiwa wafe lundo kwa utapiamlo, malaria na magonjwa mengine ya kizembe ambayo yangeweza kuzuilika??

Mkuu acha hizo bhana!
 

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Mimi sivuti sigara lakini hiyo namba 3 usivute sigara ni uongo.
Nchi zinazoongoza kwa kuvuta Sigara duniani moja wapo ni Japan.Wastani wa umri wa mtu wa Japan ni zaidi ya miaka 85

Rudia utafiti na si kusoma madesa ya kitanzania yana vitu walikaririshwa tu
Miaka tunayopaswa kuishi duniani ni 120. Kama Wajapan wanaishi wastani wa miaka 85 basi ni kweli uvutaji sigara unawapunguzia miaka ya kuishi
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,778
2,000
Uliowekwa na nani?
Kwa mujibu wa Biblia muda tuliowekewa wanadamu wa kuishi duniani ni miaka 120. Umri huo wangapi wanaufikia? Nafikiri sababu mojawapo ni kutozingatia vigezo na masharti ya kuishi. Kijana wa miaka 30 anampiga baba yake; baba anamlaani...laana inampata...kijana anapata ajali, anafariki. Hapo utasema kijana amekufa kwa sababu aliwekewa kuishi miaka hiyo michache? No, please.
Unapimaje kama huyo kijana amakufa kwa laana .
Kama huyo kafa kwa laana ya kugongwa na gari, kwa hio wote wanaokufa kwa kugongwa na gari walilaaniw. Je kwa nini mlaani amsababishie mwengine kifo wakat naye kifo kitamchukua?
 

Ngorunde

Platinum Member
Nov 17, 2006
2,507
2,000
Kifo kinasababishwa na Muda au unakataa mkuu???
Hapo ninakubaliana na wewe kwa maana moja tu..ili mtu a qualify hiyo stage kifo against muda ni lazima alindwe asidhuriwe na magonjwa ya kizembe.
Vipi, tunakubaliana mpaka hapo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom