Vitu vinikeravyo mjini Dar

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Kuna vitu viwili ambavyo vinanikera sana hapa Dar,moja ni watu wanavyo gombania kuingia kwenye daladala badala ya kupanga foleni na kuingia kistaarabu bila kukanyagana na kuumizana.Mara nyingine hii husababisha kuchafuliana nguo,kuibiwa na hata kuchaniana nguo.Hili swala la kugombania usafiri halipo nchi za jirani kama Kenya,Malawi hata Zambia likija basi watu wanapanga foleni na kuingia kistaarabu.
Jambo la pili ni jiji kubwa kama hili kuwa na kituo kimoja tu cha zimamoto na moto ukitokea pembezoni ya jiji uwezekano wa kupoteza kila kitu ni mkubwa sana.
 
Pole sana lagatege, we sijuhi ndio umeingia hivi karibuni dar au ni mwenyeji, nadhani ujawahi kukutana na mvua ya dar ukaiona kero yake, vipi kuhusu foleni ya dar, habari za maji vipi mwenzetu, joto je
 
Kupanga mstari kwa ujumla ni tatizo.

Sidewalks mjini ziko ovyo sana, hakuna standard kila mtu anajenga kwa level yake, anaweka vizingiti, minyororo, maua makuubwaaa! PLUS magari yanaparamia sidewalk hadi hakuna pa kupita.

Uvunjaji wa sheria za barabarani! Mtu anaweza akaanza kugeuza gari katikati ya barabara, haoni tatizo!

Utumiaji ovyo wa honi!

Vumbi!
 
Ukiyafikiria sana matatizo ya Dar unaweza kuhama hata mji. Tuzidi kuvuta subura "planners bado wapo kazini wana plan kuleta fly-overs, mabasi yaendayo kasi, treni za chini ya ardhi, boti toka bagamoyo to dar, watapanua TRL kuservice maeneo ya katikati ya jiji na pembezoni, n.k baada ya muda kero zitakwisha kabisa"
 
Haya yakitimia, Dar itaingia kwenye yale maajabu saba ya ulimwengu.
 
Msilalame tu na mambo hayo DAR,jaribuni kusafiri na kuchunguza hayo mambo watu wanagombea hata hizo speedtrain kwenye pick hrs. itakua daladala!!!!!!

Sasa mbona umeniqoute mimi wakati hata sijazungumzia daladala mkuu? Hivi unajua majority ya wachangiaji humu ni watu ambao wako nje ya nchi?
 
Sorry pronto!

unajua nilihisi ni kati ya wale wale ambao hatuhishi kulalamika vitu vya kijingajinga.
kutokuwajibika kwetu kwenye shuguri za kulijenga Taifa hili ndio kumetusababisha leo kufikia hapa hata hatuna hata moja ya hizo barabara za juu au mambo yote mazuri wenzetu waliondelea pamoja na scarce resources wanayo,pamoja na utajiri wetu hatuna hata cha kujivunia zaidi ya UFISADI.
 
Dar wakati wa mvua ni balaa la kutisha. Mitalo ya kupitisha maji machafu hakuna, uchafu umezagaa kila kona, umeme hakuna, maji safi na salama hakuna, joto kali ile mbaya, mbu wanaimba nyimbo zao masikioni, kila nyumba ni grocery na music mkubwa ile mbaya. Ni kwa nguvu na kudra za mungu watu tunaweza kuendesha maisha hapa Dar.
 
Ukiyafikiria sana matatizo ya Dar unaweza kuhama hata mji. Tuzidi kuvuta subura "planners bado wapo kazini wana plan kuleta fly-overs, mabasi yaendayo kasi, treni za chini ya ardhi, boti toka bagamoyo to dar, watapanua TRL kuservice maeneo ya katikati ya jiji na pembezoni, n.k baada ya muda kero zitakwisha kabisa"

He he he..keep on dreaming..
 
Dar wakati wa mvua ni balaa la kutisha. Mitalo ya kupitisha maji machafu hakuna, uchafu umezagaa kila kona, umeme hakuna, maji safi na salama hakuna, joto kali ile mbaya, mbu wanaimba nyimbo zao masikioni, kila nyumba ni grocery na music mkubwa ile mbaya. Ni kwa nguvu na kudra za mungu watu tunaweza kuendesha maisha hapa Dar.

Mazee una akili sana... do u know what does that means? ina maana moja tu kuwa pamoja na miaka zaidi ya 40 ya uhuru the most commercialized city of Tz is still taken hostage by nature..thats shows how irrelevant our government is..
 
Yaliyopita ndiyo ya kulaumiwa wao, ila haya yaliyopo na yajayo ni yetu wote tusijidanganye kuwanyooshea vidole wengine! Tukuneni vichwa tupate ufumbuzi wa haya matatizo ya jiji letu hili zuri.
 
duu ndugu yangu hilo jina lako si mchezo, ni la kiruga au
 
Dar wakati wa mvua ni balaa la kutisha. Mitalo ya kupitisha maji machafu hakuna, uchafu umezagaa kila kona, umeme hakuna, maji safi na salama hakuna, joto kali ile mbaya, mbu wanaimba nyimbo zao masikioni, kila nyumba ni grocery na music mkubwa ile mbaya. Ni kwa nguvu na kudra za mungu watu tunaweza kuendesha maisha hapa Dar.
mnaolalamika joto. , na kama joto sana basi wekeni AC au nunueni fan.
 
Back
Top Bottom