Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,592
- 29,711
Lengo la serikali kuwekeza katika mkundombinu iliyotuletea huduma ya mabasi ya mwendokasi ni kupunguza usumbufu utokanao.na foleni kubwa za magari wakati wa kuingia na kutoka mijini. Hasa nyakati za ahsubuhi na jioni.
Mimi na baadhi ya wadau tunaamini kuwa huduma hii inapaswa kurahisisha movement ya wananchi hususani wanaotingia na kutoka mijini hasa wanaoishi pembezoni mwa miji.
Jiji la Dar es Salaam limegawanyika katika maeneo makubwa matatu.
Kwa mfano kituo cha Mbagala hakijawahi kukauliwa abiria kwa saa 24 muda wote wa mwaka. Hata kibiashara mbalimbali eneo hilo lipo hai muda wote wa saa 24.
VIvyo hivyo maeneo ya Mbezi Luis yaani Mbezi mwisho kunakuwa na polika za ussfiri saa 24 ambapo inapofikia usiku wa saa 5 hivi kituo kinahamia barabara kuu ya Morogoro. Ukizunguka jiji la Dar usiku utagundua kuna maeneo watu hawakauki katika saa 24 za siku. Eneo la Kariakoo hususani makutano ya Uhuru na Msimbazi ni eneo ambalo linakuwa kama mchana muda wote.
Serikali kwa kujali ama kuangalia namna ya kurahisisha usafiri wa katikati ya jiji, ingeweka mkakati wa kuhakikisha huduma ya usafiri wa mwendokasi unapatikana muda wote. Sipendekezi mabasi yote yatumike kusafirisha abiria bali kuweka utaratibu wa basi mbili au tatu ambazo zinaanzia Kimara, kupitia Moroko, Gerezani hadi Kivukoni. Nasema hivyo kwa sababu wakati jiji limelala wapo watu ambao wanatoa huduma muhimu usiku wanapaswa kuwahi ama.kurejea makwao. Manesi, askari, sexual workers, wafanyabiashara na abiria wanaoingia kutoka mikoani usiku wote wanahitaji kufika either destinations zilizopo njia inayopita mwendokasi au katikati ya mji ambapo wanachukua feeders za daladala kutoka nje ya jiji.
Kwa mapenzi mema na kuzingatia lengo la huduma ya mabasi ya UDART, serikali izimgatie kuruhusu mzunguko wa uchumi kufanyika saa 24 na hatimaye tutazoea kufanyakazi kwa shift ili kukuza uchumi wetu.
Je Great Thinkers wenzangu mnalionaje suala hili la kuwepo kwa basi moja au matatu ya Mwendokasi yatakayotoa huduma kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 10.00 alfajiri?

- Maeneo yenye shughuli za biashara, haya maeneo yameunganika na vituo muhimu vya usafiri wa abiria wengi
- Maeneo ya ofisi mbalimbali ambayo yapo katikati ya jiji
- Maeneo ya makazi ambayo yamesambaa kutola.kati hadi.pembezoni mwa mji