Vitu mwanaume anavyotakiwa kuwa ameshavifanya akifikia miaka 30

Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,023
2,000
Mwaka unaisha na midomo inaanza kujiandaa kutamka umri mpya. Kufikia kipindi kama hiki mwakani panapo uzima, karibia kila mtu atakuwa ameshatamka umi wake mpya. Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.

Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtoto wa kiume lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia: Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
- Kuoa msichana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
- Kuoa chap chap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
- Kunogewa na usela na kusahau kuoa


2)Kujitegemea kiuchumi: Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.

3) Kuwa na kitega uchumi: Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI

4) Makazi: Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Huyu Moyes wamuondoe kabisa)!

5)Uwe na professional qualification: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo niaje!

6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea: Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia mda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama ruba till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.

7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea: Ka we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.

8) Uwe na busara: Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau!

9) Savings: Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa, Ukiacha kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote na kuishi maisha yale yale.


10) Umjue Mungu: Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni maskini).

Asante sana Nd. katawa

upeo na maarifa niliyonayo leo hii natamani ningekuwa hivi nilivyo leo nilipokuwa na miaka 30.
kijana wa miaka 30 inatakiwa ajue kuwa maisha yanabadilika kwa kasi.Jambo analoweza kufanya leo km vile kununua uwanja,kujenga nyumba ya kuishi au biashara afanye wala asisubiri miaka michache ijayo.
kijana ktk umri huu yampasa kuwa mbunifu,mpambanaji na mvumilivu asiyekata tamaa hususani kwenye malengo yake ya kupata kipato halali.
Pia anatakiwa kujua siasa nzuri au mbaya zaweza kuharibu mustakabali wa maisha yake kwaiyo inampasa ashiriki kwenye kuchagua viongozi.

A True Copy.

Tized.
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,222
2,000

7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea: Ka we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.


Mkuu hapo tupo wengi sana, kwenye familia zetu za kiafrika.

Kuna siku nilichukua karatasi na kalamu nikawa nataka niandike mafanikio yangu ya mwaka 2013, tena nilitaka walau nipate vitu vitatu tu tangible, ki ukweli nilipata viwili tu vya maana ambavyo naweza kujivunia. Nilishikwa na uchungu sana kwamba mwaka mzima nasuasua kuonyesha achievements 3? uzi mzuri sana huu.

Ubarikiwe!
 

Mkempia

JF-Expert Member
Mar 5, 2013
1,142
1,500
We unasema 30 mie nimeona 36 mtu hajieleweji kabisa, ukimwambia mbona umri wako unatakiwa uw uesogea zaid ya hapo anakutolea maneno makali hayo. Nikahisi labda kwa kuwa ni wa mwisho kwao kuzaliwa hivyo bado anajiona mtoto.
 

daviey69

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
2,237
1,225
Umeongea vizuri ila kuna matatizo katika mazingira tunayoyaishi...given
mshahara wa below 500,000/= na maisha ya ya kibongo i.e Dar, Arusha etc(housing, electricity, water, food for the family, transport, kuhonga, Bar, baba na mama kijijini wanahitaji matumizi bado wajomba, mashangazi, wadogo.....uwiiiii hata haiumi kama sina hiyo saving!
 

jamiif

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
2,414
1,195
hii hata sisi wadada inatuhusu jamani...motto wa kike kuanzia miaka 25 unatakiwa (km umejaaliwa) uwe kwenye stabe relationship ambayo itakuja kuwa ndoa na sio kuendelea kurukaruka ukidhani bado u motto...unajidanganya mwaya! maana ninaamini umri wetu sisi wakinadada huwa una-expire as ukifika kuanzia 35 huko bado hujaseto ktk relationship ni mtihani na mimi nina wadada nawajua kbs kuwa walikuwa wanachagua sana eti lazima mwanaume atakayemkubali awe ana gari, nyumba, nk...sasa akiangalia wanaokuja kwake wote ni hali za kawaida hawana hivyo anavyotaka yeye so anaishia kuendeleakuchagan hakumbukikwa umri unazidi kwenda. Kchagua sikati ila basi tupunguze makali kdg....kila la kheri kwetu sote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom