Vitimbi gani umefanya enzi za utoto?

Vitimbi gani umefanya enzi za utoto?

Simba Dar? Nadhani hii ilikuwa miaka ya 60 mkuu?
Dah...miye nakumbuka tulivyokuwa tukiiba maembe kwenye shamba la mzungu pale kisutu (ilipokuwa stand)...Tulikuwa tukitoka Magomeni na kuvuka mto msimbazi kwa mtumbwi ambao ulikuwa na viboko na mamba......tukatembea porini kisha tunatokea hospitali ya Sewahaji (sasa hivi Muhimbili)...Tuliacha baada ya kunusurika kuliwa na simba pale Jagwani tena mchana kweupee😀😀😀😀
 
utoto ni shida kuna siku nimerudi shule nikakuta mama hayupo na kuna mtoto wa dada yangu kaachiwa maagizo nisonge ugali, sasa ile nimeanza kusonga ugali tu nikasikia ( kuna jengo lipo hapa maeneo ya KAMATA) linaungua nikaacha ugali jikoni huyo mbio nawafuata watoto wenzangu tukashuudie, na hapo tulikua tunakaa chang'ombe maduka mawili tukakatisha keko......haooo mpk KAMATA nimefika hoi........ mpk jioni ndiyo narudi nyumbani miguu imevimba sababu ya kutembea umbali mrefu, mama karudi na kaacha jkoni vile vile nione sufuria ilivyo nyeusiii uwiii nilipigwaaa sitosahau toka siku ile ilikua mwisho.
 
Nilikuwa nikitumwa chumbani kwa mama kuchukua kitu najipulizia perfume yake ya Yolanda makwapani kisha narudi kupeleka alichonituma nikiwa nimebana mikono na makwapa ili yeye mama asisikie harufu ya perfume kisha nikimbie nje kwa wenzangu niwadoloshie nimepaka perfume ya mama nyie hamjapaka.

Akili yangu ilinituma nikibana mikono harufu haitasikika na mama, kumbe alisikia tangu najipulizia chumbani nilistukia tuu mfinyo wa nguvu kwenye mapaja.

Siku nyingine kaka yangu alikuwa anadokoa maziwa ya unga na sukari akayabwia mdomoni mie nikambamba nikamwambia naenda kukusemea akanishika mkono akaniambia haya njoo nikupe akanipa kidogo nikapige kelele naenda kusema hapo mama yuko sebleni. Akaniambia haya fungua mdomo, akanijazia sukari mdomoni na maziwa kibao halafu muda huo huo mama akaniita hata kuitika abee sikuweza. Nikajifuta mdomo na kuufumba nikijua mama hatajua kama nina kitu mdomoni kumbe mdomo unaonekana kuwa nimefundia kitu, nikaishia kufinywa tuu. Akili za utoto no adventure.
Hahhaa bro wako alikuwa jembe sana
 
Unacheza mpira mpaka giza linaingia, ukirudi tu home-unakutana na angalizo zito,

Ni marufuku kula/kulala hujagusa maji, poa kidume nikajikaza kuchukua maji kwenye mtungi (kulikuwa na mitungi nje ya kuhifadhia maji)nikatia kwenye ndoo, kwa wazoefu wa mtungi unakawaida ya kupooza maji sana.

Dah nafika uwani kugusa maji hivi hayaogeki, nikaaamua kupiga passport, kutoka nje nakutana na bi mkubwa tayari kabisa kwa ukaguzi dah, nikaishia kuwekewa maji mengine nirudi tena kuoga.

Nikiwa chooni natafakari nianzaje, nikapata wazo la kwenda kuchukua makaa ya moto na kuyadumbukiza katika ndoo yenye maji yangu ya kuoga, ili walau nipunguze kaubaridi, nitachukuaje na maza yupo hapo???? faza ndio kakaza nisichemshe maji maana nimezembea mwenyewe naye yuko na panasonic hapo pembeni???nikavizia gap kidogo wametoka nikawahi ile natia mkaa wa kwanza,ukatoa sauti ile ya kuzimika-chaaaaaaaaaaaa maza naye anatokea, wewe unafanya nini???

Alivyogundua lengo langu akaangua kicheko, na faza naye akatokea ile kuambiwa naye akaangua kicheko.kwa huruma na kuzingatua giza/muda na baridi nikaruhusiwa nichemshe.siku ikawa imepita.
 
Mi ilikua ni mwendo wa kutoroka shule huyo naenda zangu kuogolea mto Naura(Arusha) siku ya siku mwenzetu mmoja akashindwa kuogelea(wanasema kanyonywa na chunusi) akafariki kwenye maji.Very bad experience.... na ndio mwisho wangu wa kuogelea mtoni.

Next time tunaenda shule huku kwenye begi tumebeba visoda(vifuniko vya soda) vilivyonyooshwa(tulikua tunavipanga kwenye njia ya reli ili usiku ikifika treni ikipita inavikanyaga vinavyooka vzr) then tunachimba shimo na kutumia hivo visoda kuchezea kamari.Siku ya siku dingi akanifuma nacheza hio kamari mtaani aisee nilipigwa mboko kuanzia mafichoni mpk shulen kama 1.5 kilometres hivi kufika shule dingi kwa sifa akaomba kengele igongwe aniadhibu parade daah ilikua aibu kinoma hahah......by the way ilikua kijenge primary.

Lastly,mimi na chalii angu dennis tulitumwa na walimu wetu kununua maembe makubwa sokoni karibu na hapo shuleni,embe kipindi hicho linauzwa sh. 50 walitupa mia 7 tukalete maembe 14.
Kufika sokoni tukayanunua tukayaosha fresh ile tunayapeleka shuleni sijui pepo gani lilituingia tukaanza kuyala na mshakaji hahah,tulikula kama 6 hivi yakabaki kama 8 tukaona huu msala tayari,hatuwez peleka maembe pungufu kwa walimu so tukagawana ma4 mimi na mwenzangu halafu tukayapeleka home eti tumewaletea zawadi tuliyoipata baada ya kufanya vzr kwenye hisabati hahah(zamani walimu walikua wanatoa motivation kwa wanafunzi uki score vzr).
Sikwenda shule kama siku 2 hivi nikizuga naumwa kumbe nawakwepa walimu maembe yao.siku nimeenda shule tulipewa kichapo heavy na tukaambiwa tukalete maembe yao hahah ikabidi twende home kusema ukweli khs yale maembe hahah,tukaangushiwa kichapo kingine tena kizito hahah.....those good old days..
 
Unacheza mpira mpaka giza linaingia, ukirudi tu home-unakutana na angalizo zito,

Ni marufuku kula/kulala hujagusa maji, poa kidume nikajikaza kuchukua maji kwenye mtungi (kulikuwa na mitungi nje ya kuhifadhia maji)nikatia kwenye ndoo, kwa wazoefu wa mtungi unakawaida ya kupooza maji sana.

Dah nafika uwani kugusa maji hivi hayaogeki, nikaaamua kupiga passport, kutoka nje nakutana na bi mkubwa tayari kabisa kwa ukaguzi dah, nikaishia kuwekewa maji mengine nirudi tena kuoga.

Nikiwa chooni natafakari nianzaje, nikapata wazo la kwenda kuchukua makaa ya moto na kuyadumbukiza katika ndoo yenye maji yangu ya kuoga, ili walau nipunguze kaubaridi, nitachukuaje na maza yupo hapo???? faza ndio kakaza nisichemshe maji maana nimezembea mwenyewe naye yuko na panasonic hapo pembeni???nikavizia gap kidogo wametoka nikawahi ile natia mkaa wa kwanza,ukatoa sauti ile ya kuzimika-chaaaaaaaaaaaa maza naye anatokea, wewe unafanya nini???

Alivyogundua lengo langu akaangua kicheko, na faza naye akatokea ile kuambiwa naye akaangua kicheko.kwa huruma na kuzingatua giza/muda na baridi nikaruhusiwa nichemshe.siku ikawa imepita.

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji115] we jamaa umenifanya nicheke sana. Naona mbinu yako ilikuwa ni balaa. Utotoni tunapitia mengi sana aisee
 
Mm nakumbuka nlikweka kile kichongeo cha penseli chenye kioo chini ili wasichana wakipita nione chu.pi bahat mbaya akapita mwalimu mkuu.

Sitosahau kamwe.
 
Katika maisha mwanadamu hupitia vipindi mbalimbali vya ukuaji...infancy, childhood, adolescence, adulthood, old age & death.

Sasa katika vipindi hivi vya ukuaji kuna wakati, hasa katika vipindi vya utotoni, mtu hujikuta unafanya vitimbi ambavyo kamwe huwezi kuvifanya ukubwani.

Nakumbuka utotoni nimefanya vituko kadhaa ambavyo nikivikumbuka leo hii najishangaa sana. Wakati ule wa utoto nikirudi mchana kutoka shule nisikute chakula nilikuwa nakasirika sana hadi ikitokea nikajikwaa kwenye kiti nilichukua kile kiti na kukipasulia mbali.

Vilevile, nakumbuka kuna kipindi fulani nikiwa darasa ka kwanza mimi na kaka yangu (aliyekuwa darasa la 4) tulikacha masomo. Ikawa kila asubuhi hata kabla wazazi hawajaamka tukawa tunaamka na kutokomea porini kutega na kuwinda ndege. Kuna wakati tulikuwa tukinyimwa chakula lakini kwa kuwa porini kuna vyakula vya kumwaga, haikuwa shida sana.

Siku za mwizi ni 40. Siku moja baba alitufumania asubuhi na mapema kabla hatujazama porini na kutuswaga kama mbuzi hadi shuleni. Tulipofikishwa shuleni walimu wakaombwa watucharaze barabara lakini bahati nzuri tukawa hatuna uniform za shule. Mimi nilikuwa nimevaa shuka na kaka kavaa nguo za kawaida (sio sare) zilizokuwa zimechakaa sana.

Badala ya kuchapwa, walimu walimlaumu baba kwa kutonunulia sare za shule. Sikumbuki alikubalianaje na wale walimu lakini tuliruhusiwa kuingia darasani huku mimi nikiwa nimevaa shuka. Wanafunzi wote darasani, macho yao kwangu. Siku hiyo nilijiona tofauti sana mle darasani sema walimu wa zamani hawakuwa wanoko kama wa sasa hivi. Lazima wangenichomoa darasani.

Je, ni vitimbi gani ulivyofanya utotoni ambavyo ukivikumbuka leo hii unajishangaa sana?

Kwangu viko viwili cha kwanza wakati wa enzi ya utoto wangu nilikuwa na tabia ya kupinga hasa kupigana mateke ya makalioni ( wale Vijana wa zamani mnaijua hii ilikuwa tunaiita bong'oa ) ambapo ulikuwa ukijisahau labda unaokota kitu au umeinama basi yule uliyepinga nae anakuja kwa nyuma kisirisiri na kukupiga bonge la teke la makalioni.

Sasa kuna siku moja bila kujua au sijui siku hiyo nilidata kuna Mtu mmoja nikiwa darasa la 5 yeye akiwa darasa la 7 nilipinga nae bong'oa sasa kuna siku tuko Shuleni mida ya mapumziko saa nne nikamwona Mtu mmoja anafanana na yule niliyepinga nae kainama hivyo nikajiseti mwenyewe na kwenda kumpiga teke la bong'oa kumbe bahati mbaya hakuwa yule niliyepinga nae na alikuwa ni Head Prefect na bahati mbaya hata lile teke nililompiga nalo liligusa hadi makende yake ( m.a.p.u.m.b.u ) na aliumia mno na siyo siri nilijisikia vibaya sana na siku hiyo hiyo nilichana na huo mchezo.

Kituko cha pili nakumbuka tokea utoto wangu na hii tabia nimeenda nayo hadi Chuo Kikuu Mimi huwa ni mtoro mtoro hasa darasani na mvivu pia hivyo kuna siku moja nimeenda Shule halafu siku hiyo kukawa na ukaguzi wa Mifyagio wakati wa mistari ambapo niliamua kukimbia maporini kujificha ambapo nakumbuka nilikaa huko hadi mida ya Saa 4 wakati wa break.

Kumbe wakati Mimi nimeenda kujificha huku nyuma wenzangu walifanya test ambapo ambaye hakufanya ilikuwa siku ya pili aje kupigwa bakora za kutosha tu na pia Mzazi wake kuitwa. Ndipo nikaona kuwa sasa ule muda wa kupigwa hadi kuflet na Baba Mzazi wa GENTAMYCINE umefika pamoja na yule Mwalimu mnoko hivyo nilichokifanya hadi leo huwa najiuliza ujanja ule nani alinifundisha.

Nilichokifanya mara baada tu ya kuambiwa kuwa wenzangu walifanya test na bahati nzuri maswali yalikuwa bado yapo Ubaoni nilichokifanya ni kuchukua Karatasi na kuandika yale maswali na kuyajibu haraka haraka kisha nilipomaliza tu nikatoka na ile Karatasi na kwenda moja kwa moja staff room kuchungulia kama yule Mwalimu yupo na nilipomchungulia kwa mbali na kukuta yupo nikaziona zile Karatasi za wenzangu zikiwa bado hazijasahihisha kwani nilimsikia anaulizia kwa Walimu wenzie nani ana Kalamu nyekundu amuazime.

Baada ya kuligundua hilo nilichokifanya ni kujipa Ujasiri ambapo niliingia mule ndani ( staff room ) huku ile Karatasi yangu nimeificha mfukoni ambapo nilimfuata moja kwa moja yule Mwalimu na kumwambia kuwa kuna Mgeni wake yupo getini anamuulizia ndipo yule Mwalimu alipoamka haraka kumfuata. Wakati anaenda kule haraka huku akiniacha Mimi pale mezani kwake na zile Karatasi zake za Test nikaona kuwa nikiichomoa Karatasi yangu iliyokuwepo mfukoni wale Walimu wengine wangenishtukia hivyo nilichokifanya ni kuzipeperusha kwa kuzipulizia kwa mdomo zile za juu juu ambapo baadhi zilipeperuka hivyo nikajifanya naziokota ili nimpangie vizuri Mwalimu ndipo wakati nainama kuziokota nami kiujanja sana nikaichomoa yangu mfukoni na kuiunganisha na zile nilizoziokota na kuziweka pale mezani na kuondoka.

Wakati naondoka zangu njiani nikakutana na yule Mwalimu ambapo aliniuliza kuwa mbona ameenda na hajamwona Mtu nami nikamjibu kuwa yawezekana ameshaondoka kwani alimuulizia kwa muda mrefu ndipo na yeye Mwalimu akanijibu kuwa kama yule Mtu akija tena baadae nikamuite mule Ofisini.

Kesho yake wakati anarudisha zile Karatasi darasana na Mimi yangu ilikuwepo na niliifaulu vizuri tu ( japo kwa msaada wa Chabo ) na biashara ikaishia hapo. Na uwoga wangu haukuwa hasa kwa yule Mwalimu bali nilikuwa naogopa mno Baba yangu Mzazi angefikishiwa taarifa kuwa Mimi ni Mtoro na sikufanya test nadhani kwa jinsi ninavyomjua huyu Mzee pengine hata Mimi angenipoteza kama alivyopotea sasa Ben Saanane.

Ni hayo tu Wadau nilipenda nishee nanyi enzi zangu za utotoni.
 
Kitimbi kikubwa zaidi ambacho siwezi kusahau ni pale ambapo nilimwandikia mwalimu kimemo kuwa I love you na kuweka katikati ya daftari wakati tumekusanya akasahishe.Nakumbuka ilikuwa s/m hivi,basi Mwl yule alinikabidhi kwa Mshikaji wake ambaye naye Mwl.Nilichezea kichapo cha mbwa mwizi ukichanganyia nilikuwa natokea mtaa wenye vimbwanga.Siwezi kusahau kitimbi hiki,lakini cha kushangaza Walimu wengi walinitetea kwamba ni utoto tu.
 
Back
Top Bottom