tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,837
- 29,347
Katika maisha mwanadamu hupitia vipindi mbalimbali vya ukuaji...infancy, childhood, adolescence, adulthood, old age & death.
Sasa katika vipindi hivi vya ukuaji kuna wakati, hasa katika vipindi vya utotoni, mtu hujikuta unafanya vitimbi ambavyo kamwe huwezi kuvifanya ukubwani.
Nakumbuka utotoni nimefanya vituko kadhaa ambavyo nikivikumbuka leo hii najishangaa sana. Wakati ule wa utoto nikirudi mchana kutoka shule nisikute chakula nilikuwa nakasirika sana hadi ikitokea nikajikwaa kwenye kiti nilichukua kile kiti na kukipasulia mbali.
Vilevile, nakumbuka kuna kipindi fulani nikiwa darasa ka kwanza mimi na kaka yangu (aliyekuwa darasa la 4) tulikacha masomo. Ikawa kila asubuhi hata kabla wazazi hawajaamka tukawa tunaamka na kutokomea porini kutega na kuwinda ndege. Kuna wakati tulikuwa tukinyimwa chakula lakini kwa kuwa porini kuna vyakula vya kumwaga, haikuwa shida sana.
Siku za mwizi ni 40. Siku moja baba alitufumania asubuhi na mapema kabla hatujazama porini na kutuswaga kama mbuzi hadi shuleni. Tulipofikishwa shuleni walimu wakaombwa watucharaze barabara lakini bahati nzuri tukawa hatuna uniform za shule. Mimi nilikuwa nimevaa shuka na kaka kavaa nguo za kawaida (sio sare) zilizokuwa zimechakaa sana.
Badala ya kuchapwa, walimu walimlaumu baba kwa kutotununulia sare za shule. Sikumbuki alikubalianaje na wale walimu lakini tuliruhusiwa kuingia darasani huku mimi nikiwa nimevaa shuka. Wanafunzi wote darasani, macho yao kwangu. Siku hiyo nilijiona tofauti sana mle darasani sema walimu wa zamani hawakuwa wanoko kama wa sasa hivi. Lazima wangenichomoa darasani.
Je, ni vitimbi gani ulivyofanya utotoni ambavyo ukivikumbuka leo hii unajishangaa sana?