Vitambulisho vya Taifa: Maoni ya Mchungaji

Nimeandika issue na maoni kama haya kwenye thread ile ya kampuni ya malaysia. nadhani tatizo tulinolao serikali inaweza kufanya mambo mazuri tu lakini yasiyo na tija kama hawaangalii mambo kwa upana wake

Binafsi sioni mantiki ya kuwa na daftari/ kitambulisho cha mpiga kura inachotumika seasonal every five years. alafu tena uje uwe na kitambulisho ya taifa. Kwa nini wasiboreshe hiki kitambulisho cha mpiga kura kuwe ndo kitambulish cha taifa.

Kwa nini tuwe na maserver ma database mengi yenye taarifa zile zile ten chini ya serikali moja?



Ukichukua the thread yenyewe uchanganye na the above maelezo - yamejitosheleza kabisa.
 
Kwanza Kikwete sio Dr.
Pili Sio Rais wetu mpendwa kwa sana kam ni mpendwa ni kwako
Tatu Vitambulisho ni muhimu

Vitambulisho vya Taifa ni muhimu sana, vitatumika kila sehemu hata Bank, shule, kuombea kazi na shughuli nyingine. Swala la Vitambulisho naliunga mkono wa 1000000% kama hamtaki vitambulisho hameni nchi
mawazo mgando,hivi unajua maana ya database?
 
Naomba mfano Wa nchi iliyounganisha Hivi vyote ndio nitachangia hoja..,


Itakusaidia vipi kutoa mawazo yako ambayo yanatakiwa kuwa huru kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo vya nchi hii? Ama umegubikwa na ulimbukeni wa kufuata mzoga au huna upeo chanya wa kufanya hivyo.
 
Sioni tatizo nini ipo chini ya nani kinachotakiwa watafute njia ya kufanya vitu efficinetly.

Tutasikia na
trafiic police wanataka kuwa system ya kuwa na taarifa za magari. Je ni busara wawe na system yao wakati wanaweza kutumia System ya TRA.??Kitaalam trafic police watatakiwa kuwa na access ya kuview kwenye baadhi ya taarifa za regsitarion ya magari ya TRA. Kisiasa ndo jibu jepesi wataptisha na traffic police kuwa na syetm yao. Hili ni tatizo

The
government is one. it should not matter server au administration au data anazo nani kinachotakiwa ila taasisis inayohitaji data fulani ambazo zipo sehemu izipate badala kila taaisi kuanzisha kitu kile kile.

Wanaweza wakapewa watumishi may be wa NIDA au RITA kufanya data entry wengine wakawa na right ya kiview tu
Sasa kama hili wazo lako sio sahihi kwanini asitokee mtu akalipinga!!!? ...na kama ni sahihi ni kwa lisifikiriwe katika utekelezaji!? Je itakuwa sawa kukiri kuwa nchi sasa ina 'wafikiriaji (thinkers)' wasio na maamuzi au ina 'Waamuzi wasio fikiri'???
 
Naomba mfano Wa nchi iliyounganisha Hivi vyote ndio nitachangia hoja..,
haya mambo niyo maana yameletwa jamvini hapa kuangalia kama kweli na sisi kama Watanzania tuna la kuweza kufikifri wenyewe badala ya kuangalia yaliyofanyika kwingine. Angalia uhalisia wa mawazo!
 
wataalam wa mambo ya information systems huwa tunaita data redundancy: hii ni kweli kbs serikali ni moja iwepo database moja inayoshughulikia personal details za wananchi, madhara yake baadae kutatokea tatizo la kutoelewana btn database systems hizo za rita na nyingine mwishowe kufanya maamuzi yasiyo sahihi
Mfano wa malaysia wenyewe swala la vitambulisho vya uraia unapewa unapozaliwa (wao wanaita IC card) so unaweza ukagues umri wa mtu kwa kuangalia IC number na pia wana foreign IDs (zinaitwa ikad) na zipo chini ya immigration dept under ministry of home affairs.
naunga mkono hoja 100% ni kwanini iris wasifanye kama malaysia
ukiangalia pia kiasi cha fedha kinachokusudiwa kutumika na kutokana na uzoefu tulioupata, nadhani wengi tukisoma repoti ya bunge juu ya RICHMOND na jinsi wahusika walivyokuwa wakifuatilia usiku na mchana ungedhani kweli wana nia ya dhati kumaliza mgao wa umeme Tanzania, tuliona tulipoishia. Kuna haja ya kurejea huko!??
 
Kwanza Kikwete sio Dr.
Pili Sio Rais wetu mpendwa kwa sana kam ni mpendwa ni kwako
Tatu Vitambulisho ni muhimu

Vitambulisho vya Taifa ni muhimu sana, vitatumika kila sehemu hata Bank, shule, kuombea kazi na shughuli nyingine. Swala la Vitambulisho naliunga mkono wa 1000000% kama hamtaki vitambulisho hameni nchi

Weeee Mzalendo kweli? Mtoa hoja hajakataa vitambulisho ila jinsi ya kuvipata kwa kuwa kuna data base nyiingi na taasisi nyiingi ambazo hakuna hata moja inayofanya kazi zake kwa asilimia mia kila taasisi inagusagusa tu kwa hiyo akapendekeza iwe moja. Sasa wewe unataka watu wahame nchi unataka uishi peke yako?
 
[font=&quot]ndugu wanajamvi,
[/font]
[font=&quot]
[/font]
[font=&quot]kwa heshima kubwa napenda kuwasilisha hii hoja ili tuone inaweza kutusaidia vipi kupinga hii project ya vitambulisho vya taifa, msijali tuna nguvu kiasi gani maana saddam, mubarak, mobutu, n.k. Walionekana giants pia! Nadhani wanajamvi wengine wamesha post juu ya hili swala ila kutokana na umuhimu wake kwa taifa nakuja nalo tena.
[/font]
[font=&quot]
fikiria haya yafuatayo:
mpaka sasa kuna vitambulisho vifutavyo kutoka serikalini/taasisi za serikali:[/font]

  1. [font=&quot]tin certificate (inatolewa na tra)[/font][font=&quot][/font]
  2. [font=&quot]birth certificate (inatolewa na rita)[/font][font=&quot][/font]
  3. [font=&quot]passport (inatolewa na immigration/mambo ya ndani)[/font][font=&quot][/font]
  4. [font=&quot]voter registration card (inatolewa na tume ya uchaguzi)[/font][font=&quot][/font]
  5. [font=&quot]driving license (inatolewa na traffic police/mambo ya ndani)[/font][font=&quot][/font]
  6. [font=&quot]...nk[/font][font=&quot][/font]
  7. [font=&quot]...nk[/font][font=&quot][/font]
[font=&quot]mpaka sasa si tra au wizara ya mambo ya ndani ambayo database yake inahifadhi nusu ya watanzania, zote zina data kidogo sana na labda sizizo sahihi. Ukienda kuomba passport unatakiwa kutoa cheti cha kuzaliwa, tin unaombwa kitambulisho (sijui kipi!!) nk ila cha msingi hapa particulars la kila kitambulisho ni zile zile!

Kwa mfano, nimesoma habari inayohusu shirika la misaada la japan (jica) kutoa angalizo na maoni yake juu ya nini kinasababisha foleni jijini dar es salaam: Walioiona hiyo habari ni kuwa ziko taasisi karibia(zaidi) ya 15 zinazoshigulika na kitu kimoja - usafiri wa jiji!!! ...ambazo kutokana na maamuzi yao kutofautiana yameishia kuongeza ukubwa wa tatizo badala ya kupunguza. Wakashauri iwepo mamlaka moja tu yenye maamuzi.

kwa vile mradi huu wa vitambulisho unatiliwa mashaka na wengi, na kwa vile siku za nyuma mheshimiwa raisi wetu mpendwa sana dokta jakaya mrisho kikwete alishasema kuwa anajenga uwezo (capacity building) kwa kuelekeza nguvu kwenye kuimarisha taasisi, basi ni kwa nini hizo us $230m zinazotolewa kwa kazi hii zisiwekwe kwenye taasisi ambazo zipo tayari na zina mtandao mzuri badala ya kuanzisha mpya!!?

hii inaweza kulisaidia taifa kwenye mipango yake ya maendeleo na kuwa na 'a strong and reliable database' inayoweza kuondoa utata wa kuambiwa kuwa kuna wapiga kura milioni 22 lakini wakajitokeza milioni 7! Lakini kikubwa zaidi ni duplication of works and repetitions!

my take:
taasisi ya vizazi na vifo (registration, insolvency and trusteeship agency - rita) inaonekana ndiyo kiuhakika inahusika na kila mtanzania na ni ya kudumu (maana passport ni kwa wasafiri, leseni ni madereva, tin ni biashara, mpiga kura nk) ipewe hizo pesa ili waimarishe uwezo wao (database na administrative issues) badala ya kuzitupa "motoni"!?

(naomba kukosolewa)


nawasilisha[/font]

hapo umezungumzia vitu vingi sana,ungejaribu kuweka bayana nia yako.wizi wa kura basiiiiiiiiii.
 
Kweli kabisa, naunga mkono, hizo pesa wamepewa hao wanunue vifaa kisha wapeleke kwao. kwa Mtanzania mpaka leo hawazi kutengeza kitambulisho? kama vipi wamkodi mtaalamu, kama Zanzibar wameomba msaada Israel, na wametumia Technology ya Israel kutengeneza vitambulisho ya Mzanzibari, nashangaa sisi bara kukabidhiwa walima minazi wa Malaysia, au kiji rangi tu kinachomata?
 
Mzalendo unatakiwa uwe kidogo makini unapochangia mada. Hakuna mtu aliyekataa kuwa vitambulisho sio muhimu, ila mchakato wake uende vipi ilhali kuna taasisi zingine zinafanya kazi kama hio, na ziko well equiped with personal information, and overall security ya watu binafsi.

'Heri akunyimae pesa, kuliko Akili'
 
Angalia

Ukitaka cheti cha kuzaliwa mlolong unaopitia

  • upite kwa balozi sijui wakili au mahakami.. .....ok umepita mlolongo huo umepata cheti cha kuzaliwa

Siku ukitaka passport hata kama una cheti za kuzaliwa vile vile

  • Unatakiwa uende mahakamani au upite kwa wakili, baalozi. Hata kama una kitambulisho cha mpiga kura ni kazi bure

Sasa ngoja ngoja mje msikie utaratibu wa kupata kitambulisho cha taifa..hata kama una passport utaambiwa anzia kwa balozi. au nenda kwa wakili. Hii vitu kama viko disjointed havina maana. na watu wanaposema ukritimba ndo mambo ama haya Ma system kibao lakini mtu unazungushwa.

Yaani system za serikali zenyewe haziaminiani. Kuna haja gani ya kutumia gharama kubwa kuwa na haya mambo. kama hayarahisishi utendaji. Kitambulisho cha taifa ni kizuri ilaaaa...................

Mfano mwingine ndio maan Kutoa mizigo bandari ya Dar inachukua siku mbili zaidi ya kutoa mzigo huo huo Mombasa. Sijui TRA sijui TICS. Ndo mambo haya haya. Kila bosi anataka aweke singature
 
Kwanza Kikwete sio Dr.
Pili Sio Rais wetu mpendwa kwa sana kam ni mpendwa ni kwako
Tatu Vitambulisho ni muhimu

Vitambulisho vya Taifa ni muhimu sana, vitatumika kila sehemu hata Bank, shule, kuombea kazi na shughuli nyingine. Swala la Vitambulisho naliunga mkono wa 1000000% kama hamtaki vitambulisho hameni nchi

Hata kama humkubali Jk ila tambua kuwa he is entitled to be called Dr kwa kupewa Honorary DOctorate na vyuo mbalimbali.
Kama umebahatika kupitia chuo utakuwa wajua hili na nimeona nikuambie tu japo si sehemu ya mjadalia.
unaposema vitatumika hadi bank ina maana kadi za bank hazitatumika tena au? una uhakika na hili?
Nijuavyo mie ni kwamba vitambulisho vya taifa ni vya msingi sana na lazima viwe na ubora zaidi ya vitambulisho vya mpiga kura.
 
Great thinkers tumekuwa tukiambiwa kuwa tunapenda kulaumu kwa kiasi kikubwa pale tatizo linapotokea lakini kwa kiasi kidogo hutahadharisha pale tunapoona tatizo linaweza kutokea. Ingawaje ukisoma threads zote utaona maonyo mengi tu ambayo hutolewa kwenye jukwaa hili, ila kwa kuwa kazi yetu ni kusema, wahusika wanaona hatuwezi kuwafanya lolote.

Sasa mimi kama mmoja wa great thinkers ninaanza kutoa tahadhari mapema kabisa.

Tanzania yetu kwa sasa ina utata hasa katika muundo wa serikali yake ya Muungano. Wenzetu wa Zanzibar wameweka bayana kupitia njia mbalimbali kuwa hawakubaliani na muundo wa muungano ulivyo. Wanapendekeza Kuwa iwepo serikali ya Zanziba , ya Tanganyika na ya Muungano. Kwa hali hii wanataka Zanzibar itambulike kama nchi inayojitegemea yaani Taifa huru.

Wakati huohuo nchi iko fasta inataka kutengeneza vitambulisho vya utaifa kwa billioni nyingi zaidi ya 220. Je vitambulisho hivyo ni vya watu wa namna gani? Watanzania wa Zanzibar wanaodai kuwa na nchi huru si watataka kuwa na vya kwao. Je kwenye bajeti ya sasa ya hivyo vitambulisho si na wao wapo? Je muundo wa vitambulisho umekaaje na vinawatambulishaje watu wa bara na wa Visiwani.

Wasiwasi wangu ni kwamba tutaingia hasara kutengeneza vitambulisho vingi ambavyo bila kufikia muafaka utambulisho tutakao kuwa nao utakuwa umebadilika na kuifanya serikali itengeneze vipya. Hivyo Muafaka juu ya suala la muungano ufikiwe mapema kama vitengenezwe vya Tanganyika tuu, ili wenzetu nao watengeneze vya Taifa la Zanzibar. La sivyo utakuwa mwanya wa mafisadi kuchanganya hesabu kwa kusema kuwa vitambulisho vimekosewa. Waulizeni wanaoulalamikia muungano wanataka vitambulisho viwatambue kwa utaifa upi? Watanzania, Wazanzibari au Watanganyika?

Kwa mwenye fikra za karibu ataona hii haina tatizo ila Watanzania wenzangu fuatilieni ili muone watu wanalichukuliaje. Tahadhari tumetoa mapema. Tatizo litakalotokea sababu ya uzembe wa haya tutaendelea kukosoa na kulaumu maana tumeeleza mapema.

Mungu ibariki Tanzania
 
Watu wameshapiga hesabu zao. Vitengenezwe alafu ionekane havikidhi wananchi wote wa Muungano , mfarakano utokeee, watu wale tender mara mbilimbili. Hatukubali.
 
Back
Top Bottom