Vitabu vitano vya kukuza ujuzi wa fashion

Mema Tanzania

Member
Feb 23, 2020
66
65
Moja ya tasnia kubwa duniani ni fashion, kazi ambayo inaweza kuwa career ya kijana kama akiwa na interest nayo. Kwa mujibu wa www.indeed.com fashion designer duniani wanaingiza wastani wa $6,000 (takribani milioni 14) kwa mwezi. Ukifanya tathmini kwa mazingira ya Tanzania, tasnia ya fashion ni kazi yenye kueleweka kwa vijana wengi? Hapana!

Basi, Jennifer Beile ni moja ya waandishi wa blog maarufu duniani zinazohusu fashion na mitindo ya maisha. Mwaka 2016 katika mtandao wa Crossroads aliorodhesha vitabu vitano kwa ambaye anataka kajiajiri na kukuza ujuzi na uelewa juu ya tasnia nzima ya #Fashion. Tumeona isiwe issue, katika Readers Club yetu ya leo, tumekusogezea upate kuvifahamu;

1. Women in Clothes ~ Sheila Heti
Muandishi alifanya tafiti kwa watu wanaofanya fashion zaidi ya 600 kujua mitazamo yao juu ya hii tasnia na namna gani inavyogusa maisha yetu.

Readers CL1.png


2. In Your Face ~ Mario Testino
Kitabu kilichobeba mkusanyiko wa picha tofauti zenye kuonyesha matukio yenye kuvutia kuhusu mitindo. Unapofika kurasa ya mwisho, hutosita kurudi tena kurasa ya kwanza.

Readers CL2.png


3. The Sartorialist: Closer ~ Scott Schuman
Unapenda mitindo kutoka kwa wabunifu wa mtaani? Hiki kitabu ndio mahali pake.

Readers CL3.png


4. I'll drink to that ~ Betty Halbreich
Betty ni nguli katika mitindo mwenye uzoefu zaidi ya miaka 40. Kitabu hiki ameelezea namna mwanamke aliye katika tasnia ya mitindo anaweza kutumia fashion design kuonyesha nguvu ya mwanamke katika jamii.

Readers CL4.png


5. Champagne Supernovas ~ Kate Moss
Karne ya 20 inatajwa kuwa karne bora katika mitindo, muziki na mapinduzi ya teknolojia ya kisasa. Hakika Kate Moss ameandika moja ya vitabu bora vyenye kuangazia utamaduni wa mitindo.

Readers CL5.png



Unaweza kutufuata kupitia Facebook, Instagram, Twitter na Medium kama Mema Tanzania
 
Back
Top Bottom