Vita ya urais CHADEMA: Dr. Slaa, Zitto na Mbowe hapatoshi!

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
1,225
Na Mwandishi wetuWakati hali ikionekana kuelekea kuimarika na kuwa tulivu ndani ya CCM, Mambo yanazidi kuwa magumu kwa safu ya uongozi wa CHADEMA kwenye mbio za Urais ujao mwaka 2015.

Imezoeleka kuwa kila unapokaribia uchaguzi mkuu wa kitaifa CCM huwa inaongoza kuwa na makundi yanayosapotiana na kusigana vikali ili kupata yule atayekiwakilisha chama kwenye kinyang'anyiro cha Urais.

Lakini kwa sasa hali hiii inaonekana kuwa kali zaidi ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA baada ya makundi makuu matatu yanayoonekana kupeana vijembe vya hapa na pale.

Awali tetesi za uwepo wa makundi ndani ya chama hiki ilikuwa ni kama maneno tu, Lakini kadri siku zinavyokwenda haliinaonekana kuwa ni kweli ndani ya chama kuna makundi.
makundi hayo yapo makuu matatu.

KUNDI LA KWANZA NI LILE LA MWENYEKITI WA CHADEMA MH. FREEMAN MBOWE akisaidiwa na Muasisi wa chama na baraza la wazee linaloongozwa na Mzee Edwin mtei na watu wanaotoka kilimanjaro wamepanga kumsimamisha Freeman Mbowe kwenye uchaguzi ujao.

Inaelezwa kuwa watu wa kilimanjaro hasa wale wa kabila la WACHAGGA ambao inasemekana ndio wenye nguvu ndani ya chama hicho wanataka kumuingiza mbowe kwenye Urais ili waweze KURUDISHA FEDHA ZAO WALIZOPOTEZA KUKIUNGA MKONO CHAMA HICHO NA KUJITAJIRISHA KWA UWEPO WAKE MADARAKANI.

Lakini wananchi kwanyakati tofauti kupitia gazeti hili wamekuwa wakisema hawapo tayari kuwapa nchi watu wa kaskazini kutokana na rekodi yao mbaya ndani ya taifa hili, wengi wao walipopewa nafasi waliishia kujitajirisha na kufanya ufisadi mkubwa uliolipelekea taifa hili kuwa maskini hadi leo.

Pia Mbowe anapata wakati mgumu zaidi kwasababu alishapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama na akaishia patupu.

Wakati hayo yakiendelea John Mnyika anaonekana akimuunga mkono sana Mbowe kwenye kuhakikisha anapita kugombea Urais.

Mnyika analifanya hili kwasababu taarifa za chini zimevuja kuwa Mnyika ameahidiwa Uenyekiti wa chama mara baada ya Mbowe kumaliza muda wake.

Mnyika amekuwa akiwashawishi vijana kumtenga Zitto kabwe ndani ya chama, pia Mnyika amejitokeza na kusema ana picha za Zitto Kabwe akiwa kwenye vikao vya siri na watu wa CCM. Picha hizo amezihifadhi kwenye laptop yake.

KUNDI LA PILI NI LA DR, SLAA ambaye licha ya kutokea kaskazini amekuwa haungwi mkono kabisa ndani ya chama na hata kwa wakaskazini wenzake.

Licha ya mchango wa slaa kuwa mkubwa kutokana na kushika nafasi ya pili kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika mwaka 2010, Slaa anaonekana kuwa si chochote ndani ya chama na anaungwa mkono na kanisa la katoliki ambalo amewahi kulitumikia akiwa kama padri kabla hajaasi.

DR. SLAA ndani ya chadema amekubwa na msukosuko na ameporomoka kisiasa kutokana na kashfa ya mke wa mtu na ndoa yake.

Lakini kubwa zaidi Dr,slaa anakabiliwa na DENI KUBWA NDANI YA CHADEMA LA MILLIONI 180 ANAZODAIWA NA CHAMA HICHO na mbowe ameshatoa AMRI KWA SLAA ahakikishe anazirejesha fedha hizo haraka ilizitumike kwenye M4C mwakani.

DR. SLAA anadaiwa kujikopesha fedha hizo bila kufuata utaratibu ambapo inadaiwa alitumia nafasi yake ndani ya chamaMillioni 80 alijikopesha ili kulipa deni lake la nyumba nje kidogo na jiji la Dar es salaam (Bunju). Millioni 20 Dr.slaa alizichukua na kumpatia JOSEPHINE MSHUMBUSI ambaye naye alizibadilisha kwenda fedha za kigeni(dola) na kuziingiza kwenye akaunti yake.

Million 40 ambazo zilichangwa na wabunge wa chama hizo, Dr. Slaa alizitumia kwa matumizi yake binafsi na kupeleka wabunge kugoma kukichangia chama hadi hapo atakaporudisha fedha hizo.

Jukumu la kuhakikisha fedha haziibiwi kiholela kama alivyofanya Dr.slaa jukumu hilo amepewa Godbless Lema aliyekuwa mbunge wa arusha.

KUNDI LA TATU NI LA ZITTO KABWE ambaye amekuwa akinyoshewa kidole kwa kuwa karibu na viongozi wa CCM, Zitto kabwe ndani ya chadema licha ya kutengenezewa mitego na vitisho kama vya Mnyika kusema anapicha zake akiwa na watu wa CCM. Zitto ameendela KUNG'ARA ndani na nje ya chama kutokana na kuibua hojazito zenye manufaa kwa TAIFA.

Zitto kabwe anaungwa mkono nje na ndani ya chama na kundi kubwa la vijana jambolinaloonekana wazi kuwachanganya viongozi wa chadema ambao wanataka Mbowe awemgombea Urais lichaya kupewa nafasi hiyo na kushindwa.

Mpango wa kummaliza zitto unaonekana kuwa mgumu kutokana na ule wa awali wa maadui zake wengi wa kisiasa ndani na nje ya chadema kushindwa. Mpango huo wa kumaliza zitto ulikuwa kwenye kamati ya Ngwilizi ambapo Zitto alituhumiwa kushiriki kwenye Rushwa Lakini mwisho wa siku Zitto alishinda na kusafishwa kwamba hana hatia. Wabaya wake wa kisiasa Mbowe akitajwa alitaka kutumia mwanya wa kamati hiyo ya gwilizi kummaliza Zitto lakini alishindwa.

Habari kutoka Mbeya na kanda ya ziwa yote zinasema kuwa wanachadema hawapo tayari kuona Zitto anafanyiwa mchezo mchafu ndani ya CHADEMA kama wanavyoona maadui zake wakihaha kummaliza na kuishia patupu.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema mgogoro huu unaondela ndani ya chama kueleka 2015 kama wazee wataendelea kuingilia mambo ya chama hautakiacha chama salama.
Nawasilisha.

Chanzo cha Habari hii - Gazeti la AFRIKA LEO
TAR.21/11/2012
FRONT PAGE YA GAZETI HIYO HAPO JUUU
ASANTE
 

Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,427
2,000
Walishapotea kwenye ramani ya kisiasa kitambo baada ya kuishiwa hoja, maana kila hoja waliyokuwa wanaipigia kelele haifanikiwi, mfano mafisadi na mpaka leo hakuna aliyefungwa. Kwa ufupi Chadema inasubiri kizikwa rasmi 2015.
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,560
1,195
Walishapotea kwenye ramani ya kisiasa kitambo baada ya kuishiwa hoja, maana kila hoja waliyokuwa wanaipigia kelele haifanikiwi, mfano mafisadi na mpaka leo hakuna aliyefungwa. Kwa ufupi Chadema inasubiri kizikwa rasmi 2015.
Sasa anayetakiwa Kuzikwa ni yule Mwenye Dola anayeshindwa Kuwakamata na Kuwafunga Mafisadi au ni yule anayefichua Mafisadi? Hivi hiyo hoja yako inaizika CCM au CDM
 

Communist

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
5,391
1,225
Tunte hapa sioni kitu chochote, ni mambo ya hovyohovyo tu. Ulishasikia Dr. au Mbowe wametangaza kugombea. Haya ni mambo uchwara. Hovyo kabisa, na ilo gazeti ni hovyo kabisa kama uhuru na mfisadi.
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,855
2,000
Walishapotea kwenye ramani ya kisiasa kitambo baada ya kuishiwa hoja, maana kila hoja waliyokuwa wanaipigia kelele haifanikiwi, mfano mafisadi na mpaka leo hakuna aliyefungwa. Kwa ufupi Chadema inasubiri kizikwa rasmi 2015.
Wewe ndo Kengo kabisa, Hii nchi iko hapa kwa sababu ya Ufisadi, hata kama wewe ni mnufaila wa Huo ufisadi lakini ninaamni wapo Ndugu zako huko Vijijini wanafanya kunyang'anyana na Ng'ombe Maji
 

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
2,881
2,000
Walishapotea kwenye ramani ya kisiasa kitambo baada ya kuishiwa hoja, maana kila hoja waliyokuwa wanaipigia kelele haifanikiwi, mfano mafisadi na mpaka leo hakuna aliyefungwa. Kwa ufupi Chadema inasubiri kizikwa rasmi 2015.
subiri uone! utazika ndugu zako wote na ccm yako CDM itapeta na kuongeza wabune mara tano ya waliopo sasa.
 

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,244
1,500
Sasa anayetakiwa Kuzikwa ni yule Mwenye Dola anayeshindwa Kuwakamata na Kuwafunga Mafisadi au ni yule anayefichua Mafisadi? Hivi hiyo hoja yako inaizika CCM au CDM
HOJA IYO INAIZIKA CCM CHAMA CHA MAFISADI NA WALA RUSHWA, RUSHWA IMEWAJAA MPAKA KTK KOFIA ZAO ZA CCM, NA ZAID MNATUCHANGANYA IVI HAMUONI ZITO KIPENGELE CHA UMRI KINAMBANA, MAGAMBA BWANA WANAANGAIKA MASKINI LKN WAPI? LEO WALKUWA MTWARA WAMESHINDWA KUWAVUTA WATU WAKAFANYA ATI VKAO VYA NDANI, DANGANYA TOTO IYO WATU WAMEWASUSA, LABDA MUNGEWAONGA ELF5 ILI WAJe KUJAZA MIKTANO YAO
 

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,213
0
Walishapotea kwenye ramani ya kisiasa kitambo baada ya kuishiwa hoja, maana kila hoja waliyokuwa wanaipigia kelele haifanikiwi, mfano mafisadi na mpaka leo hakuna aliyefungwa. Kwa ufupi Chadema inasubiri kizikwa rasmi 2015.
ccm inasubiri nguvu za kofia na kanga 2015,hata kama mtatumia magazeti ya mafisadi ccm haitaachwa salama 2015, tunataka mabadiliko!
 
Top Bottom