Vita ya Uchumi haijawahi kuwa nyepesi, Hayati Magufuli aheshimiwe

umewahi jiuliza kwanini africa ni maskini ?
Sababu ni nyingi na moja ya muendelezo ni huu hapa ushahidi
Tuna Mbuga kibao nchini lakini wakatafuta mbinu za kuiba na wakafanikiwa
Nimeshangaa wengi humu wanajibu mada kwa mihemko na chuki za kiitikadi wala hawajachukua muda kumsikiliza Nyerere kwenye hiyo voice note!
Mkuu kuna watu huwa wanasoma heading na kujibu kwa mihemko kama iwe siasa, mpira na hata masuala ya uchumi wa nchi na mambo mazito kama haya
Sintashangaa kama utashambuliwa bila hoja
Nimemsikiliza Mwalimu na ameongea maneno mazito mno

Kuwa kuna maraisi waliwekwa na wazungu kwa maslahi yao na kuwatahadharisha watanzania
 
sababu wanazotoa sasa;
utasikia CORONA ndio chanzo cha haya yote, Vita ya Russina vs Ukraine ndiyo sababishi ya haya, Mvua imekuwa nyingi sukari ikaadimika, na umeme tunashindwa kuzalisha nduzo zinadondoka na nyaya kukatika, Mara ooh sisi sio kisiwa Nchi zilizoendelea wanafanya haya...ghafla oooh huwezi kuiga nchi zilizoendelea maana wale wapo mbele sana kimaendeleo na kiteknolojia.. Yaani nchi yetu hata Mungu atusamehe vipi bado uongozi tunaouweka ni TATIZO la kila jambo yaani
 
Ni sahihi kabisa hata hivyo JPM alionyesha nia na alikua anachukua hatua kupunguza hizo harakati nchini kwetu,

Na pengine kutamka waziwazi na hadharani kwa uzalendo mkubwa ni moja ya mbinu ya kimkakati (nawaza tu).
Magulifu just hakuwa na upeo wa ku-deal na issues kubwa kubwa, huu ni ukweli mchungu. Kujua matatizo na kuyashughulikia ni vitu viliwi tofauti.
 
Sababu ni nyingi na moja ya muendelezo ni huu hapa ushahidi
Tuna Mbuga kibao nchini lakini wakatafuta mbinu za kuiba na wakafanikiwa

Mkuu kuna watu huwa wanasoma heading na kujibu kwa mihemko kama iwe siasa, mpira na hata masuala ya uchumi wa nchi na mambo mazito kama haya
Sintashangaa kama utashambuliwa bila hoja
Nimemsikiliza Mwalimu na ameongea maneno mazito mno

Kuwa kuna maraisi waliwekwa na wazungu kwa maslahi yao na kuwatahadharisha watanzania
content kubwa ila watu hawamsikiliza kabisa mwalimu hapo na ndivyo bongo land tulivyo
 
kwa kufuta kifungu kinachotaka mashauri yote kusikilizwa mahakama za ndani.
Acha uongo hicho kifungu kilifutwa na JPM mwenyewe tena miezi mitatu tu baada ya sheria mpya kupitishwa na bunge maana hairuhusiwi nchi ya mwekezaji au nchi ya uwekezaji unpofanyika ndio usikilize kesi itakua biased ndio maana mnachangua nchi neutral ambayo haitokua na upande.
Baada ya awamu hii kuisha na aliyepo kuondoka na mambo yake tutabakia sisi kulipa hasara za ujinga waliofanya waliopo sasa.
Hatulipishwi sababu ya mikataba mibovu ila tunalipishwa sababu ya namna tunavyovunja mikataba ona hata Yanga na simba Mara ngapi wanapigwa fine na FIFA?

Mfano Makinikia yenye copper concerntrates kusafirishwa nje bila kuwa declared ilikua part ya mkataba? La hasha.... ila ni uzembe tu wa wakaguzi kugundua uwepo wa dhahabu nyingi kwenye mchanga. Sasa lile ni kosa la kiutendaji ilipaswa tufungue kesi ICSID na tulipwe fidia. Badala yake tukaenda kupora makontena tukakosa vyote.

Issue yetu sio mikataba ni kufuata sheria
 
Acha uongo hicho kifungu kilifutwa na JPM mwenyewe tena miezi mitatu tu baada ya sheria mpya kupitishwa na bunge maana hairuhusiwi nchi ya mwekezaji au nchi ya uwekezaji unpofanyika ndio usikilize kesi itakua biased ndio maana mnachangua nchi neutral ambayo haitokua na upande.

Hatulipishwi sababu ya mikataba mibovu ila tunalipishwa sababu ya namna tunavyovunja mikataba ona hata Yanga na simba Mara ngapi wanapigwa fine na FIFA?

Mfano Makinikia yenye copper concerntrates kusafirishwa nje bila kuwa declared ilikua part ya mkataba? La hasha.... ila ni uzembe tu wa wakaguzi kugundua uwepo wa dhahabu nyingi kwenye mchanga. Sasa lile ni kosa la kiutendaji ilipaswa tufungue kesi ICSID na tulipwe fidia. Badala yake tukaenda kupora makontena tukakosa vyote.

Issue yetu sio mikataba ni kufuata sheria
Mpuuzi wewe sheria itungwe wakati wa JPM halafu aifute mwenyewe??

Tatizo lako ni kujifanya kujua kila kitu.
 
Hiyo dhana ya ''vita ya uchumi'' ni moja ya vitu ambavyo Magufuli alifanikiwa kuwaaminisha wafuasi wake na mpaka kesho bado wataendelea kumsujudia. Ni kama vijijini, watu maskini wanavyoaminishwa na waganga au wenyewe kwa wenyewe kuwa umaskini wao unatokana na husda, vijicho na ulozi wanavyofanyiwa na maadui zao. Unakuta mtu ana nyumba ya nyasi na watoto 15, fedha yake yote inaishia kwa waganga kwa kuamini kuwa magonjwa, umaskini na kila aina ya masahibu yake yanatokana na kijicho cha maadui.
Wew mjinga kuaminisha nini pimbi kbs
 
Nimeshangaa wengi humu wanajibu mada kwa mihemko na chuki za kiitikadi wala hawajachukua muda kumsikiliza Nyerere kwenye hiyo
Mkuu tusaidie wewe kutaja watu ambao ni vibaraka wa beberu kwa Sasa HIVI....

Kuna watu ni viongozi wa juu wengine wanaushawishi mkubwa kwenye vyama vya kisiasa, lakini shida inakuja tayari ni wakara wa CI🦅.
Magulifu just hakuwa na upeo wa ku-deal na issues kubwa kubwa, huu ni ukweli mchungu. Kujua matatizo na kuyashughulikia ni vitu viliwi tofauti.
Umoja na mshikamano ni changamoto kwa tz hii, issues kubwa kama hizi zinahitaji ushilikiano wa kidiplomasia lakini katika hali ya kushangaza awamu ya tano JPM alipoteza mahusiano mazuri na wanadiplomasia wazoefu na nguli wa ndani ya nchi karibia wote.

Ndio maana vita ilikua ngumu zaidi kwani at the same time alikua anapambana na maadui wandani na wa-nje ya nchi,

Sasa swali ni kwanini alipishana nao!

Kulikua na ulazima gani wa yeye kutofautiana na we zake?

Kama raisi ni Taasisi kwanini hawaku-solve hii issue kwa maslahi ya taifa?.

je? alijua kua hawa ndio obstacles na nivibaraka wa mabeberu akaona aachane nao katika harakati za kizalendo au yeye ndio alikua pandikizi la mabeberu kuja kuharibu mikakati yetu ambayo aliipinga vikali ie. Bagamoyo PORT, LNG. Hapa Sasa ndio penye hoja ambayo Mwl Nyerere alituasa.

Nb: Mawazo yangu tu haya wadau... vip maoni yenu wakuu?
 
Habari JF, vita ya Uchumi kuanzia mitaani, mirathi na makazini hata iwe ndogo haijawahi kuwa nyepesi na haijawahi acha mtu salama.

Ukiwa kiongozi wa juu nchi za Africa huwa hakuna vita nyepesi ya uchumi sababu unakuwa unapigana watu wa ndani ya nchi lakini pia na mataifa ya nje.

Magufuli pamoja na mapungufu yake yote alieonyesha jitihada katika kupambana hii vita ndani ya nchi lakini pia nje ya kwa kupitia mikataba mibovu mbali mbali na kuivunja ingawa wimbi la kesi za kushindwa kimataifa limeongezeka. Kwanini hizi kesi ni kipindi hiki? Kuna watu wana nufaika na hizi kesi?

Ukimsikiliza hapa mwalimu Nyerere kuna kitu unaweza elewa.

View attachment 2900394

Lakini JPM mwenyewe mara kadhaa kaongea kwa uchungu sana.
View attachment 2900408

Kwa kifupi kabla hatujalaumu kwa yote tuliyopitia Awamu ya Tano au Tunayopitia awamu Hii cha kwanza jiulize unaweza vaa hivyo viatu na ukapigana na Mafisadi na Mabeberu?

Binafsi huwa namlaumu Magufuli kwa kitu kimoja tu, kutotuletea Katiba Mpya.

Tumuache mzee wetu apumzike kwa Amani.​
RIEP mwamba
 
Hiyo dhana ya ''vita ya uchumi'' ni moja ya vitu ambavyo Magufuli alifanikiwa kuwaaminisha wafuasi wake na mpaka kesho bado wataendelea kumsujudia. Ni kama vijijini, watu maskini wanavyoaminishwa na waganga au wenyewe kwa wenyewe kuwa umaskini wao unatokana na husda, vijicho na ulozi wanavyofanyiwa na maadui zao. Unakuta mtu ana nyumba ya nyasi na watoto 15, fedha yake yote inaishia kwa waganga kwa kuamini kuwa magonjwa, umaskini na kila aina ya masahibu yake yanatokana na kijicho cha maadui.
Yaan hua najiuliza watu wa namna hii, hata kama ni umasikin ndio ushindwe kutambua how African nations are made under developed? Ufusadi mkubwa ni ule wa maliasili. Kusaini mkataba unaompendelea beberu, nchi inakosa wewe binafsi unapewa kidogo unazani maraisi wote wa Afrika wanapenda? Kikwete alipenda Ile namna ya uongozi wake wa Kila mtu holela?

Kuna kua na nguvu kubwa inayokusukuma ukubali hayo. Kukukataa unakua sio mmoja wao. Watakufanyia figisu Hadi uchoke.

Tambua ndani ya nchi sio Kila mtu anakua na mawazo kama ya kwako. Hata katika chama sio wote wanakukua na mawazo ya kutimiza Irani ya vyama vyao. Wengine wapo Kwa masrahi yao.

Wewe kama mwenyekiti wa chama kupambana nao ndani ya chama ni kama Magufuri na kina Nape na January na wengine. Watu waliomlengwa tofauti na wewe ni rahisi kuhongeka na kukufanyizia lollote like Ili masrahi ya mabeberu yatawale. Wewe usipochukua wenzio watachukua.Ukikataa wanaremove obstacle.

Elewa kwamba masrahi ya mabeberu ndio chanzo Cha matatizo na ufusadi uliokithiri. Ukiwa mzalendo wanakupa jina la obstacle, then grant ya kukuremove Kwa support ya watu wako wa ndani na sio wao.

Mafisadi wa ndani ya nchi bila support ya mabeberu kumuweza rais aliekua amejidhatiti Kwa ulinzi kama JOM sio rahisi kihivyo ufikiriavyo.

R.I.P Jembe Magu...
 
Vita gani na mabeberu? Ufisadi unatumaliza kila siku alafu tunasingizia wazungu. Mfano kwa mwaka tu unakuta 30% ya makusanyo yanatapanywa je hapo vita ya kiuchumi inaingiaje. Huu ni msemo ulitungwa na CCM ili kutafuta mtu wa kumtupia lawama kwa failures zao. No wonder hata awamu ya 5 ilidai wapinzani walituchelewesha sana ilihali hawajawahi kusanya kodi au kupanga bajeti tokea uhuru!!

Ni hivi mikataba inafuata sheria sio hisia au mihemko. Mfano tulidai Acacia wanatorosha makinikia. Ilipaswa twende ICSID tufungue kesi ya madai alafu tuweke ushahidi wa vifungu vilivyokiukwa mbona tungelipwa matrillion yote yale. Sasa cha ajabu tukaenda zuia makontena mara kamata kamata ya viongozi wa Acacia n.k. Kwa style ile wakifungua kesi hutoboi maana as much as wana makosa ila expropriation ya mali za mwekezaji ni serious offence!!

Kwa hiyo huyo huyo unayemsifia ilibidi atumie akili kuliko miguvu ili kupata popularity ya wapiga kura. So hatuna vita yoyote ila incompetence yetu ikiwa exposed tunalialia eti vita.
Unadhani unaweza kushinda hata kama ushahidi upo wazi? Watanzania wenzio walikua wanatafuta dada kuiba usiku na mchana Ili wawape wale jamaa Kwa ajili ya kuandaa kupinga. Mkemia anakazimishwa abadili dada kuleta uhalisia wa mihemko.

Ile vita kama taifa lingeshikamana vyema bila bla blaa hakika tungeshinda Kwa asilimia 100. Saiz hata kesi tulizoshinda wanafufua wanashinda wanapiga pesa. Yote hayo Kwa nini? Kiongozi alieponhana uwezo wa kuwakemea hao hao wa ndani achilia support ya mabeberu.
 
Yaan hua najiuliza watu wa namna hii, hata kama ni umasikin ndio ushindwe kutambua how African nations are made under developed? Ufusadi mkubwa ni ule wa maliasili. Kusaini mkataba unaompendelea beberu, nchi inakosa wewe binafsi unapewa kidogo unazani maraisi wote wa Afrika wanapenda? Kikwete alipenda Ile namna ya uongozi wake wa Kila mtu holela?

Kuna kua na nguvu kubwa inayokusukuma ukubali hayo. Kukukataa unakua sio mmoja wao. Watakufanyia figisu Hadi uchoke.

Tambua ndani ya nchi sio Kila mtu anakua na mawazo kama ya kwako. Hata katika chama sio wote wanakukua na mawazo ya kutimiza Irani ya vyama vyao. Wengine wapo Kwa masrahi yao.

Wewe kama mwenyekiti wa chama kupambana nao ndani ya chama ni kama Magufuri na kina Nape na January na wengine. Watu waliomlengwa tofauti na wewe ni rahisi kuhongeka na kukufanyizia lollote like Ili masrahi ya mabeberu yatawale. Wewe usipochukua wenzio watachukua.Ukikataa wanaremove obstacle.

Elewa kwamba masrahi ya mabeberu ndio chanzo Cha matatizo na ufusadi uliokithiri. Ukiwa mzalendo wanakupa jina la obstacle, then grant ya kukuremove Kwa support ya watu wako wa ndani na sio wao.

Mafisadi wa ndani ya nchi bila support ya mabeberu kumuweza rais aliekua amejidhatiti Kwa ulinzi kama JOM sio rahisi kihivyo ufikiriavyo.

R.I.P Jembe Magu...
Ujinga wa kulaumu wengine wakati mikataba tunaandika sisi ni wa kizamani mno. Bandari mnayotaka kumpa mwarabu kaja kuichukuwa kwa nguvu? Kama kosa ni la viongozi mbona raia wamelemaa bila kuchukuwa hatua? Mwafrika anajiangamiza mwenyewe na hakuna wa kumlamu.
 
Hiyo dhana ya ''vita ya uchumi'' ni moja ya vitu ambavyo Magufuli alifanikiwa kuwaaminisha wafuasi wake na mpaka kesho bado wataendelea kumsujudia. Ni kama vijijini, watu maskini wanavyoaminishwa na waganga au wenyewe kwa wenyewe kuwa umaskini wao unatokana na husda, vijicho na ulozi wanavyofanyiwa na maadui zao. Unakuta mtu ana nyumba ya nyasi na watoto 15, fedha yake yote inaishia kwa waganga kwa kuamini kuwa magonjwa, umaskini na kila aina ya masahibu yake yanatokana na kijicho cha maadui.
Ukiskia vita ya Uchumi unaelewa nini?
Kuhangaika kurekebisha mikataba ya madini sio vita ya Kiuchumi?

Miradi kupigwa vita eti inaharibu mazingira sio vita ya Kiuchumi?
We ukiskia vita ya kiuchumi unaelewa nini?
 
Nadhani bora anaweza kujua hata tatizo
Yep. Hili halina ubishi. Alikuwa anachukia ufisadi na uzembe kutoka rohoni lakini tatizo alikuwa hana upeo wa kushughulikia. N ambaya zaidi akawa anachagua wanafiki kwenye serikali yake na watu waliokuwa wanamwambia ukweli alikuwa anawaona kama maadui. Pengine hii ilitokana na kasoro mbili kubwa alizokuwa nazo. 1. kupenda kusifiwa 2. kupenda baadhi ya watu kutoka kanda fulani na kuchukia wengine.
 
Uwe unatofautisha kati ya uhalisia na propaganda
 
Nyie watu vita vya kiuchumi mnavijua kweli au propaganda za yule jamaa yenu wa chato.

Hebu katazame U.S - China trade war ndio ujue vita vya kiuchumi vipoje sio huu upuuzi wenu wa jamaa yule wa chato.

Tazama sasa magharibi na Russia wanavyo pigana kiuchumi

Hivyo ndivyo vita vya kiuchumi sio vya jamaa wa chato vya maneno ya majukwaani.

Unaita vita vya kiuchumi hata kiwazo hata kimoja cha kumiza kichwa hujapigwa hivi ni vichekesho
Vita ya majogoobwawili ni tofauti na vita ya vifaranga nani akae wa kwanza kwenye bawa la mama yao.
 
Back
Top Bottom