nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2][/h]THURSDAY, 18 AUGUST 2011 13:58 NEWSROOM
NA MWANDISHI WETU UHURU
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, amemvaa Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akimtuhumu kuhusika na ugawaji wa vizimba 344 katika jengo la Machinga Complex, kinyume cha taratibu.
Zungu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Machinga Complex, ambaye aling'atuka kwa hiari yake Septemba, mwaka jana, kufuatia mchakato wa kugombea ubunge wa jimbo hilo. Hivi sasa bodi hiyo inaongozwa na Diwani wa Kata ya Upanga, Godwin Mmbaga.
Dk. Masaburi, pia ameuagiza uongozi wa bodi mpya kuvunja mikataba iliyotiwa saini na uongozi wa Zungu, na ameamuru waliopewa vizimba na uongozi huo wanyang'anywe mara moja.
Aidha, ameagiza wafanyabiashara ambao wamepewa vizimba, lakini bado hawajahamia, wanyang'anywe vizimba hivyo na kisha wapewe wafanyabiashara wengine. Kwa upande wake, Zungu alisema Dk. Masaburi hana mamlaka ya kuwahamisha wafanyabiashara katika jengo hilo.
Kimsingi, alisema mchakato wa kuwapata wafanyabiashara waliopanga katika jengo hilo, ulizingatia kanuni na sheria ambapo walichukua wafanyabiashara kupitia vyama vyao na wasio na vyama.
"Hayo mamlaka ya kuwanyang'anya watu vizimba ameyatoa wapi, wafanyabiashara wote wameingia mkataba na mkurugenzi wa jiji na si yeye," alisema Zungu kwa njia ya simu akiwa bungeni mjini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea jengo hilo lililopo Ilala, Dar es Salaam, Dk. Masaburi alisema bodi iliyokuwa inaongozwa na Zungu ilitumia mfumo mbovu kugawa vizimba hivyo.
Alisema bodi mpya inapaswa kuangalia uwezekano wa kuwahalalisha wafanyabiashara waliopangishwa kinyemela katika jengo hilo, iwapo watafuata sheria na kanuni zilizowekwa.
Pia, Dk. Masaburi aliitaka bodi hiyo kutangaza zabuni ili wafanyabiashara wakubwa wapate nao nafasi katika jengo hilo, hali itakayochangia kuongezeka kwa mapato kutokana kodi watakayolipa.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Dk. Masaburi inaonekana kupingana na agizo la Rais Jakaya Kikwete, aliyetaka jengo hilo litumiwe na wafanyabiashara ndogo ndogo. Kwa upande wake, Katibu wa Bodi mpya ya Machinga Complex, Teddy Kundi, alisema bodi itayafanyia kazi maagizo yaliyotolewa na meya, na kwamba kwa kuanzia, jana ilianza kuwanyang'anya vizimba wafanyabiashara waliotakiwa kuondoka.
Alisema watahakikisha wafanyabiashara waliopangishwa vizimba na bodi ya zamani wanaondoka mara moja na wale ambao hawajaanza kuingiza biashara wananyang'anywa na kupewa wengine. Sambamba na hilo, Teddy alisema jengo hilo linatarajiwa kubadilishwa jina, ambapo badala ya kuitwa Machinga Complex, sasa litajulikana kama Business Park.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara katika Jengo hilo, Gerald Mpagama, alisema haungi mkono uamuzi wa Dk. Masaburi wa kutaka kuwahamisha wafanyabiashara katika jengo hilo.
Alisema lengo la serikali kujenga jengo hilo ni kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, na kwamba iwapo walengwa watahamishwa katika jengo hilo, watakuwa hawawatendei haki.
Mpagama alisema tangu jengo hilo lilipofunguliwa, mwaka jana, jumla ya wafanyabiashara 800 ndio waliohamia katika jengo hilo, na kwamba idadi kubwa bado haijaingia kutokana na madai ya kukosa wateja.
Hivi karibuni, Dk. Masaburi alifanya ziara ya kukagua vitega uchumi vya Shirika la Maendeleo la Halmashauri ya Jiji (DDC), ambapo aliamua kuvunja bodi kutokana na kukithiri kwa madai ya ubadhirifu wa mali za shirika hilo
LAST UPDATED ( THURSDAY, 18 AUGUST 2011 14:45 )