'Vita' ya Masaburi, Zungu bado mbichi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Vita' ya Masaburi, Zungu bado mbichi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Aug 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]THURSDAY, 18 AUGUST 2011 13:58 NEWSROOM


  [​IMG]NA MWANDISHI WETU UHURU
  MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, amemvaa Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akimtuhumu kuhusika na ugawaji wa vizimba 344 katika jengo la Machinga Complex, kinyume cha taratibu.

  Zungu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Machinga Complex, ambaye aling'atuka kwa hiari yake Septemba, mwaka jana, kufuatia mchakato wa kugombea ubunge wa jimbo hilo. Hivi sasa bodi hiyo inaongozwa na Diwani wa Kata ya Upanga, Godwin Mmbaga.

  Dk. Masaburi, pia ameuagiza uongozi wa bodi mpya kuvunja mikataba iliyotiwa saini na uongozi wa Zungu, na ameamuru waliopewa vizimba na uongozi huo wanyang'anywe mara moja.


  Aidha, ameagiza wafanyabiashara ambao wamepewa vizimba, lakini bado hawajahamia, wanyang'anywe vizimba hivyo na kisha wapewe wafanyabiashara wengine. Kwa upande wake, Zungu alisema Dk. Masaburi hana mamlaka ya kuwahamisha wafanyabiashara katika jengo hilo.

  Kimsingi, alisema mchakato wa kuwapata wafanyabiashara waliopanga katika jengo hilo, ulizingatia kanuni na sheria ambapo walichukua wafanyabiashara kupitia vyama vyao na wasio na vyama.

  "Hayo mamlaka ya kuwanyang'anya watu vizimba ameyatoa wapi, wafanyabiashara wote wameingia mkataba na mkurugenzi wa jiji na si yeye," alisema Zungu kwa njia ya simu akiwa bungeni mjini Dodoma.

  Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea jengo hilo lililopo Ilala, Dar es Salaam, Dk. Masaburi alisema bodi iliyokuwa inaongozwa na Zungu ilitumia mfumo mbovu kugawa vizimba hivyo.

  Alisema bodi mpya inapaswa kuangalia uwezekano wa kuwahalalisha wafanyabiashara waliopangishwa kinyemela katika jengo hilo, iwapo watafuata sheria na kanuni zilizowekwa.

  Pia, Dk. Masaburi aliitaka bodi hiyo kutangaza zabuni ili wafanyabiashara wakubwa wapate nao nafasi katika jengo hilo, hali itakayochangia kuongezeka kwa mapato kutokana kodi watakayolipa.

  Hata hivyo, kauli hiyo ya Dk. Masaburi inaonekana kupingana na agizo la Rais Jakaya Kikwete, aliyetaka jengo hilo litumiwe na wafanyabiashara ndogo ndogo. Kwa upande wake, Katibu wa Bodi mpya ya Machinga Complex, Teddy Kundi, alisema bodi itayafanyia kazi maagizo yaliyotolewa na meya, na kwamba kwa kuanzia, jana ilianza kuwanyang'anya vizimba wafanyabiashara waliotakiwa kuondoka.


  Alisema watahakikisha wafanyabiashara waliopangishwa vizimba na bodi ya zamani wanaondoka mara moja na wale ambao hawajaanza kuingiza biashara wananyang'anywa na kupewa wengine. Sambamba na hilo, Teddy alisema jengo hilo linatarajiwa kubadilishwa jina, ambapo badala ya kuitwa Machinga Complex, sasa litajulikana kama Business Park.


  Naye, Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara katika Jengo hilo, Gerald Mpagama, alisema haungi mkono uamuzi wa Dk. Masaburi wa kutaka kuwahamisha wafanyabiashara katika jengo hilo.


  Alisema lengo la serikali kujenga jengo hilo ni kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, na kwamba iwapo walengwa watahamishwa katika jengo hilo, watakuwa hawawatendei haki.


  Mpagama alisema tangu jengo hilo lilipofunguliwa, mwaka jana, jumla ya wafanyabiashara 800 ndio waliohamia katika jengo hilo, na kwamba idadi kubwa bado haijaingia kutokana na madai ya kukosa wateja.


  Hivi karibuni, Dk. Masaburi alifanya ziara ya kukagua vitega uchumi vya Shirika la Maendeleo la Halmashauri ya Jiji (DDC), ambapo aliamua kuvunja bodi kutokana na kukithiri kwa madai ya ubadhirifu wa mali za shirika hilo


  LAST UPDATED ( THURSDAY, 18 AUGUST 2011 14:45 )
   
 2. k

  kautipe Member

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata masaburi hana lolote! kafilisi mradi wa mabasi ya wanafunzi wa dar es salaam yaliyokuwa chini ya umoja wa vijana. Kabla yake mradi ulikuwa unaendelea vyema, alipokuja ukafa
   
 3. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Je, mkuu wa nchi anasemaje juu ya haya mambo ya kipuzi puzi yanayoendelea ndani ya hii nchi? Au yuko safarini kama kawaida yake?
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyu Mayor Masaburi anataka kuleta balaa. Anasema 'zabuni itangazwe ili wafanyabiashara wakubwa nao wapate nafasi katika jengo hilo'. Really? Hivi inawezekana kuwa kusudi kubwa la Masaburi kuvunja bodi, kufukuza baadhi ya machinga ni mkakati wake wa kuwapatia nafasi 'wafanyabiashara wakubwa? Kama ndivyo, nini hasa maana ya kujenga jengo la Machinga? Kwanza machinga ni mtu wa aina gani?

  Nashauri Mh Zungu aandae maandamano. Bila hivyo huyu Mayor wa Dar es Salaam atauza hili jiji lote. Ana kila dalili za kuwa mtu katili. Hana huruma hata kidogo kufukuza watu wadogo kama machinga kwa kisingizio cha kupata kodi kubwa toka wafanyabiashara wakubwa! Hawa waliofukuzwa walishe vipi familia zao? Kama sio kusukuma watu kuwa vibaka ni nini hasa huyu mayor anafanya? Maandamano Mh Zungu tafadhali.
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hoja yako ni nzuri mno ila umeitoa kwa jazba mno kiasi naona kama onaenda offtrack (maono yangu), mimi simuungi mkono juu ya hoja ya kuwapa wafanyabiashara wakubwa, lakini nilivyomuelewa ni kuwa wale wanaohodhi yale maeneo na hawatumii wanyanganywe (kama ni kweli big up). Sasa sijui unataka zungu aandamane kutetea kuwa hii cemplex iendelee kuwa danguro na kijiwe cha mihadarati (kama ilivyosasa) au huna habari hii?, namuunga mkono Mayor kuwatimua wanaomiliki vizimba sasa kwa sababu hawavitumii.
  <br />
  <br />
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  wote wanafikiria kwa kutumia mananiii yao
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu masaburi ana digrii ya kuvunja bodi nini?....UDA.........Machinga Complex....next?
   
 8. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mbunge Zungu akishindwa kuitisha maandamano basi CDM chukueni hiyo nafasi ya kutetea watu wanyonge wasidhurumiwe haki zao na mafisadi!!!!!!!!!!!!! Masaburi hatumii akili, anafikiri kwa kutumia viatu!!!!!!!!
   
 9. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Akimaliza hapo anaenda soko la Kariakoo
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wewe pia huna lolote wamachinga wamelalamika muda mrefu hata Kikwete analielewa hili kuwa pale happana biashara kwa sababu ya lile soko la ilala.
  Wakati watu wanasubiri soko la ilala livunjwe na watu warudi machinga yeye anakuja na mbinu zake za kutaka kujinufaisha kwa ajiri ya machinga.

  Avunje kwanza mchikichini halafu na machinga wamchikichini warudi i katika vizimba vyao huko machinga complex
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Wewe unataka kutatua tatizo au kukuza tatizo-?, soko la ilala livunjwe ili machinga complex wafanye biashara? Kwa hiyo macginga wa machinga complex hawafikirii kufanya biashara nyingine tofauti na ile ya ilala?
  <br />
  <br />
   
Loading...