Vita ya maneno kati ya Rwanda na Burundi: Ina maana Ndayishimiye hajui tu kama amekalia kuti kavu?

Umemuandika Ndayishimiye kama mtu binafsi zaidi na sio kama Rais aliyeapa kuilinda Burundi.

Wasi wasi wako mkubwa upo kwenye Urais wake na sio Burundi.

Uenda, hana uchungu na urais wake kuliko Nchi yake.
Sasa kama anajipenda yeye na nchi ni bora angetumia ujuzi wake kuepusha vita kati ya nchi hizo mbili maana bila hivyo itakula kwake.
 
Nakubali asilimia mia Fdrl wana silaha kali sana za kivita ila tatizo lao moja ,majeshi ya Congo kutelekeza silaha na kutimua mabio uwanja wa vita ni kawaida sana
Mwanajeshi anaenda vitani huku ana redio akifika sehemu anaweka bunduki chini, anawasha redio na kuanza kumsikiliza falii pupaa huku akikataa mauno kama yote.

Akija kushtuka M23 wapo nyuma yake, wanamnyang'anya silaha na kumuua au kumteka.
 
Wampige mande majirani zake wote aliohasimiana nao DRC&Burundi najua Uganda anaweza toa msaada hata asipokuwa Frontline.
Hapana Uganda hatoingilia maana wana kaundugu fulani. Burundi na Congo wanaweza kujiunga, ila tatizo Burundi itajikuta inapambana peke yake huku jeshi la Congo likiwa limetimkia Lubumbashi kwenye shoo ya Kofi Olomide.
 
Kwamba ww unataarifa kuliko raisi wa nchi ya burundi?

Taarifa za jeshi ni siri, we Uganda umeipimaje?

Punguza kushinda karume pale kijiweni
Unaweza kuwa raisi lakini baadhi ya mambo ukawa huyajui mpaka watu wa pembeni kama sisi tukuambie.
 
Ila bongo Kuna wajuaji wengi ambao sio wafuatiliaji wa mambo na ujuaji unaponza wengi.

Najua umeanza kumjua Ndarishimiye alipoteuliwa kama Katibu mkuu wa Chama tawala nchini humo na Nkuruzinza na historia yake ya nyumba huifahamu

RAIS wa Burundi wa Sasa kabla ya kuingia siasani alikuwa ni mkuu wa majeshi wa nchi hiyo na sidhani kama wewe unayeishi uvinza utakuwa na taarifa za intelijensia za usalama na ulinzi kuliko mtu ambaye amewahi kuwa mkuu wa majeshi wa Taifa.

Tatizo mnajazwa upepo mnajaa kabisa ila nakuhahakishia Rwanda Sasa hivi atatulia mazima maana Tshisekedi anaichemsha dawa yao na aliahidi wakati wa kampeni
Ndayishimiye watu tunamjua kabla hata ya vita vya Burundi kuanza. Nnachoshauri asije akafuata ushauri wa mtu kama wewe baadae akaja kujilaumu kwa ujinga ataotumia kujipima ubavu na Rwanda.
 
Kweli ....tatizo la askari wa kagame lipo kwenye akili ....akili zao zinadhani urefu wao ndiyo akili hivyo ni rahisi sana kuwashinda kivita ....kwa sasa askari wa kagame congo wanauliwa kama kumbikumbi
Mkuu umetumia cha Arusha au cha mw/nyamala?
 
Back
Top Bottom