Vita ya biashara ya machimbo ya ziwani: Mazingara na Miiko ya Uvuvi wa Dagaa katika Ziwa Victoria.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
IMG_6939.GIF


Nikiwa kama shuhuda wa uvuvi wa dagaa katika Ziwa Victoria, mwanzoni mwa 2000s, nimeona nishare nanyi juu ya intelligence itumikayo katika uendeshaji wa shughuli za uvuvi katika Ziwa hilo.
Ziwa Victoria, ndilo probably Ziwa bora kabisa kuliko maziwa yote duniani kutokana na kuwa na upana mkubwa (nyuma tu ya Ziwa Superior) tena katika Ukanda wa joto jingi huku likiwa na kina kifupi (mita 71) kinachowezesha mwanga wa jua ku-penetrate kwa ubora hadi chini. Hali hii imewafanya samaki wa asili wa Ziwa hilo kuwa watamu sana (achana na sangara, dagaa na sato (wapya) - wote hao ni wa kuja tu). Sato wa asili (hawapatikani) na wengine wengi waliopotea, ndio wamechangia kwa kiwango kikubwa ku-mold jamii za watu among the brightest hapa Tanzania (Wahaya, Wakerewe, Wakara na Wazinza etc). Baada ya samaki wa asili hasa sato kushindwa kuhimili ongezeko la mahitaji nchini, Waingereza waliamua kudumbukiza sangara miaka ya 1950s, ikifuatiwa na Sato wapya, pamoja na dagaa.

IMG_6935.JPG IMG_6936.JPG IMG_6942.JPG
Uvuvi wa Dagaa, ni shughuli inayofanyika katika kipindi cha usiku wa giza kwa kutandaza taa (karabai) juu ya maji, hali inayowavutia dagaa kuufuata mwanga huo. Kwa kuwa, kwenye mbalamwezi kuna mwanga duniani, uvuvi huwa unasimama. usiku wa giza (Giza) huwa unachukua wastani wa wiki 2 - 3 kulingana na upatikanaji wa dagaa. Giza ambazo huwa nzuri kwa mwaka, ni za Msimu wa Kiangazi kuanzia Mwezi Julai - Novemba. Kipindi hiki mawimbi ya Ziwa huwa siyo makubwa na pepo huwa hazibadiliki badiliki (reliability) tofauti na kipindi cha mvua unaoanza Mwezi Disemba - Mei. Zamani (kabla ya 2000s), kipindi hicho cha mvua, uvuvi wa dagaa ulikuwa ukisimama kwani watu waliwekeza nguvu kwenye kilimo ili kupata chakula. Mvua zilikuwa nyingi na za mfululizo, zijulikanazo kama "kabhoja." Kwa kawaida dagaa aliyevuliwa hatakiwi kuguswa na maji akishaanikwa kwani ubora/bei yao hupungua maradufu. Kipindi hicho cha mvua, ndipo samaki wengine kuanzia sato (tilapia), furu, sangara, kambale, gogogo (ngere) na wengine walikuwa wakipatikana kwa wingi sana. Na kwa kuwa wenyeji wa Kanda ya Ziwa, hupendelea samaki aina ya sato, mumi, kambale, kamongo (emamba), gogogo (Ngere), ningu, mbofu etc, ilipelekea uvuvi wa dagaa kusimama.

Zifuatayo, ni baadhi ya tabia zilizozoeleka sana kwenye jamii za wavuvi kiasi cha kutengeneza miiko na utamaduni mpya katika industry ya uvuvi katika Ziwa Victoria.
Ziwa ni eneo la maji lenye mazingara mengi na ya hatari sana kwa walitumialo. Ukiwa abiria hautaweza kuelewa uzito wa hoja hii lakini kama unatafuta maisha kupitia maji, ni lazima ufuate miiko ya majini ili ufanikiwe. Mnapokuwa ziwani, mnaweza kutokewa na mazingara ya aina yoyote: mrembo mkali sana, meli kubwa sana ambayo hutegemei kuiona ziwani humo, ama meli inakuja kama kuwagonga, ama kitu chochote cha ajabu. Unachopaswa kufanya ni kunyamaza na kutulia kabisa bila kuongea juu ya ulichokiona. Unaweza kuwakonyeza tu mwenzako tu lakini si kuongea. The moment mtakapoongea basi ndio mkosi wenu: mnaweza kuzama ama kuambulia kapa kabisa. Ikitokea ukaongea, utatakiwa kukata kidole chako ili damu uitiririshe majini kama ishara ya kuomba msamaha. Miungu hiyo inaweza kukubali ombi lako ama ikakataa. Hali ikiendelea kuwa mbaya, ina maana hawajakubali ombi lako so amini nakwambia wenzako lazima watakudumbukiza ziwani.
Mitumbwi ya uvuvi lazima izindikwe ili iweze kufanya kazi zake vyema. Msipouzindika mtumbwi na vyombo vya uvuvi, hamwezi kamwe kupata dagaa. Mnaweza kuwa mnapata mikosi ya kila aina ya kuharibikiwa mashine ama mtumbwi kwa mazingara ya kishirikina. Mtumbwi usiozindikwa ni rahisi kupasuliwa na kiboko (Hippo) na kuwazamisha. Kiboko hawasogekei mitumbwi iliyozindikwa.

Kwa muda mrefu, Giza ya Mwezi wa Sita ilikuwa ikiogopwa sana na wavuvi kwa kuwa, ilikuwa ni lazima kila mwaka, angalao mtumbwi mmoja uzame na kuua watu. Hivyo, wananchi wengi walihusisha suala hilo na utoaji kafala ziwani. Baadhi ya wavuvi kwa kipindi hicho cha Mwezi Juni, walikuwa wakikacha kwenda kutega giza hiyo kwa kuamua kukaa tu nyumbani. Hata hivyo, sidhani kama hali hiyo inaendelea hivi sasa.
Zamani, ilikuwa ni aibu sana kwa kijana kujihusisha na uvuvi na ilikuwa ni kitu nadra kabisa kwa mabinti/wanawake kwenda mialo ya uvuvi kwa kuwa ilionekana ni umalaya wa hali ya juu. Hata hivyo miaka ya 1990s, baada ya mahitaji ya dagaa kuongezeka Nchi nzima mialo ya uvuvi imevutia wengi.
Kambi za uvuvi (vijiji), zimeendelea sana katika style ya maisha. Licha ya changamoto ya umeme, wakazi wengi kutoka mijini (Mwanza, Bukoba, Musoma etc) kwenda kufanya biashara huko visiwani na kupelekea kuwepo kwa ustaarabu mkubwa sana maeneo hayo. Biashara iliongezeka sana huku ikitegemea hali ya giza. Leo hii mialo imekuwa centre kubwa tu za kibiashara.
Wavuvi wanapokuwa wameua sana dagaa, hali huchangamka sana watakuwepo: utumaji pesa nyumbani; gesti kujaa muda wote; bia hutafunwa sana na wazee wa gambe (bia). Kanda ya Ziwa wanakunywa sana bia kutokana na wingi wa wavuvi na wachimbaji wa madini.
Kazi ya uvuvi huchosha sana, hivyo wavuvi wanapokuwa na Giza nzuri, basi huwa wanapendelea hali ya hewa kuwa mbaya siku za mwisho mwisho ili walale nchi kavu na kukutana na wanawake (malaya), hii ni kwa sababu, hali isipokuwa mbaya wataendelea kutega bila kulala na michepuko Yao iliyozagaa huko. Uzoefu unaonyesha kuwa, watu wengi kwenye mialo huombea hali ya hewa iwe mbaya siku za mwisho mwisho ili wavuvi washindwe kuingia majini na kujikuta wanaspend kwa siku hizo. Wavuvi wengi waliooa, hujikuta wakiwa na mahawala huku wengi wakijikuta wakizaa nayo (na hivyo kuoa mke wa pili).
Ukiacha kwenye migodi ya Dhahabu iliyotapakaa Kanda ya Ziwa na ya Tanzanite Mirerani, walahi hakuna sehemu yoyote nchini ya vijijini ambako kuna mabinti/wanawake wakali wanaojiuza kama kwenye mialo ya uvuvi. Mabinti ni wakali balaa lakini huwa wanaanza kuja hasa wiki ya pili baada ya uvuvi kuchanganya. Linapokuja suala la kugambeka na mikasi, hakuna maeneo nchini ya kuyalinganisha nayo hata wa mijini hawafui dafu.
Zamani kidogo kabla ya 2000s, kulikuwa kukifanyika matamasha ya kimziki/disco vumbi maarufu kama "mazinduke." Yalikuwa nayo yanaanza siku za kuanzia wiki ya pili ya giza lakini walikuwa wakikusanya hela nyingi balaa. Kwenye disco hilo, wavuvi walikuwa wakishindana ili kupigiwa muziki na kucheza huku anayetangaza dau kubwa anapigiwa muziki wa dakika 5 hivi. Dau liliweza kupanda hadi 100,000. Mabinti wao huwa ni washapu kutoa huduma ya haraka (chomolea). Hata hivyo, Serikali ilikuja kupiga marufuku mazinduke baada ya wavuvi kuwa wanarudi majumbani kwao mikono mitupu.
Fedha za uvuvi kama zilivyo za madini, huwa zinalalamikiwa kuwa ni za mashetani kwa namna zinavyoisha bila kutarajia. Masikini kupata fedha kwa mkupuo, huwa kunamzuzua na ukifikiria alikuwa hajaipangilia, hivyo atapiga kwa expectation ya kupata nyingine. Ndiyo maana wavuvi kama ilivyo wachimbaji madini wengi wao huishia kuwa masikini tu kulinganisha na let's say wamachinga walioko maeneo hayo. Ni wachache huwa wanafanya vitu vya maana.
Zamani kabla ya 2000s, mialo ya uvuvi, ilikuwa ndo kimbilio namba 1 la wahalifu nchini kwa kuwa hakukuwepo Serikali huku ubabe na kufanyiziana kukiwa kwa kawaida sana. Hata hivyo, nowadays kuna wasomi wengi tu huko nao wanaenda kufanya biashara na hata nguvu ya Serikali imeimarishwa kwa kiwango kikubwa.
Ujambazi ni jambo ambalo kwa kiwango kikubwa lilitaka kuua biashara ya dagaa kutokana na kumbuka kwa tabia ya utekaji na mauaji ya kutisha. Wale wauaji ambao mara nyingi walidaiwa kutokea mijini (Mwanza, Bukoba na Musoma) walikuwa wanawatenda vibaya sana wavuvi wasio na makosa kwa kuiba karabai na nyavu. Kwa kuwa kila wavuvi wanaponyang'anywa vyombo vya uvuvi walikuwa wanatuhumiwa na matajiri zao kuwa wameuza vifaa vya uvuvi, majambazi yaliamua kuja na njia za kumwachia alama/kovu mvuvi ili asisumbuliwe na bosi wake. Majambazi walikuwa wakikuuliza kuwa "unataka kucheka (kukatwa midomo) ama kaoshi (kukatwa mikono)?" Ukizingua mwenyewe walikuwa wanakuua.
Pamoja na kuwa mkali wa Jiografia kipindi hicho tangu O-level, nilishangaa jinsi wavuvi ambao hawajasoma walivyokuwa na sense kubwa sana juu ya hali ya hewa. Wakati wa asubuhi kwa kuona tu hali ya upepo, walikuwa na uwezo wa kubashiri kwa usahihi kuwa, hali ya hewa wakati wa usiku itakuwa mbaya ama nzuri. So, sisi tusio na uelewa huo wa elimu ya pepo tulikuwa tukishangaa tu kuona wenzetu wataalam wakitoa udhuru na kusafiri kwenda kuona familia zao hadi kesho yake kwa sababu hata ninyi hamtaenda kuvua. Hili suala limekuwa likinifanya nijiulize sana juu ya aina ya elimu yetu na maana ya intelligence.
 
Sasa hao wanaowatokea wavuvi na ku-control uvuvi wao huko majini ni akina nani? Fallen Angels? Aliens? Majini? Mahoka, Shetani, Watchers?
Who are they anyway?
Nasema haya coz mimi kama mkristo nilikuwa nayapinga sana masuala hayo but nilivyokwenda kujifunza uvuvi kipindi hicho natafuta karo ya shule, ndipo nilikubaliana kuwa, kuna kitu kinatu-control bila msaada wa mtu mwingine. Possibly na mimi ningeadhibiwa kwa sababu tu nilishangaa kuona ndege jamii ya bata halafu mzuri sana nikajisahau na kumwongelea licha ya kukatazwa kuongea chochote nitakachoona majini. Isingekuwa uwepo wa ndugu yangu, sijui suala hilo lingeishaji. Vilevile, nilipata shuhuda za baadhi ya wavuvi juu ya watu waliokataa awali kuizindika mitumbwi yao, wote hao walishindwa mapema biashara na kwenda kuizindika.
Vilevile, nilichojifunza huko ni kuwa, dawa ya kuzindika zinazidiana, kuna mwingine anakuja na dawa yenye nguvu halafu atatamba kwa muda fulani na ataanguka na kuja mwingine. Hii ni kwa sababu, dawa wanazozindika, zina-expire muda wake lazima u-renew.
 
Umenikumbusha,, 2014 nilienda kisiwani huko kufuata dagaa nikiwa na sister duu wa huko visiwani ambae niliunganishwa awe mwenyeji wangu... Ile nimefika kwenye ule mwalo unajua kupandiwa dau na kugombaniwa huku mi sina habari!!
kiufupi kule pesa ipo ukijichanganya lazima utoke..
nawashangaa wale wanaotafuta kazi wakati huko kazi zimejaa
 
Usiku ule tulienda disco vumbi acha kabisa yani kuna vituko vyenye raha ndani yake.... Ila wavuvi wana uchu sana wa wanawake sijui kwa nini??
Unasema kweli, wanaume wanaofanya kazi ngumu huwa hawapati muda wa kustarehe, so wanapopata chance huwa wana ugwadu mkubwa sana na kwa kuwa huwa wana hela huwa hawataki kukubali kushindwa. On top of that, weka sifa nyingine ya sisi wengine tuliotoka maisha ya kimasikini, it's likely ukipata fedha unakuwa kama limbukeni fulani hivi. Hii tabia ipo mpaka nchi za mbele: angalia ulimbukeni wa akina Tyson, 50 cent na wengine kibao, walivuna mabilioni but today wanaelekea kuwa masikini, Why? Mnamuona yule dogo Mayweather, kiukweli anatuaibisha sisi blacks popote tulipo. Haonekani kujifunza kuwa hatapigana miaka yote. Ananunua saa ya bei ya kufuru ya nini, mtu mwenyewe alizipata fedha kwa kuaibika ulingoni kwa kushushiwa mingumi usoni halafu anajidai mjanja.
 
Unasema kweli, wanaume wanaofanya kazi ngumu huwa hawapati muda wa kustarehe, so wanapopata chance huwa wana ugawadu mkubwa sana na kwa kuwa huwa wana hela huwa hawataki kukubali kushindwa. On top of that, weka sifa nyingine ya sisi wengine tuliotoka maisha ya kimasikini, it's likely ukipata fedha unakuwa kama limbukeni fulani hivi. Hii tabia ipo mpaka nchi za mbele: angalia ulimbukeni wa akina Tyson, 50 cent na wengine kibao, walivuna mabilioni but today wanaelekea kuwa masikini, Why? Mnamuona yule dogo Mayweather, kiukweli anatuaibisha sisi blacks popote tulipo. Haonekani kujifunza kuwa hatapigana miaka yote. Ananunua saa ya bei ya kufuru ya nini, mtu mwenyewe alizipata fedha kwa kuaibika ulingoni kwa kushushiwa mingumi usoni halafu anajidai mjanja.
Hahaha!!! Sie maskini tuna tabu sana
 
Mkuu sio kila mtumbwi unazindikwa(ila wapo wanaozindika)
Kuhusu viboko kwa sasa wamepungua sana, mara ya mwisho kuona kiboko ilikuwa 2006 au 2007.
halafu miezi mizuri kwa upatikanaji wa dagaa inatofautiana kulingana na maeneo kwa mfano visiwa vya Bumbire mwezi wa 7na 8 dagaa hawapatikani lakini goziba na kinagi dagaa wanapatikana kwenye miezi hiyo.
Nimezaliwa kisiwani,nimesomea kisiwani na bado nipo kisiwani,in other cases you are right
 
Mkuu sio kila mtumbwi unazindikwa(ila wapo wanaozindika)
Kuhusu viboko kwa sasa wamepungua sana, mara ya mwisho kuona kiboko ilikuwa 2006 au 2007.
halafu miezi mizuri kwa upatikanaji wa dagaa inatofautiana kulingana na maeneo kwa mfano visiwa vya Bumbire mwezi wa 7na 8 dagaa hawapatikani lakini goziba na kinagi dagaa wanapatikana kwenye miezi hiyo.
Nimezaliwa kisiwani,nimesomea kisiwani na bado nipo kisiwani,in other cases you are right
Huko visiwani gongo kama maji vile
 
dah uko ndiko nilizaliwa kwenye kisiwa cha Meisome ila tulihama kitambo sana
Maisha ya kisiwani raha sana
Yani kisiwani raha sanaa... nililala gest moja charge elfu mbili mlango hauna kitasa afu njemba ziko nje zinanilinda kuhakikisha hakuna anaekula mzigo wala mimi kuibiwa...
Alfajili nikasindikizwa na belia zote wakapigiwa cm sikusumbuliwa mimi na mzigo wangu
 
Mkuu sio kila mtumbwi unazindikwa(ila wapo wanaozindika)
Kuhusu viboko kwa sasa wamepungua sana, mara ya mwisho kuona kiboko ilikuwa 2006 au 2007.
halafu miezi mizuri kwa upatikanaji wa dagaa inatofautiana kulingana na maeneo kwa mfano visiwa vya Bumbire mwezi wa 7na 8 dagaa hawapatikani lakini goziba na kinagi dagaa wanapatikana kwenye miezi hiyo.
Nimezaliwa kisiwani,nimesomea kisiwani na bado nipo kisiwani,in other cases you are right
Uko sawa kabisa, kanda za uvuvi Ziwa a Victoria huwa zinahama hama. Hata hivyo, Zone ya Kisiwa cha Goziba iliyopo Kati ya Bukoba na Ukerewe ndiyo inayo-dominate karibia kwa mwaka mzima kutokana na kuwa katikati ya Ziwa, tena Ukanda unaopata mvua nyingi kuliko eneo lolote katika Kanda ya Ziwa.
Nafurahi kuwa una uzoefu wa kutosha, so utasaidia kujibu hoja za wadau humu.
 
Back
Top Bottom