sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Maamuzi mengi ya serikali yanapitia kwenye Baraza la Mawaziri chini ya Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Uwajibikaji wa serikali unamlenga waziri mkuu kwa kuwa ndiye msimamizi mkuu wa kazi zote za serikali,na waziri Mkuu huyu atapokea maelekezo toka kwa Rais na si vinginevyo.
Drama inaanzia pale Mwenezi wa chama anapompa msimamizi wa maelekezo ya Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama siku Sita kutatua migogoro ya Ardhi kupitia wizara tatu ambayo wizara moja Iko chini ya ofisi ya Rais ambaye ndiye mwenye dhamana ya kupeleka jina la Mwenezi kwenye Halmashauri kuu.
Hii ni zaidi ya drama,anayetafutwa kuangushiwa zigo ndiye mbuzi wa kafara.
Kilichotokea kwa Lowassa Sasa kinajirudia kwa njia nyingine yenye mfanano wa maudhui. Ndiyo maana nasema kama Kuna udhaifu katika serikali,Rais anawajibika Majaliwa atabaki kuwa mbuzi wa kafara tu uzoefu unatukumbusha.
Ndani ya CCM wa kumvika paka kengele bado HAJAZALIWA,rudini kwa wananchi kujua matatizo yao na suluhisho lake, Ngorongoro na Msomera hiyo ni mmoja lakini msafara wa mamba kenge wamo kibao.