Vita vya kibiashara ni haramu katika Uislamu

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,502
Reaction score
16,716
Rasi Donald Trump wa Marekani anajaribu kadri iwezekanavyo bidhaa kutoka nje ziwe ghali kiasi kwamba wananchi wake wasizipate kwa urahisi ijapokuwa kwake hazipo.Na kinyume chake.

Mu'az amesimulia: Nimemsikia Mtume wa Allah akisema" Mbaya ni yule anayelundika bidhaa na kuifanya iwe adimu. Kama Allah akifanya bidhaa kuwa rahisi, yeye anachukia na kama Allah akiifanya kuwa ghali, anafurahi, (Razin, Baihaqi).

Maangamizo yatawathubutikia wapunjao (wenzao) Ambao wanapojipimia kwa watu hupokea (kipimo) kamili. Lakini wanapowapimia kwa (kipimo cha) vibaba au mizani (au vinginevyo), wao hupunguza. (83:1-3).

Na timizeni kipimo mpimapo; na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni (kwake). (17:35).

Anas amesimulia kuwa wakati mmoja katika wakati wa Mtume wa Allah bei ya vitu ilikuwa ghali. Wakamuomba Mtume: Ewe mtume wa Allah panga bei kwa nafuu yetu. Mtume wa Allah akajibu: Hakika Allah ndiye anayemiliki bei, anapunguza, anatoa kwa wingi, anatoa riziki, na ninapendelea sana nikutane na Bwana wangu katika hali ambayo hapana yeyote kati yenu atakayenifanya niwe na dhima juu ya damu (iliyomwagika kwa sababu yangu) au mali (aliyopunjwa kwa sababu yangu)! (Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).

Hadithi hii inatupa fundisho kubwa kuwa Uislamu kama usivyoruhusu kukandamizwa na kudhulumiwa mnunuzi ndivyo hivyo hivyo isivyoruhusu kukandamizwa kwa mchuuzi au muuzaji.

Mtume (s.a.w.) akiwa kiongozi mkuu wa Serikali ya Kiislamu, hakuthubutu kutumia madaraka hayo na kuingilia haki za wafanya biashara waliopewa na Allah (s.w.).

Jibu lake kwa namna nyingine lilikuwa "anayepanga bei ni Allah (s.w.) kwa bei". Kutokana na hadithi hii hapana yeyote mwenye haki ya kukaa chini na kumpangia mfanya biashara bei iliyo kinyume na ile iliyojitokeza yenyewe sokoni. Kinachotakiwa kifanywe na nguvu za dola ni kutokomeza njama zote za ulanguzi na vikwazo vyote vya uchumi. Kisha kuwaacha huru wafanya biashara wauze bidhaa zao kwa bei halisi inayokubaliwa katika soko huru.
 
Hakuna haram kwenye Uislamu:

Nyama ya Nguruwe ni haram, ukiwa na njaa kula:
Kwani wanaokula nyama ya
Nguruwe walikuambia kuwa wameshiba ?

Biashara zote zinafanywa na Uislamu na Waislamu, na hakuna biashara isiyo na ushindani.

Nyookeni acheni hizo rangi mbili:
 
Acha mdomo huo.Hayo ni maelekezo ya ALlah mwenyewe.
Huna haki ya kubadilisha na hata ukijaribu utaishia kujimaliza mwenyewe
 
Niambie sasa kuna bishara gani mnazozifanya bila ushindani?

Benki za Kiislamu zinaongoza kwa kutoza Riba kubwa:

Allah/Muhamadi aliongea mambo mengi sana yasiyo tekelezeka:
Kwenye hicho Qurani:
 
Nani anataka kujua kuhusu huo ujinga. Na ninan kakuambia hizo bidhaa hazipo marekan
 
Riba ndio kabisa hairuhusiwi na ina makatazo makali zaidi.
Ushindani wa kibiashara upo maeneo mengine sio kufanya ni vita.
 
Nani anataka kujua kuhusu huo ujinga. Na ninan kakuambia hizo bidhaa hazipo marekan
Huo unaouita ujinga ndio umeileta dunia kuwa pahala salama pa kuishi.
Allah kaumba kwa hekima zake na kwa uadilifu mkubwa kila eneo liwe na rasilimali zake ili waja wake wakaribiane
Marekani hawezi kuwa na kila bidhaa kama unavyodai.Zile walizonazo wengine lazima aziagize kwa nidhamu na za kwake asilazimishe wengine wazikose kifisadi.
 
Trump sio muislam sasa why aishi kwa masharti ya kiislam? Mchina na Mkorea nae atakuja na slogan za Buddha kwamba hairuhusu ABCD, then Mhindi nae atakuja na story zake za Hindus kwamba kile na hiki ni makosa; amsikilize nani? Waislamu wanakimbia kwenye nchi zao kwasababu ya shariah law halafu wakifika nchi za kigeni wanataka shariah law tena, hutaki hayo, rudini kwenu. Tanzania jumla ya kodi zinazo lipwa na wafanyabiashara ni kubwa kuliko anacho toza Trump, Tanzania ina Waislamu wengi zaidi kuliko USA (kwa maana ya %), viongozi wa ngazi za juu wenye maamuzi wengi ni Waislamu na hawa practice hiki ulicho kiandika humu, hu kama sio unafiki ni nini? Kwamba haramu kwa uislam wakifanya Wamarekani (ambako Waislamu sio wengi kiviiile kulinganisha na bongo in terms of %) lakini hapa mpo kimya, kule kwa makafiri unahubiri sheria za mashariki ya kati, upuuzi
 
Uislam umeleta usalama Hahahahaa. Mzee kajipange upya. Huyo mwanzilish mwenyewe cku za uhai wake kapigqnisha mavita na kuua watu hovyo na kuoa mpaka kitoto cha miaka 9. Unasemaje wewe
 
Dini ni usanii tu, hakuna sehemu Mungu aliposema kama hauna dini hautauona ufalme wake hata kabla ya ujio wa dini watu walikuwepo na walikuwa wanakufa sasa hao walienda wapi...!!!!
 
Mungu alikuwepo na aliwafundisha watu mambo mema hata kabla ya kuja hizo dini zenu:

Chukulia mfano kwa hawa WAHADZABE tunaowaona leo wanaishi katika misitu ya Tanzania hii yetu:

Wanaishi maisha kama yale ambayo Mungu aliwafundisha watu wakati wa unabii:

Wanaishi maisha ya kistaarabu na matakatifu kabisa na wamejiwekea sheria zao walizo kubaliana na wanafurahia maisha:

Hatuwaoni wakikatana mikono, wala kuchinjana kama baadhi wenye dini wanafanya:

Wanaishi kwa upendo, kuheshimiana na kusameheana na sio kwa jino kwa jino:
Hakuna adhabu za kupigwa mawe hadi kufa:

Na wanayafurahia maisha yao kwa 100%.

Popote penye watu, Mungu yupo pale pia ili kuwaongoza na kuwalinda:

Walimu na Manabii wa Uongo ndio wanao potosha na kuumiza jamii za watu wanao waamini:
Ni kama Wachawi:

Mimi niko radhi kuishi maisha ya WAHADZABE ambayo yanaonekana ni ya kujali ustawi wa Binadamu kuliko kuishi kwenye maisha ya kinafki na ushenzi wa SHARIA LAW:
 
Hakuna haram kwenye Uislamu:

Nyama ya Nguruwe ni haram, ukiwa na njaa kula:
Kwani wanaokula nyama ya
Nguruwe walikuambia kuwa wameshiba ?

Biashara zote zinafanywa na Uislamu na Waislamu, na hakuna biashara isiyo na ushindani.

Nyookeni acheni hizo rangi mbili:
Hebu punguza makasiriko.
 
Trump sio muislam sasa why aishi kwa masharti ya kiislam? Mchina na Mkorea nae atakuja na slogan za Buddha kwamba hairuhusu ABCD, then Mhindi nae atakuja na story zake za Hindus kwamba kile na hiki ni makosa; amsikilize nani? Waislamu wanakimbia kwenye nchi zao kwasababu ya shariah law halafu wakifika nchi za kigeni wanataka shariah law tena, hutaki hayo, rudini kwenu. Tanzania jumla ya kodi zinazo lipwa na wafanyabiashara ni kubwa kuliko anacho toza Trump, Tanzania ina Waislamu wengi zaidi kuliko USA (kwa maana ya %), viongozi wa ngazi za juu wenye maamuzi wengi ni Waislamu na hawa practice hiki ulicho kiandika humu, hu kama sio unafiki ni nini? Kwamba haramu kwa uislam wakifanya Wamarekani (ambako Waislamu sio wengi kiviiile kulinganisha na bongo in terms of %) lakini hapa mpo kimya, kule kwa makafiri unahubiri sheria za mashariki ya kati, upuuzi
Kuna kitu kinakupa tabu katika kichwa chako au hujakubaliana nacho.
Kitu kinapokuwa haramu haiwahusu waislamu peke yao ijapokuwa waislamu wasipotekeleza basi wanakuwa wanatafutia shida kwa makusudi.Hii ni kwa vile uharamu na uhalali umewekwa wazi kwenye dini yao.

Uharamu na madhara ya kufanya kilicho haramu hata akikifanya ambaye si muislamu tuseme mkristo au budha basi ubaya wake hautamuacha hapa duniani na atakuwa anawadhuru wengine ambao wanajiepusha na haramu hiyo.Kwa vile sote tunaishi sayari moja tuliyopangiwa na muumba wetu.

Wewe na mwengine yeyote yule wa dini yoyote ile basi hamna namna ya kuisha mbali na yale yaliyoharamishwa au kuhalalishwa na Mungu (ALLAH) ambayo kwa sasa yapo kwenye Qur'an na suna za Mtume s.a.w

Ni wajibu wa muislamu akiona haramu hizo zinatendeka duniani basi apate hofu kwani madhara yake hayataishia kwa hao wanaotenda peke yao.
 
Dini ni usanii tu, hakuna sehemu Mungu aliposema kama hauna dini hautauona ufalme wake hata kabla ya ujio wa dini watu walikuwepo na walikuwa wanakufa sasa hao walienda wapi...!!!!
Umetajwa kwa urefu kuwa utauona ufalme wake lakini katika namna ya kuchukiza kama utakufa bila kufuata maamrisho yake.
 
Mungu alikuwepo na aliwafundisha watu mambo mema hata kabla ya kuja hizo dini zenu:

Chukulia mfano kwa hawa WAHADZABE tunaowaona leo wanaishi katika misitu ya Tanzania hii yetu:

Wanaishi maisha kama yale ambayo Mungu aliwafundisha watu wakati wa unabii:

Wanaishi maisha matakatifu kabisa na wamejiwekea sheria zao walizo kubaliana na wanafurahia maisha:

Hatuwaoni wakikatana mikono, wala kuchinjana kama baadhi wenye dini wanafanya:

Wanaishi kwa upendo, kuheshimiana na kusameheana na sio kwa jino kwa jino:
Hakuna adhabu za kupigwa mawe hadi kufa:

Na wanayafurahia maisha yao kwa 100%.

Popote penye watu, Mungu yupo pale pia ili kuwaongoza na kuwalinda:

Walimu na Manabii wa Uongo ndio wanao potosha na kuumiza jamii za watu wanao waamini:
Ni kama Wachawi:
Sio kweli.Unajipa moyo tu na kupambiwa na shetani kuwa upo sahihi.
 
Mungu alikuwepo na aliwafundisha watu mambo mema hata kabla ya kuja hizo dini zenu:

Chukulia mfano kwa hawa WAHADZABE tunaowaona leo wanaishi katika misitu ya Tanzania hii yetu:

Wanaishi maisha kama yale ambayo Mungu aliwafundisha watu wakati wa unabii:

Wanaishi maisha matakatifu kabisa na wamejiwekea sheria zao walizo kubaliana na wanafurahia maisha:

Hatuoni wakikatana mikono wala kuchinjana kama ya baadhi wenye dini:

Wanaishi kwa upendo, kuheshimiana na kusameheana na sio kwa jino kwa jino:

Na wanayafurahia maisha yao kwa 100%.

Popote penye watu, Mungu yupo pale pia ili kuwaongoza na kuwalinda:

Walimu na Manabii wa Uongo ndio wanao ziumiza jamii za watu:
Ni kama Wachawi:
Acheni kuwadanganya hao washamba, Wahazabe na Wamasai ni aibu kwa Taifa, wanahitaji kufundishwa ustaarabu, mambo ya kunya vichakani na kujisiriba kwa majani na kulala mapangoni, kujizonga mashuka na kuvaa ngozi za wanyama ni ushamba dunia imesha ondoka huko, acheni kuwadanganya waelemisheni waje waishi nyumba bora wapige pamba wa enjoy maisha, waache kuishi kama wanyama.
 
Anyway, the US is not a muslim country which makes your comments completely irrelevant.
 
Back
Top Bottom