Kwanini awe sahihi kumshambulia wakati yeye Marekani pia anamiliki?
Yaani wewe uwe na haki ya kumiliki nyuklia halafu mwenzako asiwe na haki hiyo hiyo?
Kama ni nchi iliyopaswa kupogwa marufuku kutokumiliki nyuklia basi ni Marekani kwasababu yeye ndiye nchi pekee iliyowahi kutumia nyuklia dhidi ya raia wasio na hatia.
Marekani, China, Urusi, Ufaransa pamoja na Uingereza hayo ni mataifa ambayo tangu mwanzo yalikuwa yana miliki Nuclear kabla hata ya 1967 ambapo huo mkataba kusainiwa.
Makubaliano ya huo mkataba yalikuwa ni kuzuia uongezekaji wa silaha za Nuclear, hivyo wakaafikiana kuwa technology ya nuclear itumike katika kuzalisha nuclear kwa ajili ya matumizi salama kama maswala ya nishati na mambo mengine ambayo ni useful kijamii.
Mtataba haukuwa ni kuondoa silaha za Nuclear kwa nchi ambazo tayari zinamiliki, bali ilikuwa ni Nchi zisizokuwa na silaha (kama Iran) zilikubali kutotengeneza au kupata silaha za nyuklia.
Na zile nchi ambazo zilikuwa tayari zinamiliki hizo silaha (Marekani, UK, france, China na Urusi) ziliruhusiwa kuendelea kubaki na nuclear kwasababu walikuwa nazo kabla ya 1967 lakini zilikubali kufanya mazungumzo ya kupunguza na mwisshowe kuziondoa kabisa.
Mapungufu ya huu mkataba yapo eneo hili
Hayakuweka muda rasmi wa deadline kwa kila nchi kufikia ukomo wa hayo matumizi ya nuclear ili kuhakikisha kuwa pindi tu baada ya kufika tarehe hiyo basi kila nchi iwe haina silaha za nuclear.
Hii inafanya hata wakiulizwa wapate majibu mepesi tu kuwa tunaendelea kupunguza kwasababu hawabanwi na sehemu yeyote kuwa wamevuka ukomo wa muda uliowekwa.